DOKEZO Afisa Elimu wilaya ya Sikonge (msingi) anakula rushwa, pia anatumia madaraka yake kukandamiza wengine

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jina la ni lako umeandika?
Mbona hauja weka picha yako?

Weka hata humu kwa uzi na kitambulisho chako tujue ni wewe kweli umeandika. Na topic ni Afisa Elimu wewe upo nae ofisini kila siku ya kazi na kuongozana nae pia. Hizo millioni weka orodha ya kila senti umetumiaje hapa. 😊
 
Jamiiforum mnasikitisha sana kusema vitu ambovyo ni uongo mtupu mimi ni mwalimu mkuu

Kama mwalimu mkuu Unatoa aibu kutaja Jamiiforums.com na sio mleta mada. Umekurupuka kwa uoga sio? Asiondolewe mkaamua wewe mtetezi

Nitakuamini ukijibu post yangu ya mwanzo humu.
 
Kwanza ukitazama mtoa mada ni kama umetumiwa kiujumbe na mtu na wewe bila kufanya reseach unapeleka public.


1.Hoja ya afisa elimu kufanya uteuzi mbona ni uongo, mwenye mamlaka hayo katika serikali za mitaa ni Mkurugenzi.
Na ili tukuelewe ilikua n vizuri ukaweka na barua za hao walio teuliwa hawana sifa na ukatusaidia na sifa za uteuzi zipoje

2.Lakini ikumbukwe kuwa Hakuna mwalimu chuo alienda kusoma Ualimu mkuu ila anaenda kusoma ualimu. kwahyo kama utendaji kazi wa kiongozi hauridhishi lazima utolewe na aje mwingine. sasa ukitolewa unakimbilia kwenye majukwaa kupiga kelele utazani umenyang'anywa Ualimu kumbe uongozi ambao hujausomea.
Hii ni upuuzi na Ujinga.

3.Na kama umepata uthibitisho kwamba Anakula Rushwa kwanini usipeleke mambo hayo kwa Mamlaka zinazo shughulikia Rushwa ili achukuliwe hatua? Lakini kwavile umeondolewa kweny nafasi ya ukuu wa shule umenuna na bila kutafakari umeona uchafue watu.


4.Watumishi hasa walimu kila mwaka wanaenda kujiendeleza na hili la kujiendeleza ni sheria ambayo Inamtaka Mwajiri Kumuendeleza Kimasomo mtumishi wake sasa tangu lini afisa elimu akasomesha mwalimu?.

Na watu tangu zaman wapo wanao soma masafa yaani open university na wengine main cmpus. Sasa kuambiwa kasome masafa nayo ni dhambi? Kama huridhishwi na kusoma Masafa njia nzuri ni kumfata Mkurugenzi na kumwambia kwamba huhitaji njia hii ya kusoma unampa na sababu. Na kwavile alikupa barua ya kukuweka kwenye Mpango nazani atakuelewa na kukuruhusu.



La mwisho japo sio kwa upana,Nikushauri upunguze hasira kama umetolewa kwenye nafasi ya kuwa kiongozi Tulia na ujifunze kwamba nafasi uliyopewa umeshindwa kuleta tija.


Ila hiki unachofanya ni Majungu,Uongo na fitna tu
 
Umekumbusha wimbo wa snow ukiitwa informer. Unajifanya mbea mbea watakugongomea.
 
Umeongea logic kubwa sana
 
SIKONGE ni miongoni mwa sehemu mfu ataendelea kufanya awezalo
 
Mkurungezi anateua watu/walimu wakuu waliopendekezwa na afisa elimu sasa hao wanaopendekezwa na afisa elimu wanakuwa hawana sifa sitahiki kuwa wakuu wa shule
 
Naona chawa mmeitana kushambulia. Eti mkurugenzi mkurugenzi, unafanya watu wajinga kama vile mkurugenzi anayejua kutoka mbinguni. Mkurugenzi si anapitisha majina ya DEO tu
 
Hawa jamaaa ni nouma we acha tuu mimi nina mautumbo ya huyo afisa elimu mpk maulozi
 
Wewe ni miongoni mwa walimu wakuu wajinga na mliopewa vyeo hivyo au mmenunua.

Kwenye Uhamisho wa walimu na uteuzi wa walimu wakuu mhusika ni idara ya elimu . Mkurugenzi anaweka saini Tu.

Hapa unasema unaongea Kwa niaba wa walimu wakuu ,, wewe Kama nani au wewe ndio Mwenyekit wa TAPSHA huko ?
 
Watu wamekaza fuvu wasijue kwenye mambo ya elimu mkurugenzi siku zote anafuata kile anachoambiwa na afisa elimu.... Mwalimu hauwezi ukapewa ukuu wa shule, kwenda kusoma au favour yoyote Ile bila afisa elimu kutaka vinginevyo kama una ukaribu au undugu na walio juu ya huyo afisa elimu....
 
Sikonge Tabora, Kila tuhuma itafanyiwa kazi serikali ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…