Africa tungepewa uhuru kwa makabila badala ya mataifa bandia tungekuaje leo hii ?

Africa tungepewa uhuru kwa makabila badala ya mataifa bandia tungekuaje leo hii ?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Katika jambo baya sana wakoloni walilotufanyia Africa ilikuwa ni kugawa bara la Africa mezani katika vipande mbalimbali bandia walivyoviita nchi.

Hili ni jambo ambalo limewatesa sana Waafrika baada ya wakoloni kuondoka. Mataifa yetu yalipaswa yapatikana kwa mchakato wa asili wa sisi wenyewe kujitafuta kama sehemu nyingine duniani, kwa njia hiyo huenda tungekuwa mbali sana leo hii maana mataifa yangekuwa yanaundwa na watu wenye mtazamo mmoja na muelekeo mmoja zaidi katika mambo ya msingi, vipaumbele, utamaduni wa kujitawala na kujiongoza.
 
atika jambo baya sana wakoloni walilotufanyia Africa ilikuwa ni kugawa bara la Africa mezani katika vipande mbalimbali bandia walivyoviita nchi.
Ukisema bandia una maanisha nini! Kwamba Tanganyika ni kitu ambacho hakipo au ?
 
Ukisema bandia una maanisha nini! Kwamba Tanganyika ni kitu ambacho hakipo au ?
Mataifa artificial kwa maana sio raia wenyewe wa mataifa husika waliosababisha mataifa haya kuwepo bali waliamuliwa na watu wa nje wa bara lingine kabisa namna mataifa yao takavyokuwa.
 
wengi labda hawalielewi hili lkn mengi yanayoitwa makabila leo hii ni artifial kabla ya foreigners kuja hayakuwepo au hawakujiita hivyo at least kwa mfano tu wagogo, wagogo siyo kabila au niseme kabla ya caravan ya utumwa kupita watu wa hilo eneo hawakujiita wagogo hivyo ni matokeo ya caravani ya utumwa iliyopita hapo kutokea kongo, kgm-tbr mpaka bagamoyo i.e bila ya utumwa hao wanaoitwa/jiita wagogo leo hii wasingekuwepo hivyo wagogo ni "kabila" artificial pia huo ni mfano mdogo tu na utakuta mifano kama hiyo karibia kila mahali.

you see its even more complicated kwanza Christians hata wametusaidia sana kama ukiniuliza mimi wametutengezea kila kitu na kutuachia nchi yenye kila kitu ni sisi tu tumeshindwa kuitumia walituwekea mipaka ndani yake kuna maziwa, mito, bahari coast line ya tanzagiza ni >1400 km ktk tanga mpaka mtwara, rift valley linapita karibia nusu nzima ya nchi yetu (rift valley is the most fertile area in afrika), walitujengea reli kuunganisha bandari na mikoa karibia yote reli inapita katikati ya nchi ktk mashariki mpaka magharibi kgm, mpaka tzote zimeunganishwa reli , mashariki mpaka kaskazini moshi, arusha zote ziliunganishwa na bandari ya tanga kwa reli, plus form of government kila kitu kipo, bado unataka nini tena?

btw lugha zinatengenezwa na watu na lugha nyingi zilitengenezwa tu, kuna mengi sana hatuelewi ...
 
Mataifa artificial kwa maana sio raia wenyewe wa mataifa husika waliosababisha mataifa haya kuwepo bali waliamuliwa na watu wa nje wa bara lingine kabisa namna mataifa yao takavyokuwa.
Okay nimekuelewa. Je huo mchakato wa asili ambao tungetumia ni upi kutengeneza mataifa? Na kwanini unafikiri ingekuwa bora zaidi ya hivi!
 
Katika jambo baya sana wakoloni walilotufanyia Africa ilikuwa ni kugawa bara la Africa mezani katika vipande mbalimbali bandia walivyoviita nchi.

