Afghanistan: Taliban imesema ni marufuku mfanyakazi wa Serikali kutokuwa na Ndevu. Kama huna Ndevu usikanyage kazini

Afghanistan: Taliban imesema ni marufuku mfanyakazi wa Serikali kutokuwa na Ndevu. Kama huna Ndevu usikanyage kazini

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Nchini Afghanistan, viongozi wa Taliban wamepiga marufuku wafanyakazi wa serikali ambao hawana ndevu kufika ofisini.

Taliban wanasema mfanyakazi yoyote wa serikali lazima awe na ndevu za kueleweka, hakuna kunyoa ndevu na wafanyakazi wote ambao hawana ndevu wamepewa muda kabla hawajafukuzwa kazi moja kwa moja.

Ni uchaguzi wako, ufuge ndevu ama ufukuzwe kazi😂

Kila Jamii ina haki ya kulinda utamaduni wake

Hata sie kuna nchi zinatushangaa inakuaje Ofisi za Umma wameweka aina chache tu za mavazi unayoruhusiwa kuvaa bila ya kujalisha Wewe ni mfanyakazi pale au ni mfuata Huduma, mf. Immigration kwanini wasiruhusu vimini au vipensi kwa wateja wao? Kwanini Askari haruhusiwi kufuga Afro au rasta ndevu?

Ni kama issue ya ushoga…wakati Wewe unashangaa mataifa yaliyohalalisha Ushoga kuna Mataifa yanakushangaa kwanini uzuie watu wa jinsia moja kuparamiana…

Wakati Tanzania inaruhusu Watu kuvaa hijabu kwny ofisi za Umma kuna mataifa yamepiga marufuku watu kuvaa hijabu kwny ofisi za Umma iwe ww ni mtoa huduma au mpokea huduma huruhusiwi kuvaa hijabu
 
Imani iambatane na vitendo

Hongera Talibani.

Osama anaenziwa kikamilifu.
 
Nchini Afghanistan, viongozi wa Taliban wamepiga marufuku wafanyakazi wa serikali ambao hawana ndevu kufika ofisini.

Taliban wanasema mfanyakazi yoyote wa serikali lazima awe na ndevu za kueleweka, hakuna kunyoa ndevu na wafanyakazi wote ambao hawana ndevu wamepewa muda kabla hawajafukuzwa kazi moja kwa moja.

Ni uchaguzi wako, ufuge ndevu ama ufukuzwe kazi😂

Hawa makobazi mtihani mtupu.
 
Kwani sie suruali ya Jeans ukivaa kazini zinapunguza competence hadi zikazuiwa?

Bungeni ukivaa Kanzu bila ya kofia unatolewa nje…tunasubiri BBC wa post ndio nasi tushangae?
Ndevu ni tofauti na suruali. Ndevu ni natural phenomenon. Hazioti kwa mapenzi au utashi wa mtu.

Kuweka kigezo cha lazima (mandate) katika taasisi zinazohudumia wananchi wote kwa kutumia kitu ambacho kiko nje ya uwezo ama utashi wa kibinadamu kama ndevu ni sahihi?
 
Juzi tu wamewapiga pini mabinti wasiende shule. Kuna jamii za watu zina matatizo sana.
 
Back
Top Bottom