Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani Afande sele havioni vituo vya Afya, zahanati, shule na huduma za maji na umeme vikijengwa ,kuboreshwa na kusambaza kila kukicha, mbona hata huku niliko Mimi naendelea kuona huduma karibu yangu huku wananchi wakiendelea kufurahia na kuridhishwa na namna fedha zilivyotumika, au yeye yupo wapi huko ambako haoni namna mh Rais alivyofanya kazi kubwa katika ujenzi wa miradi mbalimbali iliyosaidia pia kutoa ajira kwa vijana hasa wa maeneo husika
Tozo zinajulikana matumizi yake maana sisi wananchi tunaona miradi mbalimbali ikijengwa na kuboreshwa, tunaona namna huduma zinavyosogezwa karibu yetu, Tunafurahi kuona tukiijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyeweAfande sele ni moja ya wasanii wanaojitambua sana
Wananchi wanaweza kuwa hawachukii tozo ila ni jinsi zutakavyotumika
Kwani Afande sele havioni vituo vya Afya, zahanati, shule na huduma za maji na umeme vikijengwa ,kuboreshwa na kusambaza kila kukicha, mbona hata huku niliko Mimi naendelea kuona huduma karibu yangu huku wananchi wakiendelea kufurahia na kuridhishwa na namna fedha zilivyotumika, au yeye yupo wapi huko ambako haoni namna mh Rais alivyofanya kazi kubwa katika ujenzi wa miradi mbalimbali iliyosaidia pia kutoa ajira kwa vijana hasa wa maeneo husika
Miradi yote ya serikali inayojengwa na iliyojengwa kila Kona ya nchi yetu inasaidia pia katika mzunguko wa fedha maana wajenzi na wasimamizi wake Ni watanzania hasa vijana, miradi hii inatoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, kiufupi wananchi wengi tunanufaika na uwepo wa miradi hii karibu yetu,Akili kubwa sana.
TOZO sawa lakini tuone miradi pesa zetu zinapoendea. Na mtu wakutueleza na kutuonyesha mradi huu zimetokana na pesa fulani. Magu alikuwa anatuonyesha kwa vitendo na tukibanwa kwenye tozo tunaridhika.
Nakumbuka kipindi cha Magu pesa mtaani kuanzia tarehe 20 hadi mwisho wa mwezi pesa mtaani zilikuwa zinaonekana ila huyu hatari 27 week end pesa hamna mtaani. Mzunguko wa pesa mtaani hamna,kama kungekuwa na miradi tungeziona pesa mtaani.
Kwa akili yako kisoda unataka kila mtu asafiri kuzunguka nchi kuona hayo unayosema? Kama ni kweli yapo si wajitokeze wasema makusanyo kwa mwezi ni kiasi gani na zimetumika wapi na wapi? Alafu watu tulinganishe thamani ya tozo tunazokatwa
Msipende kuupotosha huu msemo wa kula kwa urefu wa kamba yako....kwani Kuna tatizo kula kulingana na urefu wa kamba yangu?kamba yangu ni kipato changu NI mshahara wangu,urefu wake NI laki 6 kwa mwezi ,lazima NIISHIE hapo,maana huo ndio urefu wa kamba yangu...SASA MNATAKA NILE KWA UREFU WA KAMBA YA MWENZANGU?(HIYO NDIYO RUSHWA SASA,NDIYO MATUMIZ MABAYA YA MADARAKA YAKO)Ujinga sana huu,mkuu anasema wale kwa urefu wa kamba zao,hiyo kauli ilibidi isitoke kinywani mwake,tuhurumiwe jamani,maisha magumu sana,TAMISEMI wametutema,SENSA wametutema,koneksheni zinatamalaki,mitaji ndiyo hivyo,halafu kinachouma zaidi ni waliobahatika kuingia kwenye system wanavyozidi kuzitafuna hela,sisi ambao toka miaka ya 2016,tuko mtaani,ajira Hanna,inatuuma sana,basi tu.
Usijifanye kama vile umepata uraia wa Tanzania leo,ulijiuliza kwanini 'MKUU aliwaambia kua NAJUA MNAKULA KWENYE MAENEO YENU' akawasihi wasivimbiwe,ulijiuliza kua mtu anaweza akavimbiwa mshahara?Msipende kuupotosha huu msemo wa kula kwa urefu wa kamba yako....kwani Kuna tatizo kula kulingana na urefu wa kamba yangu?kamba yangu ni kipato changu NI mshahara wangu,urefu wake NI laki 6 kwa mwezi ,lazima NIISHIE hapo,maana huo ndio urefu wa kamba yangu...SASA MNATAKA NILE KWA UREFU WA KAMBA YA MWENZANGU?(HIYO NDIYO RUSHWA SASA,NDIYO MATUMIZ MABAYA YA MADARAKA YAKO)