Afande Sele atashtakiwa kwa kosa gani baada ya kumtukana Mungu?

Afande Sele atashtakiwa kwa kosa gani baada ya kumtukana Mungu?

Atashtakiwa Kwa kosa kama la nabii Tito. Anochafanya ni dhihaka Kwa wanaoamini ambayo inaweza sababusha uvunjifu WA Amani.
 
Kuna watu waliwahi kuimba wakimlaumu mungu kwanini ameruhusu mabaya yawafike.Sijui wanaitwa Ambasadors.Wale jamaa walisema kama alivyosema Afande sele ila Tofauti ni kuwa wao hawakuvuta bangi Kwahiyo wakajizuia kutukana
 
Haya ndiyo Mtume aliyasema, yaani watu wajinga wajinga wanaisemea dini na kufanya maamuzi kama haya. Sasa sijui huu ujinga wameuota wapi, Mtume alikuwa anawapa nasaha na kuwaombea kheri Allah awaongoze watu hawa.

Ukiangalia kwa jicho la kielimu jambo alilofanya Afande Sele limekubikwa na ujinga wake ndiyo maana baadae nimekuja kusikia kwamba ameomba radhi.
Kukosea kupo na yeye Kiskhi anaweza kukosea kama mwanadamu ila kumuita ' mjinga mjinga' mtu kama yule anayefanya kazi kubwa na ameshajijengea heshima miongoni mwa watu kwangu mimi naona siyo fair.
 
Kukosea kupo na yeye Kiskhi anaweza kukosea kama mwanadamu ila kumuita ' mjinga mjinga' mtu kama yule anayefanya kazi kubwa na ameshajijengea heshima miongoni mwa watu kwangu mimi naona siyo fair.
Nachokidema nakijua kaka, nina sehemu nimerejea.
 
Amesemaje, ametukana nini?

Mungu akitukanwa aachwe ajitetee, kama hawezi kujitetea mwenyewe basi hayupo.

Mungu ndie aliemashauri jpm asichukue tahadhari? Kama ni yeye basi alaumiwe na kama sio yeye basi marehemu alaumiwe kwa uzembe.
Magu hakufa kwa corona Bali marafhi ya moyo
 
Umeongea logic sana mkuu[emoji109]
Hili jambo ni la hatari. Linaweza shawishi mauaji to prove a point sababu ya ushindani.

Kama MUNGU amekasirika atamuadhibu kwa namna anayoona YEYE na ujumbe utafika. Si lazima kumshawishi mbele ya makamera.
 
Nachokidema nakijua kaka, nina sehemu nimerejea.
Ok sawa , ila Mtume Muhammad (saw) alikuwa akiwaelekeza maswahaba zake kwa lililo bora katika majambo mbalimbali bila kumdhohofisha kutokana na fikra zao mfano mara nyingi rai za Umar ibn Khattab (r.a) juu ya maadui wakubwa wa kiislamu wanapotiwa nguvuni alikuwa anapendekeza kuuliwa kutokana na mapenzi makubwa na uchungu mkubwa alionao ktk dini lakini alielekezwa taratibu kwa lililokuwa bora zaidi.
 
Sasa hili kwanini limemshinda Kishki na akakurupuka kurupu kwenda kumuombea dua mbaya muhusika, wakati alipaswa kurudi katika mapito ya Mtume na maswahaba kumpa nasaha muhusika ?

Au alichokifanya Kishki ni sawa ? Sasa hawa masheikh waache kukurupuka na anatakiwa ya wapo masheikh wenye elimu kumzidi yeye, wamekaa kimya.
 
Mungu aje amjbu mwenyewe bhana

Tunachoka kila siku kumtete

Ps: naamini Mungu yupo
 
Back
Top Bottom