Tetesi: AFCON 2027 huenda ikapelekwa South Africa

Tetesi: AFCON 2027 huenda ikapelekwa South Africa

Tukiwa tunapambana na Ripoti ya Jaji Chande. Huenda AFCON 2027 ikapelekwa Bondeni kutokana na na maandalizi duni. Viwanja bado, hoteli duni, barabara hoi.

**Tujiandae kwenda bondeni.
Afcon itachezwa africa mashariki,iwe iwavyo
 
Hizo habari zinakuzwa sana huko instagram na watu ambao hawajui chochote kuhusiana na maandalizi ya michuano ya afcon mwakani.

Wale jamaa wenye kusambaza habari negative wapo mbele katika kutamani michuano ihamishiwe South Africa.
Wanaitwa haters hao. Na kadiri Mama Samia anavyopiga hatua za kimaendeleo, ndivyo haters wanavyozidi kuongezeka. Jambo la kufurahisha ni kwamba wote wanaenda kushindwa vibaya!
 
Huyo kama sio Mange itakuwa vijana wa chadema
Chadema wamekula hela za uwanja wa Arusha.
HCoiAwGXcAAme-0.jpeg
 
Kupoteza fursa za biashara hakumkomoi mwanasiasa kwa kiwango sawa na raia wa kawaida anapopoteza fursa. Ugeni wa Afcon ni fursa nzuri ya biashara.
Mafisadi wenyewe ndo wanahujumu fursa ya Afcon
Hao wahuni wamekula mabilion ya uwanja wa Arusha
 
  • Masikitiko
Reactions: Tsh
Kupoteza fursa za biashara hakumkomoi mwanasiasa kwa kiwango sawa na raia wa kawaida anapopoteza fursa. Ugeni wa Afcon ni fursa nzuri ya biashara.
Mwenye akili ya kibiashara anaelewa hivyo, wale waliosalimisha akili zao kwa siasa za majitaka hawawezi kufikiria faida za ugeni mkubwa kwa uchumi wa Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Elimu ya biashara ni muhimu boss ila pia lazima tujitahidi vizazi vijavyo visiwachukie wanasiasa.
Chuki zetu zinasababishwa na uelewa mdogo, kwanza tukuze uelewa binafsi ili media zenye lengo la kutulisha propaganda zisiweze kufanikiwa.

Tatizo la sasa ni uchawa unaofanywa na wanahabari, jaribu kufikiria kwamba yupo mwandishi wa habari anamfuata waziri au mkuu wa taasisi aliyeapishwa na Rais halafu anamuomba ampe tshs 50,000 ili aweze kuandika makala za kumpamba!.

Mwandishi wa namna hiyo anapokosa kupewa pesa na huyo kiongozi anaweza kupewa na adui wa kiongozi huyo na atakachofanya ni kumharibia yule aliyekataa kumhonga, tuangalie hali za namna hiyo kwani wanasiasa wa baadae wanakuzwa katika mazingira ya upotoshaji mwingi wa taarifa na mara nyingi kwa makusudi.
 
Ni kweli, ila huo ni upande wa kwanza wa shilingi, upande mwingine ni wanasiasa wenyewe kufanya mambo yanayosababisha jamii iwachukie.
 
Back
Top Bottom