Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

Huo mchezo ulikuwepo na Magomeni pia
Salaam Wakuu,

Polisi wana mbinu nyingi za kutengeneza mazingira ya Rushwa na kukupiga faini. Huwezi pona kwenye 18 zao, watatafuta kosa hadi walipate.

Sitaki kusema Chuo cha Polisi Moshi (CCP) hawafundishi ila nadhani wanatakiwa kubadili Mitaala yao. Kuna vitu wanavifanya Polisi wetu hadi unajiuliza huko CCP walienda kusoma Ujinga? Polisi wanatakiwa watoe huduma sababu ni Watumishi wa Umma.

Rais Samia kaongeza Mshahara ili mfanye kazi kwa Tabasamu, sasa hasira za nini?

Mfano: Kuna askari pale Stesheni (maeneo ya Central/TRA (kwenye Zebra)) ana watu wake wa kukatiza zile zebra ili apige watu fine. Anaitwa WP 4548 CPL Veronica, ayafanyayo anakosea na kudhalilisha Jeshi letu.

Unaweza kuwapisha watu, utakaa hadi waishe, ukianza kuondoka ghafla utaona anaibuka mtu na kutaka kukatiza zebra. Anafanya timing, Ukianza kuondoka anapita anakimbia na Vero anakupiga Mkono. Anakuwa na wenzake wawili. Unaulizwa Kwanini huheshimu watumiaji wengine wa barabara? Anakupiga fine.

Mimi ninahofu, wale jamaa wanatengenezwa? Kwanini wao tu ndo wakatize kwa kuchelewa siku zote?

Pili: Polisi wanatakiwa Wasimamishe Magari ili watu wavuke na wakishaisha wawaruhusu muondoke. Lakini wao wanasimama pembeni pale, Nyie madereva Mtajisimamisha wenyewe watu wavuke na wakishavuka mnajiruhusu wenyewe. Hapo ndipo kwenye mtego wa kuliwa hela.

Polisi tunaomba msaada wenu, mtusaidie muwapo kazini. Sababu Polisi kazi sio kupiga fine tu bali hata kutoa elimu ya barabarani kwa watumiaji wa barabara.

Polisi na Raia ni Ndugu, tushirikiane. Tusiishi kama paka na panya.
Mm mwenyewe imekwisha nitokea hii
 
kila fine 5000
Kama ni kweli hii sio sahihi,kuna trafiki anaitwa john uwa anajificha kutokea mtaa wa swahili kuingia msimbazi road la mwendokasi,aitakiwi kukunja pale unatakiwa kunyosha kama unaenda sokoni kariakoo unatokea mnadani unaingia tena msimbazi,kwa kutokea mnadani kunakuwaga na jam hata lisaa unaweza kujikuta umekwama huko,sasa uwa wanakwepa kuingia kule,huyo trafiki badala ya kwenda kule ndani kuongoza magari yeye ujificha kusubiria wataovunja sheria ili awaandikie,yule trafiki atakufa kifo kibaya sana kwa ile dhulma anayoifanya pale
 
Back
Top Bottom