Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

sasa gari moja unakuja kupiga kelele hapa!!!ushawahi sikia mwenye dala dala analia lia na traffic?

hela huna road unatembea kiwaki,lazima uliwe kichwa.
Daladala zinatoa hesabu ya siku, kuna njia asubui daladala zote utoa hela ya brush ya siku so wanakuwa huru kuivunja Sheria hadi kesho yao tena asubui hela yao imeisha siku inaanza upya.

Ukitunga sheria yeyeto means umewatengenezea pesa wasimamia sheria. Hata TRA wapo unatumwa dukani kanunue usidai risiti kisha unawalengesha wanavuta pesa kwa mwenye duka unapewa percentage yake.

Kuna idara kuna vishoka Ili upate huduma hata ukienda ubalozini kuomba viza maadamu yupo mswahili utazungushwa ukitumia agent dakika.

Suala la uadilifu ni msiba kwa watz maana nao uiga toka kwa viongozi wa juu.
 
AAMU INARUHUSU YOTE HAYA NA BADO MENGI TUTAYAONA
 
Salaam Wakuu,

Polisi wana mbinu nyingi za kutengeneza mazingira ya Rushwa na kukupiga faini. Huwezi pona kwemye 18 zake.

Sitaki kusema Chuo cha Polisi Moshi (CCP) hawafundishi ila nadhani wanatakiwa kubadili Mitaala yao. Kuna vitu wanavifanya Polisi wetu hadi unajiuliza huko CCP walienda kusoma Ujinga? Polisi wanatakiwa watoe huduma sababu nu Watumishi wa Umma.

Rais Samia kaongeza Mshahara ili mfanye kazi kwa Tabasamu, sasa hasira za nini?

Mfano: Kuna askari pale Stesheni (maeneo ya Central/TRA (kwenye Zebra)) ana watu wake wa kukatiza zile zebra ili apige watu fine. Anaitwa WP 4548 CPL Veronica, ayafanyayo anakosea na kudhalilisha Jeshi letu.

Unaweza kuwapisha watu, atakaa hadi waishe, ukianza kuondoka ghafla utaona anaibuka mtu na kutaka kukatizazebra. Anafanya timing, Ukianza kuondoka anapita anakimbiwa na Vero anakupiga Mkono. Anakuwa na wenzake wawili. Unaulizwa Kwanini huheshimu watumiaji wengine wa barabara? Anakupiga fine.

Mimi ninahofu, wale jamaa wanatengenezwa? Kwanini wao tu ndo wakatize kwa kuchelewa siku zote?

Pili: Polisi wanatakiwa Wasimamishe Magari ili watu wavuke na wakishaisha wawaruhusu muondoke. Lakini wao wanasimama pembeni pale, Nyie madereva Mtajisimamisha wenyewe watu wavuke na wakishavuka mnajiruhusu wenyewe. Hapo ndipo kwenye mtego wa kuliwa hela.

Polisi tunaomba msaada wetu, mtusaidie muwapo kazini. Sababu Polisi kazi sio kupiga fine tu bali hata kutoa elimu ya barabarani kwa watumiaji wa barabara.

Polisi na Raia ni Ndugu, tushirikiane. Tusiishi kama paka na panya.
 
Mwambie huyo afande kama ana shida ya pesa aje achukue asiwaonee madereva wengi magari sio yao anawapa msongo wa mawazo.
 
Hiyo fine mnampa cash au anawaandikia?

Kama ni cash na mazingira ndiyo hayo, uwezekano wa kuwa mchezo upo!

Kama anaandika fine,then ananufaikaje na waigizaji anawalipaje?

Kuna commission anapewa kwa wingi wa fine alizoandika?
Yawezekana hujui, polisi wana kamisheni kwa kila fine atakayoandika, nao hulipwa 3000/- kwa kila fine. Hulipwa mwisho wa mwezi. Akipiga fine watu 20 kwa siku mara 3000 mara 30 anapata 1,200,000/- cash kwa mwezi bado rushwa na mshahara.
Acha u traffic uuzwe tuu kule CCP.
 
