Afanyeje ili aweze kumsahau mwanaume anayempenda na kuendelea na maisha yake?

Habari yako,

Mimi ni binti wa miaka 23, nipo chuo mwaka wa pili. Kuna kitu kinaniumiza sana kichwa kiasi kwamba kuna muda nashindwa hata kusoma vizuri. 🥹🥹 Kuna mkaka mmoja tulikutana tu kawaida kipindi mimi ndo naanza form five, lakini mpaka namaliza form six bado nilikuwa naye.

Sasa baada ya mimi kwenda jeshini maana nilipangiwa nikaenda, lakini nilikuwa na simu na tulikuwa tunawasiliana vizuri tu mpaka akaniambia amehamishiwa kikazi mkoa mwingine. Mimi nikamwambia hamna shida, nikienda chuo tutaonana. Mapenzi yakawa yanaendelea kama kawaida. Nilipomaliza jeshi kweli nikaenda chuo Dar es Salaam, lakini baada ya kufika chuo mabadiliko nilianza kuyaona mwenyewe. Mara akae wiki hajanitafuta, mara nimuulize anakuwa na visingizio vingi sana. Namsamehe, inaisha. Yote hayo nilikuwa naona kawaida tu.

Lakini kilichokuja kuniumiza kichwa ni kwamba huyu mwanaume ni wa ajabu sana kwani hayupo tayari kunisaidia kwa pesa yoyote ile. Yeye anachotaka ni nimwambie "nimekumiss" na yeye ajibu "nimekumiss pia" basi maisha yasonge. Mpaka kuna muda najiuliza au shida ni nini kwa sababu yeye haongelei mambo ya mapenzi kabisa na huwa ananikwepa nikileta hizo mada.

Juzi nilimpigia, nikajifanya kumwambia baba kanipigia anaumwa nione atakavyonijibu. Alijibu "pole, atakuwa sawa"... na hajawahi kuniuliza anaendeleaje hata siku moja. Ananikosea sana kwa sababu vocha ninunue mwenyewe, nimpigie, bado hajali kabisa.

Na text zake zote ananiita mke wake. Nimeshajaribu mara kadhaa kumuacha lakini sijui huwa ni kwa nini nashindwa. Unakuta kanikosea yeye lakini mimi ndo namuomba msamaha. Ni mtu wa kukasirika mapema sana.

Nina miaka mitatu nipo naye.

Kwa nyie wenzangu huwa mnatumia mbinu gani kumuacha mtu unayempenda kweli 😭😭😭 bila kumuambia 😭

Tafadhali naomba unipostie pia naomba ufiche jina langu.
kwani baba yako huyo mpaka kukupa hela ya matumizi iwe lazima, uko chuo unapewa boom tumia vizuri likusaidie
 
Natoa dawa ya kumvuta mpenzi ulio achana nae au mtu aliyepo mbali, atakufuata mwenyewe

dawa hii natoa bure.. Narudia ni BURE Kwa atakaye hitaji

baada ya kurudi huyo mtu. Uje uniambie asante

dawa itakayofuata ni kumfanya akupende hadi ashindwe kwenda kazini na kushindwa kuchepuka nje. Dawa hii inauzwa kwa $€
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtu uko chuoni afu unahangaishwa na mapenzi uko serious?? Si uwe buzz na masomo, mapenzi yapoo tyuuh. Lol
 
Inawezekanaa kweliii?
Inawezekana vizuri si unalipotezea tyuu.!! Unaanza kuruhusu watu wapya kwenye maisha yako.!! Unajua kuna watu hupita kwenye maisha yetu kutupa funzo, hiyo ndio kazi ya universe. Ila sisi na ubishi wetu tunaforce mambo.!!
Unaweza kusema “mimi kwa huyu mwanaume siwezi kumpata mwingine kama yeye” kumbe huyo ni cha mtoto kwa mwanaume ambaye ndiye hatma yako.
Kumng’ang’ania mtu asiyekuhitaji ni kujifungia Bahati zako na kujichelewesha kule unakotakiwa kuwepo kwa ukiziwi na upofu wako.!!
 
