Afghanistan: Taliban 'wafanya msako wa nyumba kwa nyumba' Umoja wa Mataifa umeeleza

Afghanistan: Taliban 'wafanya msako wa nyumba kwa nyumba' Umoja wa Mataifa umeeleza

Taliban


Taliban wako kwenye operesheni ya kuwatafuta watu waliofanya kazi kwa vikosi vya Nato au serikali ya zamani ya Afghanistan, waraka wa Umoja wa Mataifa umeeleza.

Usema wapiganaji hao wamekuwa wakienda nyumba kwa nyumba kuwatafuta wanaowalenga na kuzitishia familia zao.

Kundi hilo lenye msimamo mkali wa Kiislamu limejaribu kuwahakikishia Waafghan tangu kutwaa madaraka, na kuahidi hakutakuwa na "kisasi".

Lakini kuna hofu kwamba Taliban wamebadilika kidogo tangu miaka ya ukatili ya 1990.

Onyo ambalo limetolewa kuhusu kundi hilo linalowalenga "washirika" lililetwa katika hati ya siri na Kituo cha RHIPTO cha Norway cha Uchambuzi ambacho hutoa usaidizi wa masuala ya ujasusi kwa UN.

"Kuna idadi kubwa ya watu ambao kwa sasa wanalengwa na Taliban na tishio liko wazi," Christian Nellemann, ambaye anaongoza jopo la walioandaa ripoti hiyo, aliiambia BBC.

"Ik kwenye maandishi kuwa wasipojisalimisha Taliban watakawamata na kuwashtaki, na kuwaadhibu wanafamilia kwa niaba ya watu hao."

Alionya kuwa mtu yeyote kwenye orodha ya Taliban yuko katika hatari kubwa, na kwamba kunaweza kuwa na mauaji ya watu wengi.

Kumbe ni "umoja wa mataifa umeeleza" unategemea nini 😁😁😁 pumbaf zao
 
Wakiitwa Terrorists wanasema wanasemwa vibaya. Sasa kuwafanyia hivyo raia ni nini kama sio ku' terrorise raia.

Kwaiyo unakubaliana na propaganda, tena taarifa yenyewe imetoka BBC unategemea nini!!!! Marekani, israel na nchi nyingi za europe wameuwa mamilioni ya civilians mbona hamuwaiti terrorists!!!!!


Kwa taarifa yako Taleban imesharudi kushika nchi, na nchi itaendeshwa kwa sheria za dini pasipokua na unyanyasaji, vita, dhuluma, ubaguzi n.k. everybody atapata haki yake.
 
Ukiwaita hivyo,kuna watu humu wanakumind vibaya yani,nadhani hayo wanayofanya itakuwa sio ugaidi.

Ngoja uone watakavyokushambulia.

Nyie ata mkiletewa propaganda mtazipokea tu, ndiyo akili ya mtu mweusi ilipoishia, ila wako wanaojitambua.
 
Sasa, jeshi lao limefata nini huko miaka yote 20? Na isitoshe jeshi la serikali lilikuwemo!!!!! Labda mwenze2 ulikuwepo afghan waweza kutupia nondo
Ulitaka wakae milele?
Lengo lao lilikuwa kumkamata Osama na kumuadhibu Mullamulah na hiyo kazi waliimaliza, unatakaje?
Vita ni gharama walikuwa sahihi kuondoka
 
Waafrica kwenye hili unawaonea hakuna race ya wajinga duniani km waarabu
Afghanistan ni moja kati ya nchi masikini sana duniani but inamiliki silaha nzuri na za kisasa and very expensive yaani halafu wanaozitumia hizo silaha hawana viatu vya maana miguuni. Wafrica na waarabu nadhani tunafanana fanana
 
Kuna mwenzetu mmoja amechangia kwenye group letu la WhatsApp kuhusu hii mada, naomba kumnukuu bila kumtaja jina.
COPY AND PASTE
Nationalism is a spirit, it can never be bought with any amount of money, donations and what have you. The 100,000s of Afghan military that the US trained using trillions of US taxpayers money had Taliban spirit sequestered in their inner selves waiting to manifest at the opportune moment. This moment came when the US forces withdrew, so the Taliban spirit unveiled itself and manifested vividly by surrendering to insurgent forces (fellow Taliban of course) without meaningful resistance. And now, to all Afghani (read "Taliban"), patience has paid off after 20 long years of breath-holding.
 
Back
Top Bottom