Kwenye zebra unatakiwa usimame bila kusimamishwa hata kama hamna mtu anaetaka kuvuka ukijiridhisha hamna mtu karibu ndo unaendelea na safari Kama hulijui hilo iko siku utapigwa faini kwa kupita kwenye zebra bila kusimama hata Kama hamna mtu ndo utashangaaa zaidi
Hivi hii ni sheria ya wapi. Mbona mnadanganya watu hivyo? Hii sheria ya kusimama zebra kila nikifka haipo na Kuna siku wamenikamata niliwakatalia na sikuawapa lesen make ukisha wapa lesen tayari umejipiga kitanzi. Tulienda Hadi kwa RCO. Haipo ni uonevu wao tu

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Ninajiuliza sana swali hili- - Kwanini polisi wanapenda sana hela ? Kuna wengine wanapokea hata rushwa ya elfu moja toka kwa wapiga debe. Inanisikitisha.
ukitaka kujua buku ni nyingi,inamtoa mtu mbagala mpaka morocco.

hiyo buku akichukua kwa makonda 50 kwa siku tayari ni balaa.
usipige hesabu kivivu namna hiyo.
 
najua utaanza kusema tushajua una gari
basi nikuambie mie dereva tu nawaandesha WAHINDI mshahara 250000/=

haya turudi kwenye MADA kama sio dereva huwezi kujua adha ya TRAFFIC anachosema ndio kipo na hiyo MICHEZO sio hapo tu ipo sehemu nyingi.

Usione watu wajinga walipofurahia yule TRAFICC morocco aitel kuporomoshewa MITUSI ya nguoni na dreva daladala.

Hao jamaa ni wapuuzi AKILI zao zimejaa pesa zaidi kuliko kuongoza magari
jana nimepanda daladala dereva kasimamishwa mataa ya chang'ombe kawa mkali kama pili pili kichaa,yule mama anamwambia kwanini unakimbia bila tahadhali na umejaza watu namna hii,abiria wanajibu (sisi hatujalalamika).watz wengi ni viazi yaani wasikupe nguvu wapigapo kelele kumzomea mtu,wanaongozwa na upumbavu mwingi.
jamaa alikuwa anakimbia sana nusu agonge bodaboda mwenye abiria pale relini karume.

kama una kumbu kumbu hamza anaitwa shujaa leo,wacha kesho kichaa mwingine aue askari na raia utasikia story tofauti kabisa.

traffic wanapenda hela hilo liko wazi,ni wewe kuchagua-kuuwanyima rushwa uchukue risiti ya 30k au kujisimamia barabarani,simple.
 
Salaam Wakuu,

Polisi wana mbinu nyingi za kutengeneza mazingira ya Rushwa na kukupiga faini. Huwezi pona kwemye 18 zake.

Sitaki kusema Chuo cha Polisi Moshi (CCP) hawafundishi ila nadhani wanatakiwa kubadili Mitaala yao. Kuna vitu wanavifanya Polisi wetu hadi unajiuliza huko CCP walienda kusoma Ujinga? Polisi wanatakiwa watoe huduma sababu ni Watumishi wa Umma.

Rais Samia kaongeza Mshahara ili mfanye kazi kwa Tabasamu, sasa hasira za nini?

Mfano: Kuna askari pale Stesheni (maeneo ya Central/TRA (kwenye Zebra)) ana watu wake wa kukatiza zile zebra ili apige watu fine. Anaitwa WP 4548 CPL Veronica, ayafanyayo anakosea na kudhalilisha Jeshi letu.

Unaweza kuwapisha watu, atakaa hadi waishe, ukianza kuondoka ghafla utaona anaibuka mtu na kutaka kukatizazebra. Anafanya timing, Ukianza kuondoka anapita anakimbiwa na Vero anakupiga Mkono. Anakuwa na wenzake wawili. Unaulizwa Kwanini huheshimu watumiaji wengine wa barabara? Anakupiga fine.

Mimi ninahofu, wale jamaa wanatengenezwa? Kwanini wao tu ndo wakatize kwa kuchelewa siku zote?

Pili: Polisi wanatakiwa Wasimamishe Magari ili watu wavuke na wakishaisha wawaruhusu muondoke. Lakini wao wanasimama pembeni pale, Nyie madereva Mtajisimamisha wenyewe watu wavuke na wakishavuka mnajiruhusu wenyewe. Hapo ndipo kwenye mtego wa kuliwa hela.

Polisi tunaomba msaada wetu, mtusaidie muwapo kazini. Sababu Polisi kazi sio kupiga fine tu bali hata kutoa elimu ya barabarani kwa watumiaji wa barabara.

Polisi na Raia ni Ndugu, tushirikiane. Tusiishi kama paka na panya.
Nasikia kwa kila faini inayotolewa, kuna percent inaenda kutoka hazina kwenda kwa huyo polisi mtoa faini.
 
Wametanda kuanzia fire hadi kimara Temboni, ni usimamisha magari na komba hela.
 
Back
Top Bottom