Afilisiwa kiwanja na nyumba kisha kukatwa mkono kisa madeni ya vikoba vya mke wake

Wakuu habarini!

Hawa wanawake wasiojitambua Ni changamoto Sana!

Hapa kitaa Kuna kisa kimetokea na ugomvi kuzuka wa hali ya juu!

Ni hivi, Kuna mzee mmoja hapa mwenye mke na watoto, ambaye kwa hali ngumu za kimaisha lakini kakomaa na kununua kiwanja kisha akajenga nyumba yake ya kuishi na family yake na ziada ya wapangaji vyumba vitatu!

Sasa, mke wake kaingia kwenye vikoba, kakopa kisirisiri kisha kaweka lehani hati ya nyumba ( ambayo aliiba bila mmewe kujua) kwa madai ya kuwa atarejesha! Mambo yakamgeukia mama huyo lakini ilimladhimu kuwa msiri kwani aliogopa kumshirikisha mmewe.

Muda umeenda Sana, one daya mara ghafla bini vuu , mapolisi, na wanavikoba wamekuja pale wako mobu Sana, wanaulizwa kulikon, mzee anaambiwa hii nyumba sio yako, mke wako aliweka rehani kama dhamana ya mko wa tsh mil5 ambazo zimemshinda kurejesha, muda aliopewa na mahakama umefika na hivyo mahakama imetoa amri ya kutaifishwa kwa nyumba na kiwanja! Kwa hiyo, wakaamuliwa kutoa kila kitu , wakatoa wakafukuzwa kutafuta hifadhi kwa wasamalia.

Siku kadhaa mbele wamekuja ndg wa mwanaume na ugomvi ukazuka kati yao na mwanamke kiasi ambacho mmoja wao ( shemeji yake) akaanyanyua panga kumkata yule mama , lakini kabla hajafikisha upanga, kumbe mme mtu kaingia kumkinga mke wake na hivyo upanga ukatua kwenye mkono wa kulia!

Jamani tuishi na wanawake kwa akili
Anahitaji msaada wa kisheria.Dhamana ya nyumba lazima mke na mume waridhie kwa pamoja.Kwahiyo wote lazima wasign mikataba ktk ukopaji.Moja akifanya bila mwingine kujua inakuwa sio dhamana hali.Mzee akienda mahakamani wanarudishiwa kiwanja na nyumba.
 
Hii story haina uhalisia kisheria mkuu ula kikitaa ndio kama hivi.
 
Hii inatokea sana hati kuibwa kwenda kukopea bila mume kujua
 
Naomba kufahamu ,je kisheria mwanamke ambaye hamjafunga ndoa na mmezaa na kuishi pamoja ana haki sawa na mwanamke aliyeolewa kwa ndoa kwenye ishu ya mgawo wa mali mnapoachana iwapo mali zote ni za mwanaume
Kisheria mke ambae umeishi nae ndani ya miaka isiyo pungua miwili
Jamii yote inayo wazunguka ikatambua mnaishi kinyumba ( mke vs mume)
Huyo ni mkeo kwenye dhana ya ndoa
Hivyo basi anahaki sawa na aliefunga ndoa
Pia hata mkiachana anahaki ya kupata mgao wake kwa kiasi alicho changia

Bi Hawa Mohamed vs Ali seifu

Shauri hili lilitoa mwongozo
 
Back
Top Bottom