Afilisiwa kiwanja na nyumba kisha kukatwa mkono kisa madeni ya vikoba vya mke wake

Anahitaji msaada wa kisheria.Dhamana ya nyumba lazima mke na mume waridhie kwa pamoja.Kwahiyo wote lazima wasign mikataba ktk ukopaji.Moja akifanya bila mwingine kujua inakuwa sio dhamana hali.Mzee akienda mahakamani wanarudishiwa kiwanja na nyumba.
 
Hii story haina uhalisia kisheria mkuu ula kikitaa ndio kama hivi.
 
Hii inatokea sana hati kuibwa kwenda kukopea bila mume kujua
 
Naomba kufahamu ,je kisheria mwanamke ambaye hamjafunga ndoa na mmezaa na kuishi pamoja ana haki sawa na mwanamke aliyeolewa kwa ndoa kwenye ishu ya mgawo wa mali mnapoachana iwapo mali zote ni za mwanaume
Kisheria mke ambae umeishi nae ndani ya miaka isiyo pungua miwili
Jamii yote inayo wazunguka ikatambua mnaishi kinyumba ( mke vs mume)
Huyo ni mkeo kwenye dhana ya ndoa
Hivyo basi anahaki sawa na aliefunga ndoa
Pia hata mkiachana anahaki ya kupata mgao wake kwa kiasi alicho changia

Bi Hawa Mohamed vs Ali seifu

Shauri hili lilitoa mwongozo
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…