Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Marekani na Uingereza na nchi zingine washiriki wametuma vikosi vya jeshi kurudi tena nchini Afghanistan ili kufanya operesheni ya kuwaokoa raia wa nchi hizo pamoja na raia wa Afghanistan wenye pasi mbili za kisafiria.
Marekani inatuma vikosi vya wanajeshi wapatao 3000 huku Uingereza ikituma vikosi vya wanajeshi wapatao 600.
Miongoni mwa raia wa nchi za Uingereza, Marekani washirika wake ni maofisa katika balozi zao, mashirika ya kimataifa na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Raia wa Afghanistan wenye pasi mbili za kusafiria yaani ya Afghanistan na moja ya nchi za kimagharibi ni miongoni mwa wale watakaopewa kipaumbele katika operesheni hiyo ambayo imepewa jina la "Non Combatant Evacuation Operation" NEO na Pentagon makao makuu ya ulinzi wa Marekani.
Raia wengine watakaookolewa ni wale raia wa Afghanstani ambaio walikuwa wakisaidiana na majeshi ya Marekani, Uingereza na majeshi shirikishi kwa shughuli za ukalimani na ambao maisha yao kwa sasa yapo hatarini baada ya wanamgambo wa Taliban kuwasaka popote walipo.
Wanamgambo wa Taliban walianza kampeni ya kuikomboa Afghanistani kutoka kwa serikali kibaraka ilowekwa kwa na kusaidiwa na nchi za magharibi baada ya mgogoro ulochokuwa zaidi ya miaka 20 ilopita.
Katika kampeni yao hiyo Taliban tayari wamekomboa na kuichukua sehemu yote ya kusini wa nchi hiyo jimbo la Lashkar Gah, kuendelea juu na kuchukua mji wa Kandahar ambao ndo kitovu cha biashara na uchumi wa nchi hiyo.
Leo hii Taliban wanaelekea mji mkuu wa Kabul na tayari wameteka jimbo la Logar ambalo lipo kusini mwa Kabul.
Hadi kufikia Jumapili ya leo jioni Taliban watakuwa wamefika mji wa Char Asyab ambao ni kilomita saba kutoka Kabul, na kufanya idadi ya majimbo makubwa ambayo hadi sasa yapo chini ya Taliban kufikia 18.
Lakini tujaribu kuangalia hali hii imetoakea vipi mpaka Taliban wakaamua kuanza kampeni ya kuikomboa Afghnistani?
Wiki kadhaa zilizopita utawala wa vibaraka wa nchi hiyo ulianza kushuhudia kuanguka kwa mori katika vikosi vya majeshi ya ulinzi ambayo yalifunzwa kwa garama kubwa na jeshi la Marekani kwa miaka ishirini huku dola zipatazo milioni 90 zikitumika kugharamia mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yalikuwa ni ya kulitayarisha jeshi jipya la Afghnistani lenye uwezo wa kijeshi ambao agnalu unakaribiana na viwango vya kimataifa kuweza kukabiliana na kuibuka upya kwa wanamgambo wa Taliban baada ya vikosi vya Marekani kuondoka kabisa kwenye nchi hiyo ifikapo mwishoni wa mwezi huu.
Kitu ambacho kimeshuhudiwa ni kwa vikosi vya jeshi jipya la Afghanstani likisalimu amri kwa wanamgambo wa Taliban huku wakiwa hawajaribu hata kutumia silaha, mafunzo na mbinu walopewa na wamarekani.
Kusalimu huko amri kumeambatana na kuvua na kubadilisha nguo za kijeshi na kujiunga kujificha kwa wananchi wanokimbia na hata kuamua kujiunga na wanamgambo hao wa Taliban ambao safari hii wamekuwa ni hatari zaidi yaani yaani kwa kiingereza twasema wamekuwa "Ruthless".
Lakini kiini khasa cha mgogoro huu wa sasa ni kwa wananchi wengi wa Afghanstani kukosa huduma muhimu kama maji na umeme, huku wanajeshi wa jeshi jipya, polisi watumishi wa serikali ya vibaraka wakikosa kulipwa mishahara yao na malipo na mavazi.
Jibu walolipata wa-Afghanstani ni kwamba utawala wa vibaraka wa nchi hiyo na makamanda wa jeshi wamekuwa wakila fedha hizo za mishahara na kuchukua bidhaa kama chakula cha wanajeshi na polisi.
Miaka 20 ya kutawaliwa na majeshi ya kigeni na matumizi makubwa ya fedha bado yameiacha Afganstani ikiwa ni nchi maskini, yenye jamii ilogawanyika na iloyo nyuma kimaendeleo.