Uduguuu hili Dini ni Almas afu linawakaa balaaa, tishaa sanaaa!!
[emoji482][emoji482][emoji482][emoji482]
 
Ukweli ndio huo uduguu, tunajichelewesha sana kukumbatia watu ambao sio sahihi kwetu.!! Inatakiwa turuhusu hatma ifanye kazi yake.
 
sitakuwa na mengi ya kusema zaidi ya
pole sana jitahidi kunywa maji mengi
 
Habari yako,

Mimi ni binti wa miaka 23, nipo chuo mwaka wa pili. Kuna kitu kinaniumiza sana kichwa kiasi kwamba kuna muda nashindwa hata kusoma vizuri. 🥹🥹 Kuna mkaka mmoja tulikutana tu kawaida kipindi mimi ndo naanza form five, lakini mpaka namaliza form six bado nilikuwa naye.

Sasa baada ya mimi kwenda jeshini maana nilipangiwa nikaenda, lakini nilikuwa na simu na tulikuwa tunawasiliana vizuri tu mpaka akaniambia amehamishiwa kikazi mkoa mwingine. Mimi nikamwambia hamna shida, nikienda chuo tutaonana. Mapenzi yakawa yanaendelea kama kawaida. Nilipomaliza jeshi kweli nikaenda chuo Dar es Salaam, lakini baada ya kufika chuo mabadiliko nilianza kuyaona mwenyewe. Mara akae wiki hajanitafuta, mara nimuulize anakuwa na visingizio vingi sana. Namsamehe, inaisha. Yote hayo nilikuwa naona kawaida tu.

Lakini kilichokuja kuniumiza kichwa ni kwamba huyu mwanaume ni wa ajabu sana kwani hayupo tayari kunisaidia kwa pesa yoyote ile. Yeye anachotaka ni nimwambie "nimekumiss" na yeye ajibu "nimekumiss pia" basi maisha yasonge. Mpaka kuna muda najiuliza au shida ni nini kwa sababu yeye haongelei mambo ya mapenzi kabisa na huwa ananikwepa nikileta hizo mada.

Juzi nilimpigia, nikajifanya kumwambia baba kanipigia anaumwa nione atakavyonijibu. Alijibu "pole, atakuwa sawa"... na hajawahi kuniuliza anaendeleaje hata siku moja. Ananikosea sana kwa sababu vocha ninunue mwenyewe, nimpigie, bado hajali kabisa.

Na text zake zote ananiita mke wake. Nimeshajaribu mara kadhaa kumuacha lakini sijui huwa ni kwa nini nashindwa. Unakuta kanikosea yeye lakini mimi ndo namuomba msamaha. Ni mtu wa kukasirika mapema sana.

Nina miaka mitatu nipo naye.

Kwa nyie wenzangu huwa mnatumia mbinu gani kumuacha mtu unayempenda kweli 😭😭😭 bila kumuambia 😭

Tafadhali naomba unipostie pia naomba ufiche jina langu.
Huyo mwanaume kumbe ameona tatizo nini. Kumbe ulitaka awe anakusaidia pesa? Ndo baba yako? Ndo yeye anakusomesha? Halafu unataka amhudumie babayo tena? Umekuja kutuuzia chai?
 
Hizi mada zenu mnazotoa fesibuku na insta na kuzileta huku sijui huwa mnakua na maana gani aisee.
Ajabu ukute mleta uzi wala hamjui huyo alieomba msaada
 
Sasa baba anaumwa nyumbani hamna wanaomba,baba wendigo,baba wakubwa ,shangazi mchangishane na mtu hajakuoa unampa majukumu ya familia .Ungetoa taarifa tu kwake anaumwa na usiexpect chochote maana kulia shida za familia kama kipimo haijakaa sawa.
 
Back
Top Bottom