View attachment 348773Mashabiki wa Yanga wakimpongeza Dida kwa kazi nzuri aliyoifanya leo Angola ikiwa ni pamoja na kuokoa penati.
Alikaa golini mechi na Al Ahly klabu bingwa
Afrika akishuhudia goli la jioni na lililobaki kama
alama ya uchungu kwake , wanayanga na
watanzania kwa ujumla . Goli lililoiondoa Yanga
katika michuano hiyo .
Leo tena akiwa langoni dakika zile zile refa ana
amuru ipigwe pennati langoni mwake .
Alivuta pumzi ndefu na kulitazama benchi la
ufundi kisha wachezaji wenzake na kwa haraka
fikra zake zikasafiri maelfu ya kilomita hadi
nchini kwake ( kwetu) na kuziona nafsi karibu
milioni 40 zikijenga tumaini la magharibi juu yake
, . Taifa nzima likimtazame yeye aamue furaha
yao au wahuzunike tena ...
Aliuma meno na na kujiweka sawa langoni .
.... Penati akaipangua ... Taifa likazizima kwa
furaha ... mikono yake ikawa mali kuliko almasi
za waangola... Kwa hasira na jiwe wakampiga..
Wakamuona adui na katili mkubwa kuliko nduli
wao hayati Jonasi Savimbi aliyewatesa kwa
miongo kadhaa... Oooh Dida...
Una neno gani kwake?! !