Bado wananchi walio wengi wa nchi hiyo wanaishi kwa kipato cha dola moja au chini ya hapo huku familia chache zenye kufahamiana au kujuana na utawala wa nchi hiyo wakizidi kuwa matajiri na wenye uwezo mkubwa wa mali na fedha zinazotokana wizi wa fedha za misaada kutoka nje na mikataba ya kughushi ya jeshi jipya.
Hivyo chuki kubwa imejengeka kutoka kwa raia wengi ambao wamechioshwa na matuko haya yote ya ufisadi na ambao wanategemea kilimo pekee kuwakomboa kiuchumi.
Viongozi wengi wa utawala wa Kabul wapo nje ya nchi hiyo ama ughaibuni au nchi zingine jirani wengi wakiwa hawazungumzi lugha kuu mbili za nchi hiyo Pashto na Dari na pia wengi wao wanabeba pasi mbili za kusafiria.
Raisi Ashraf Ghani ambae yupo madarakani kwa baraka za nchi za magharibi amekuwa akishinda uchaguzi ambao wananchi wengi wanadai tayari matokeo yanakuwa yamepitishwa kabla.
Kama inavyoonekana hapo juu kuwa kuna tatizo kubwa ambalo limesababishwa na Marekani na washirika wao ambalo ni kuikalia nchi hiyo kwa miaka zaidi ya ishirini huku viongozi wa utawala wa vibaraka wakiwa wanaponda mali za nchi hiyo, wakiendekeza ufisadi na kuwagawana fedha zote za kodi, misaada ambazo zingwleta maendeleo kwa nchi hiyo.
Kuna haja kubwa kwa nchi ambazo bado zinatathmini uwezekano wa kuruhusu uraia wa nchi mbili au uraia pacha ambao kwa miaka kadhaa sasa umekuwa ukizungumzwa na watanzania waishio nje.
Lakini mfano huu wa utawala wa Afghanstani ambao umekuwa wa kifisadi kwa kiwango cha juu huku ukilindwa na majeshi ya kigeni ndo umesababisha kurudi kwa wanamgambo wa Taliban ambao lengo lao ni kuikomboa nchi hiyo kutoka katika mikono ya utawala wa vibaraka.
Sasa hivi majeshi ya Marekani na Uingereza yanarudi kwa mgongo wa kuwakomboa raia wa nchi hizo, lakini kwa wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia wanafahamu kwamba majeshi haya ni lazima yarudi mjini Kabul kuulinda mji huo ambao ndipo yalipo makazi ya balozi nyingi ukiwemo wa Marekani.
Vita vya Afghanstani na kurudi upya kwa majeshi ya Taliban na Marekani na washirika wake na ubeberu wa nchi hizo ni masuala ambayo yanatabirika.
Alfred MacCoy ambae ni profesa wa Historia katika chuo kikuu cha Wisconsin Madison mwaka 2016 aliandika kitabu kiitwacho "Washington's Twenty First Century Opium Wars" alokitoa mwezi februari, akiilenga Pentagon na akahitimisha kwa kusema "Looming disaster" yaani dhoruba inokuja.
Profesa MacCoy ameelezea masuala makuu matatu, kwanza ni gharama halisi ya vita ambavyo Marekani inagharamia nchini Afghanstani kuwa inafikia dola trilioni 2 zikwa ni fedha za walipa kodi.
Pili, anaitaja Afghanstani kuwa nchi ya kwanza duniani kwa kuzalisha madawa ya kulevya aina ya heroin.
Na tatu, anasema namnukuu" Despite spending trillions (tax payers money) the pentagon has not won a war since 1945"- mwisho wa kunukuu.
Tafsiri - Licha ya kutumia matrilioni ya fedha za walipa kodi Pentagon hawajawahi kushinda vita tangu mwaka 1945.
Kurudio kwa majeshi ya Marekani Afghanstani upya kupambana na Taliban ni ishara tosha kwa vikundi vingine vya aina hiyo katika nchi za Irak, Syria, Libya, Lebanon, Yemen na hata sasa nchini Msumbiji.
Nihitimishe tu kwa kusema kwamba hakuna anaeweza kutabiri yajayo na hakuna ambae angetarajia kuona wanamgambo wa Taliban wanarudi mazima.
Hivyo suala la kuleta amani na maridhiano baina ya wananchi walogawanyika wa Afghanstani ndilo muhimu kwa sasa.
Mwisho, ni hili la uraia pacha kwamba nchi kama Tanzania bado ina nafasi ya kujifunza kinagaubaga katika kuelewa watanzania walipo katika diaspora na kujidhihirisha kabla ya kuamua kutoa uraia wa nchi mbili.
Vyanzo: Sky news, Aljazeera, Kitabu cha Profesa MacCoy na gazeti la Kabul times.