Afanyeje ili aweze kumsahau mwanaume anayempenda na kuendelea na maisha yake?

Afanyeje ili aweze kumsahau mwanaume anayempenda na kuendelea na maisha yake?

Fine Wine

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2023
Posts
595
Reaction score
1,686
Habari yako,

Mimi ni binti wa miaka 23, nipo chuo mwaka wa pili. Kuna kitu kinaniumiza sana kichwa kiasi kwamba kuna muda nashindwa hata kusoma vizuri. 🥹🥹 Kuna mkaka mmoja tulikutana tu kawaida kipindi mimi ndo naanza form five, lakini mpaka namaliza form six bado nilikuwa naye.

Sasa baada ya mimi kwenda jeshini maana nilipangiwa nikaenda, lakini nilikuwa na simu na tulikuwa tunawasiliana vizuri tu mpaka akaniambia amehamishiwa kikazi mkoa mwingine. Mimi nikamwambia hamna shida, nikienda chuo tutaonana. Mapenzi yakawa yanaendelea kama kawaida. Nilipomaliza jeshi kweli nikaenda chuo Dar es Salaam, lakini baada ya kufika chuo mabadiliko nilianza kuyaona mwenyewe. Mara akae wiki hajanitafuta, mara nimuulize anakuwa na visingizio vingi sana. Namsamehe, inaisha. Yote hayo nilikuwa naona kawaida tu.

Lakini kilichokuja kuniumiza kichwa ni kwamba huyu mwanaume ni wa ajabu sana kwani hayupo tayari kunisaidia kwa pesa yoyote ile. Yeye anachotaka ni nimwambie "nimekumiss" na yeye ajibu "nimekumiss pia" basi maisha yasonge. Mpaka kuna muda najiuliza au shida ni nini kwa sababu yeye haongelei mambo ya mapenzi kabisa na huwa ananikwepa nikileta hizo mada.

Juzi nilimpigia, nikajifanya kumwambia baba kanipigia anaumwa nione atakavyonijibu. Alijibu "pole, atakuwa sawa"... na hajawahi kuniuliza anaendeleaje hata siku moja. Ananikosea sana kwa sababu vocha ninunue mwenyewe, nimpigie, bado hajali kabisa.

Na text zake zote ananiita mke wake. Nimeshajaribu mara kadhaa kumuacha lakini sijui huwa ni kwa nini nashindwa. Unakuta kanikosea yeye lakini mimi ndo namuomba msamaha. Ni mtu wa kukasirika mapema sana.

Nina miaka mitatu nipo naye.

Kwa nyie wenzangu huwa mnatumia mbinu gani kumuacha mtu unayempenda kweli 😭😭😭 bila kumuambia 😭

Tafadhali naomba unipostie pia naomba ufiche jina langu.
 
Natoa dawa ya kumvuta mpenzi ulio achana nae au mtu aliyepo mbali, atakufuata mwenyewe

dawa hii natoa bure.. Narudia ni BURE Kwa atakaye hitaji

baada ya kurudi huyo mtu. Uje uniambie asante

dawa itakayofuata ni kumfanya akupende hadi ashindwe kwenda kazini na kushindwa kuchepuka nje. Dawa hii inauzwa kwa $€
 
Natoa dawa ya kumvuta mpenzi ulio achana nae au mtu aliyepo mbali, atakufuata mwenyewe

dawa hii natoa bure.. Narudia ni BURE Kwa atakaye hitaji

baada ya kurudi huyo mtu. Uje uniambie asante

dawa itakayofuata ni kumfanya akupende hadi ashindwe kwenda kazini na kushindwa kuchepuka nje. Dawa hii inauzwa kwa $€
Dawa ni kuwa na pesa ukiwa na pesa anakuja mwenyewe, (anajivuta) mwenyewe
 
Soma kwanza ukimaliza masomo utakuwa umepata namna nzuri ya kumuacha ila saivi hutaweza maana bado uwezi wako wa kufikiri ni mdogo sana

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Mapenzi ni kama ugonjwa wa akili

ktk pitapita za maisha nilikutana na jamaa mmoja hv, demu wake alikuwa akija yeye ndio anapika, anaosha vyombo, anafagia. Nikamuliza kwa nini shemu asikusaidie jibu alilonipa nikaona jamaa ni mshamba wa mapenzi
 
At that age she is still young, focus kwenye masomo, pata kazi kwanza au fungus business, akihamishia attention yake huko atasahau overtime, but safari haitokuwa rahis
 
Back
Top Bottom