Afisa Makao Makuu CHADEMA: Mbowe anaendekeza Ukabila. Kati ya wafanyakazi 19 wanaolipwa Mishahara na CHADEMA 9 wanatoka Killimanjaro

Afisa Makao Makuu CHADEMA: Mbowe anaendekeza Ukabila. Kati ya wafanyakazi 19 wanaolipwa Mishahara na CHADEMA 9 wanatoka Killimanjaro

Kuna vitu maalumu wadada wote walikuwa wachaga adi anayetokea Lindi,karatu ,saivi akachaguliwa sijui nani minja tokea Dodoma.

Yaani jamaa ukabila wangeuweka pembeni wangekuwa watawala wa kwanza wa nchi hii.
 
Hakuna mtu mkabila Tanzania hii kama mbowe, unakumbuka kila siku alikuwa ana kosoa Magufuli kuongea na kusalimia watu kisukuma wakati huo kila mtu anakua 75% ya wafanyakazi chadema wametoka mkoa mmoja, na kwa siasa hizi za mbowe chadema itakuwa just hapo inaimba democracy democracy tume tume, maandamano no one will take it serious.

Na mikoa mingine imeamka, atazunguka Tanzania watu wana mtazama tu, siasa za Kenya haziwezi kufanya kazi Tz.

Ni lazima chama kiwa na sura ya kitaifa na kikubaliwe na watu wote. Hayo ndio makosa walifanya CUF.

Nyerere alijenga chama, chama cha kila mtu, kikashika hadi vijijini huko Tanzania kote, ndio maana tuna struggle kukiondoa, inafika kipindi hata kiazi kikisimama Urais kinashinda.
 
Kuna watu hawana akili kwa kweli, hata hili wanaona kawaida; eti maadam hao wanao shika hizo nafasi wana sifa. CHADEMA wamefanya makosa mengi sana ni muda sasa kulipa gharama za uhuni wote wamekuwa wakifanya. Mbowe akumbuke kuwa watu waliipenda CHADEMA baada ya NCCR Mageuzi na CUF kuanza kukosa sifa za kupendwa, kwa sasa CHADEMA ni chama ambacho hakina jambo lolote la maana , ni vile tu watu hawaipendi CCM, lakini kwa hali inavyo enda CHADEMA itachukiwa kuliko CCM.
 
Mwenye chama chake!!
 

Attachments

  • Screenshot_2024-12-21-10-58-21-719_com.twitter.android.jpg
    Screenshot_2024-12-21-10-58-21-719_com.twitter.android.jpg
    274 KB · Views: 3
XxxxxX
Twende Pamoja, kwa muda mrefu wapinzani wetu kisiasa wamekuwa wanasema udini na ukabila zaidi kwa swala la Ukabila wanalengwa watu kutoka mkoa wa Kilimanjaro anakotokea Mwenyekiti wetu wa Taifa. Naomba nikushirikishe na wewe upime Je kuna ukweli wowote?

Secretariat ambacho ni chombo cha kiutendaji cha kila siku yaani engine ya Chama ina wajumbe 10 mpaka sasa. Wajumbe hawa wamegawanyika katika sehemu kuu tatu

1. Wajumbe wa kuchaguliwa na Baraza Kuu. Hapa naongelea Makatibu wa Mabaraza yote matatu (Bavicha , Bawacha na Bazecha)

2. Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na baraza kuu. Hapa nawaongelea Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Mkuu

3. Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Kamati Kuu. Hapa nawaongelea wakurugenzi

Kwa mantiki hiyo, wajumbe wa moja kwa moja wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa ni Katibu Mkuu, Naibu Bara , Naibu Zanzibar na wakurugenzi.