Hili ni jambo ambalo limewatesa sana Waafrika baada ya wakoloni kuondoka. Mataifa yetu yalipaswa yapatikana kwa mchakato wa asili wa sisi wenyewe kujitafuta kama sehemu nyingine duniani, kwa njia hiyo huenda tungekuwa mbali sana leo hii.
Du
 
Okay nimekuelewa. Je huo mchakato wa asili ambao tungetumia ni upi kutengeneza mataifa?
Vita au/na makubaliano kati ya makabila/jamii.
 
Ingekuwa tofauti sana. Nadhani nchi zingekuwa zimeendelea zaidi. Ukisoma michakato waliyokuwa wanafanya wachagga kabla ya uhuru, ilikuwa ya kusonga mbele hasa. Pia diversity sometimes ni mbaya sana. Watu hawawi na lengo moja kama nchi.

Lakini pengine vita na kugombania mipaka, maji, na rasilimali kama wanyama zingekuwa juu.
 
wengi labda hawalielewi hili lkn mengi yanayoitwa makabila leo hii ni artifial kabla ya foreigners kuja hayakuwepo au hawakujiita hivyo at least kwa mfano tu wagogo, wagogo siyo kabila au niseme kabla ya caravan ya utumwa kupita watu wa hilo eneo hawakujiita wagogo hivyo ni matokea ya caravani ya utumwa iliyopita hapo kutokea kongo, kgm-tbr mpaka bagamoyo huo ni mfano tu mdogo na utakuta mifano kama hiyo karibia kila mahali.

you see its even more complicated kwanza Christians hata wametusaidia sana kama ukiniuliza mimi wametutengezea kila kitu na kutuachia nchi yenye kila kitu ni sisi tu tumeshindwa kuitumia walituwekea mipaka ndani yake kuna maziwa, mito, bahari coast line ya tanzagiza ni >1400 km ktk tanga mpaka mtwara, rift valley linapita karibia nusu nzima ya nchi yetu (rift valley is the most fertile area in afrika), walitujengea reli kuunganisha bandari na mikoa karibia yote reli inapita katikati ya nchi ktk mashariki mpaka magharibi kgm, mpaka tzote zimeunganishwa reli , mashariki mpaka kaskazini moshi, arusha zote ziliunganishwa na bandari ya tanga kwa reli, plus form of government kila kitu kipo, bado unataka nini tena?

btw lugha zinatengenezwa na watu na lugha nyingi zilitengenezwa tu, kuna mengi sana hatuelewi ...
Hao wazungu ndio waliowagawa Wamasai katika Kenya na Tanzania, Wanyarwanda katika DRC na Rwanda, Warundi katika Burundi na Rwanda. Nigeria imekuwa taifa kituko kabisa kwa sababu Nigeria Kaskazini na Kusini zinakaliwa na watu tofauti kabisa kimtazamo upande mmoja unatazama kushoto wakati mwingine unatazama kulia, hali ni hivyo karibia nchi zote za Sub-Sahara Africa zilizoachwa na wakoloni.
 
Ingekuwa tofauti sana. Nadhani nchi zingekuwa zimeendelea zaidi. Ukisoma michakato waliyokuwa wanafanya wachagga kabla ya uhuru, ilikuwa ya kusonga mbele hasa. Pia diversity sometimes ni mbaya sana. Watu hawawi na lengo moja kama nchi.

Lakini pengine vita na kuginbania mipaka, maji, na rasilimali kama wanyama zingekuwa juu.
Unachosema kinaweza kuwa sahihi sana lakini mataifa yote duniani tofauti na Africa yamepatikana kwa vita tena vya muda mrefu tu.
 
