JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni, Daud George (28) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuiba mita za maji na kuisababishia hasara ya Sh904,277. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa).
George amefikishwa Mahakamani hapo leo, Jumatano Januari 8, 2025 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu.
Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Erick Kamala, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
Hakimu Nyaki ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 21, 2025 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma ~ Ruvuma: Huu utaratibu wa mteja kulipia mita za maji zilizoibwa upoje? Au mnaiba wenyewe ili tuwaongezee mapato?