UKABILA
Mpaka sasa hivi Makao Makuu wapo wakurugenzi wanne kati ya hawa wakurugenzi watatu wanatoka mkoa wa Kilimanjaro majina yao ni
Reggy Munisi - Mchaga kutoka moshi (machame)
Jonathan Mndeme - Mpare kutoka same na John Mrema - mchaga kutoka vunjo. Mkurugenzi mmoja tu ndo anatoka Mkoa wa Kagera Mzee Lutembeka na ni kwa vile tu wanamtumia ku save nafasi mbili kama Katibu Mkuu wa BAZECHA TAIFA na kwa taaluma yake wanamtumia kama mkurugenzi wa FEDHA NA RASILIMALI

Twende kwenye watumishi wa kawaida Maafisa

Hapo Makao Makuu mpaka sasa wapo wakuu wa idara na maafisa 9 kati ya Hao wakuu wa idara na maafisa 5 wanatokea mkoa wa Kilimanjaro. Kwa majina ni
1. Zuhuru Nkya - Mchaga anatokea HAI
2. Karimu Muro - mtoto wa mwisho wa kumzaa wa Zuhura Nkya - Mchaga anatokea HAI
3. Lucas Mrema - Mchaga anatokea Vunjo
4. John Ngauro - Mchaga anatokea moshi
5. Aron Mashuve - mpare anatokea same

UDINI
Hivi tunavyozungumza pale makao makuu Muislamu anayefanya kazi Makao Makuu ni lazima awe anatokea Mkoa wa KILIMANJARO. Wasiotokea mkoa wa KILIMANJARO wote baada ya chama kuanza kupokea RUZUKU wameondolewa kwenye UTUMISHI

Watumishi waliopo makao makuu ambao ni waisilamu ni watatu ambao ni Karimu Muro, Zuhura Nkya, Reggy wote hawa wanatokea mkoa wa KILIMANJARO . Watumishi ambao ni Waislamu wameondolewa kwa sababu Hawatoki KILIMANJARO ni Zainab Ashraf Kutoka Tanga na Halima Lichonyo Kutoka Ruangwa Lindi. (Chunguzeni)

Kwa ujumla wake makao makuu inawatumishi kwa maana ya Secretariat na Maafisa jumla 19. Kati ya Hao 9 wote wanatoka mkoa wa Kilimanjaro, Waislamu wote wanatokea Kilimanjaro isipokuwa mmoja tu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Hivyo, Wapinzani wetu wamekuwa wanatupiga sana kwenye hii hoja ya UDINI na UKABILA kitu ambacho kwa jicho la kiuhalisia ni Kweli, tunatakiwa kuwa smart na kuondoa ombwe la namna hii. Lazima tupate mchanganyiko kutoka pande mbalimbali kutoka mikoa yetu. Uwakilishi uwe na uwiano wa haki na usawa.

Lazima tumwambie Mapema Mwenyekiti wetu Mtarajiwa TUNDU ANTIPASI LISSU , kuwa hii Propanganda ambayo tunapigwa ya muda mrefu tuifute kwa kuja na mkakati mpya wa upatikanaji wa wakurugenzi na watumishi wa Makao Makuu wenye sura ya Kitaifa zaidi

Ikumbukwe hapa sijaongelea walinzi wala madereva

Naomba wajumbe wapiga kura tafadhali hilo tufanyie uamuzi sahihi Tuletee TUNDU LISSU ili tuje tujenge upya Chama chetu

Tusimame na LISSU 21 January.......!

Remigius Celestine
22.12.2024
Ila Mbowe anabalaa jamani,🤣🤣🤣
 
FAM siyo kiongozi wa kwanza kufanya hivyo - baada ya kufeli kwa mapinduzi 1980s idara kadhaa zilijaa watu wa Mara
  • Charity starts at home;
  • Asiyependa wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini;
 
FAM siyo kiongozi wa kwanza kufanya hivyo - baada ya kufeli kwa mapinduzi 1980s idara kadhaa zilijaa watu wa Mara
  • Charity starts at home;
  • Asiyependa wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini;
Acha uongo, Nyerere hakua mkabila otherwise angejenga majengo mengi sana Mara. Labda kidogo tu jeshini tena sababu alitaka kuwa secured ila sio sababu ya ukabila.
 
Back
Top Bottom