Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,201
Lovie Lady umenitoa machozi asubuhi hii, umenifanya nijitafakari hata mimi kipi nilichofanyia jamii yangu kwa kidogo nilichobarikiwa [emoji24][emoji24] Maisha ya Milembe yamenipa chachu na mimi nifanye jambo nikumbukwe kwa Wema kama hivi, niombewe Duaa njema na Watoto Yatima, Wajane, Maskini na Walemavu,Dream Queen
Wengi wanaomchukia kwanza hawamjui na hawakubahatika kujuana nae in person..na wengi wao wanamchukia kwasababu aliwazidi sana Kiuchumi yaan aliwapiga gape kubwa sana..na kubwa zaidi ambalo litandelea kubaki kwenye nyoyo zetu ni namna ambavyo Marehem Milembe alivyojua kuigusa Jamii alikua VOICE OF THE VOICELESS PEOPLE IN THE SOCIETY
Kuibeba jamii yeye kwake ilikua ni Primary concern kwenye maisha yake[emoji3590]
Watu wenye chuki binafsi na roho mbaya wamekatisha uhai wake na kuumiza maisha ya wengi waliokua nyuma yake [emoji17]
Kuna watoto yatima wapatao 31 alikua anawalipia Ada wengine wako Vyuo mbali mbali, wengine wako Advance wengine Secondary wengine Primary level wamemuua nani atakaetimiza ndoto za Yatima hawa waliokua wakibebwa na Milembe?
Na alikua akiyafanya hayo kimya kimya wala hakujitangaza [emoji17]
Hakuishia hapo tu alisaidia Wajane waishio Dar Kigamboni na maeneo mengine mbali mbali (WAJANE WALEMAVU WA VIUNGO) aliwanunulia BAJAJI na kuwapa bure..waweze kujikwamua kiuchumi na wala hakutaka kuwapiga picha na kuwatangaza aliyafanya haya kimya kimya Marehemu..Sasa hao wanaomkashifu na kumponda wao wamefanya nini kwenye Jamii???
Tutaendelea kumuenzi kwa mazuri yake na kumuombea Milele [emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji120][emoji120][emoji120]
Tulikupenda sana Milembe pumzika Mwamba..waliokufanyia huu unyama watalipa tu damu yako haitaenda kihasara hasara [emoji120]
Allaahuma Aamiiiin [emoji120][emoji120][emoji120]
Aendelee kupumzika kwa Amani Shujaa Milembe, tukisema ni shujaa basi tunamaanisha kweli ni Shujaa aliyemulika Maisha ya wengi,
Waliomuua hawatakaa wapate amani ya moyo na laana itawatafuna hadi vizazi vyao vya 10, kila wafanyalo damu ya Milembe isifutike kwenye mikono yao,
Wanaoshabikia kifo chake hawatopata baraka, vilio vya Yatima, Wajane, Walemavu na Maskini viwe vizito katika nyoyo zao, wawe wanaota ndoto za maruwe ruwe tu,
Innalillah wainna Illah Raji'un [emoji120]