Afisa polisi OCS mshukiwa wa kifo cha Albert akana uhusika! Agoma kuwa mbuzi wa kafara

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Ninatolewa kafara. Sasa mimi ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Albert Ojwang, ingawa sina hatia.
Maafisa wa DCI walipomleta Albert Ojwang katika Kituo Kikuu cha Polisi, alikuwa katika hali mbaya. Alionekana kuteswa. Niliwataka maafisa wa DCI kumpeleka hospitalini kabla ya kumwingiza mahabudu, lakini walikataa wakidai walikuwa wakitekeleza maagizo kutoka juu.

Maafisa wa DCI walimfanyia nini Albert kabla ya kupelekwa seli sijui. Sasa, ninatolewa kafara ili kuwalinda wale ambao kwa hakika walifanya uhalifu—kumlinda ‘mtu mkubwa’ nyuma yake.
Afisa huyo anasisitiza: Ningekuwa na maslahi gani ya kumuua Albert, ikilinganishwa na wale waliomleta kutoka Homabay? Ninakataa kuwa mbuzi wao wa kafara.~OCS Kituo cha polisi cha Central Samson Taalam
1749658690739.jpg
 
View attachment 3364753
cc:Kingai aione kwenye jalada kwa kumbukumbu za maisha.
 
Siku ya kifo cha nyani miti yote hutereza.

Wameuwa wangapi waovu hawa, akiwamo huyu?

Kwani Ile hadithi ya kujigonga marehemu ukutani huyu hakuwa sehemu yake?
 
Haiwezi kutokea Tanzania kwa sababu watakwambia kuwa mpole tunashughulikia na kweli badae watakutoa.

Huko Kenya ni hamna tu, watakwambia kuwa mpole halafu watakutoa, mwisho wa siku ukizubaa unakula miaka unawaacha uraiani.

Kuna siku niliangalia kama stori fulani BBC Swahili walimtembelea gerezani kumuhoji aliyewahi kuwa mkuu wa kituo cha polisi huko kaunti fulani Kenya, ambaye alisingiziwa kesi ya mauji na kufungwa. Nilimsikiliza kwa makini yule bwana, hakika alisingiziwa lakini kwa kuwa yeye ni mkuu wa kituo hakuwa na namna. Kesi ile inataka kufanana na ya huyu bwana. Inaonekana wakuu wa vituo vya polisi Kenya wanaangushiwa sana majumba mabovu!

Ni bora huyu mkuu wa kituo amesema ukweli yule mtu aliletwa akiwa mahututi. Swali, je alichukua hatua gani? Kuna kila dalili ya kuangushiwa jumba bovu.
Nawazaaa tuu hiii kama inaweza kutokeaa hapa Tanzania......nawazaa tuuu
 
Back
Top Bottom