Na asilimia kubwa ya wanaofurahi juu ya hiki kifo cha kikatili ni mafukara waganga njaa, rizki wanazipata kwa kuzurura kama mijibwa koko, wanaishi uswekeni na hizi mvua ni mwendo wa kuchanua miguu na kukanyaga matope ili wafike kwenye vibanda vyao, familia imewaelemea hawana furaha tena,
Kundi lingine ni la graduates, wameshatembeza bahasha hadi soli za viatu zimelika upande, wamekata tamaa wanachomiliki ni smartphone na laptop, wamepanga chumba kimoja wanakimbizana kwenye kodi au wanaishi kwa mashemeji zao, wamepauka kwa mawazo na wengine wamezeeka kabla ya umri wao,
Kundi lingine ni la wale wamama waliozalia nyumbani, wamepitia manyanyaso kuanzia kwa baba wa watoto wao, ndani ya familia, hadi kwa majirani, walijiingiza kwenye vikoba bila kua na shughuli maalum, madeni yanawatokea puani, kuna hawa wengine walisoma soma wakapata vidiploma na degree, ndoa hakuna, kazi ina mshahara mdogo, umri unasonga, akiingia mitandaoni anakutana na slogan ya kataa ndoa, akitoka nje anakumbana na wadogo zake wanatolewa mahari yeye kaamua kununua pete kwa machinga kajivesha,
Kuna hili kundi lingine liliwahi kuoa, likapoteza kazi, likatumia akiba yake yote kufanya biashara, likaangukia pia, likarudisha mpira kwenye nyumba ya urithi, huku kuna dada aliachika, kule kuna shangazi, pale kuna mjomba na familia yake, full heka heka, furaha ya maisha itoke wapi.....