Hao wazungu ndio waliowagawa Wamasai katika Kenya na Tanzania, Wanyarwanda katika DRC na Rwanda, Warundi katika Burundi na Rwanda. Nigeria imekuwa taifa kituko kabisa kwa sababu Nigeria Kaskazini na Kusini zinakaliwa na watu tofauti kabisa kimtazamo upande mmoja unatazama kushoto wakati mwingine unatazama kulia, hali ni hivyo karibia nchi zote za Sub-Sahara Africa zilizoachwa na wakoloni.

sawa lkn swali linakuja kabla ya hapo hali ilikuwaje? hakuna ushahidi wowote ule kama kulikuwa na advanced civilized societies isitoshe hata kabla ya ukoloni societies za kiafrika zilikuwa zinapigana vita na walioshindwa kumezwa na kuwa replaced kwa mfano wabantu asili yao ni west afrika lkn walihama west afrika kuhamia kusini ambapo (inaitwa bantu migration look it up) na hili eneo letu waliwa replace natives waliokuwpo pia kwa mfano bush men au wasandawe na wahandzabe hao ndoio native wa hili eneo tunaloishi leo hii, hata wamasai walikuwa replaced pia unajua eneo lote wanaloishi wachaga leo hii mpaka nairobi yote ilikuwa ni masai land?

lkn mnasingizia wazungu kila kitu kwa sababu mmedanganywa sana na communists, kabla ya wazungu kuja arabs walikuwepo pia na yanayoitwa makabila leo mengi tanzagiza yalianzishwa na arabs slave traders mfano mwingine wanyamwezi, wanyamwezi kabla ya utumwa hawakujiita hivyo, hivyo kabila ni artfial.

usisahau muda wazungu waliokaa east afrika haufiki hata miaka 100 hapa kwetu walikaa kama miaka kama 50 tu wote wajerumani na waingereza vita ya dunia peke yake zote 2 zilikula kama miaka 10 hivyo unaweza kusema all in all walikaa miaka kama 30/40 tu, kenya na uganda miaka kama 60 tu sasa mtu aliyekaa miaka <100 ndiyo umlaumu kwa kila kitu ktk maisha yako? what about 1000 mpaka 5000 years ago? arabs peke yao wamekaa karibia miaka 1000 lkn hamuwalaumu kwa chochote mnakuja kulaumu wazungu for everything that goes wrong in afrika ingawaje wamekaa miaka 50 tu hapa kwetu? ...
 
sawa lkn swali linakuja kabla ya hapo hali ilikuwaje? hakuna ushahidi wowote ule kama kulikuwa na advanced civilized societies, halafu mnasingizia wazungu kila kitu kwa sababu mmedanganywa n communists, kabla ya wazungu kuja arabs walikuwepo na yanyaoittwa makabila mengi yleo hii tanzagiza yalianzishwa na arabs slave traders mfano mwingine wanyamwezi, wanyamwezi kabla ya utumwa hawakujiita hivyo na siyo kabila ni artfial, usiahau muda wazungu waliokaa east afrika haifikia hata miaka 100 hapa kwenye walikaa kama miaka 50 tu wote wajerumani na waingereza, kenya uganda miaka kama 60 tu sasa mtu aliyekaa miaka <100 ndiyo umlaumu kwa kila ktk maisha yako? what abojut 1000 mpaka 5000 years ago? arabs peke yao wamekaa karibia miaka 1000 lkn hamuwalaumu kwa chochote mnakuja kulauma for everything that goes wrong in afrika ingawaje wamekaa miaka 50 tu hapa kwetu? ...
Sasa utawalaumu vipi Waarabu kwa kutengeneza makabila unayosema ikiwa hayo makabila baadaye yalikuja kuchanganywa yote kwa pamoja katika Sufuria la kupikia kama kuchanganya mchele, unga wa ugali, mihogo viazi, ngano, ndizi na mtama pamoja?!
Hao Wanyamwezi huko Tabora wangeachwa wakae wenyewe au wauangane na watu wanaokubaliana zaidi wangeweza kujiamulia mustakabali wao kwa ufanisi zaidi kuliko sasa hivi ambavyo wanatakiwa wakubaliane mambo na wewe Mnyakyusa mla kitimoto wa Mbeya
 
Back
Top Bottom