Afghanistan: Hii ndo nchi ambayo hakuna aliyewahi kuivamia akashinda

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Kwenye historia ya dunia, kuna mataifa yenye jeshi kubwa na silaha za kisasa, lakini kuna eneo moja linalofahamika kama "Makaburi ya Makamanda". Hapa tunazungumzia Afghanistan!

Hata uwe na vifaru, ndege za vita au bajeti ya trillion za dola, nchi hii imekuwa na kizingiti kikuu kwa kila anayejaribu kuitawala. Je, ni kwanini?

Kwanini ni vigumu kuivamia na kuitawala?

1️⃣ Milima ya Hali ya Juu (Hindu Kush): Jiografia yake imezingirwa na milima mikali na mabonde ya hatari. Vifaru na magari ya kijeshi lazima yapite kwenye njia moja nyembamba—kitendo kinachowafanya wawe chakula rahisi cha mashambulizi ya ghafla (ambush).
Na mkipigana ukawashinda, wao nduki milimani, hapo huwaoni , wnaenda kujipanga tena.😁

2️⃣ Hakuna Serikali Moja Inayoshika Kila Kitu: Hata ukiteka mji mkuu (Kabul), bado hujateka nchi. Mamlaka halisi yako mikononi mwa viongozi wa kijiji, makabila, na mabonde mbalimbali. Hakuna "button" moja ya kuisimamisha nchi nzima. Na huko vijijini hadi vichaa wanamiliki bunduki.

3️⃣ Mbinu ya "Muda ni Wetu": Wavamizi huwa wanakuja na saa, lakini wenyeji wana muda! Mbinu zao za vita vya msituni na milimani (Guerrilla warfare) zimeundwa kukuchosha hadi ukimbie mwenyewe.
Utashika nchi, sawa ila wao watakuwa wanakuvizia kuna kambi imekaa kizembe wanaivamia, hivyo vita hawashindi, ila wanakua wanakutia hasara, kila siku mwisho unachoka, utaondoka mwenyewe.

Mataifa Makubwa Yaliyojaribu na Kugonga Mwamba:

🇬🇧 Uingereza (Karne ya 19): Kwenye Vita vya Kwanza vya Anglo-Afghan (1842), jeshi lote la Uingereza lililokuwa likirudi nyuma lilifutwa kabisa milimani. Walibaki na somo la kutokurudi tena.

🇷🇺 Umoja wa Kisovieti / USSR (1979–1989): Walipambana kwa miaka 10 dhidi ya wapiganaji wa Mujahideen. Hasara ya fedha na wanajeshi ilichangia kwa kiasi kikubwa kusambaratika kwa USSR yenyewe.

🇺🇸 Marekani na NATO (2001–2021): Walikaa miaka 20 wakitumia trillioni za dola na teknolojia ya hali ya juu kabisa duniani. Mwaka 2021 waliondoka na kuiacha nchi hiyo mikononi mwa Taliban.

Historia imethibitisha mara kwa mara: Afghanistan unaweza kuivamia kwa siku chache, lakini huwezi kuitawala!

Unadhani kuna nchi nyingine duniani yenye msimamo kama huu?
 
Mmmmh sio kama marekani walimaliza kilichowqpeleka kummaliza bin laden au ulitaka wahamie mazima kama wayahud?
 
Unawavamia watu ambao kufa kwao ni ushujaa, utukufu na ufia dini (martyr) Utawashind vipi?

Osama alikusanya wapiganaji (Mujahedeen) dunia nzima kumtoa Mrusi/Soviet hapo Afghanistan. Watu wanakwenda kupigana ili wafe, sasa unawashinda vipi? 😊
 
Lengo la Marekani ndani ya Afghanistan lililotimia ni lipi?
Afghqn hakuna chakuiba ndio maana wqlivyomalizanq na mtu wakajichenga kisingizio cha kuweka serikqli ya kiraia ilikua ni politics vita ionekane ina mashiko kama wangekuq na wese wamba wangekomaq na taliban wangeganyika mbele ya fungu wangetwangana wenyewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom