Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Hii ni ajabu sana Marekani, Kanada, Australia na sijui kanchi kanaitwa New Zealand wamekataa kumpigia kura kura Sepp Blatter na wameamua kumpa kura Mwarabu ajulikanye kama Ali bin Al Huseni kutoka nchi ya Jordani lakini kubwa na muhimu kuliko yote Waafrika (CAF) na Waasia (AFC) wameamua kubaki na kumpa shavu Sepp Blatter, hivyo hiyo inatosha kabisa kumbakisha mpiganaji Sepp Blatter ambaye kwangu mimi namkubali sana ikumbukwe ya kwamba ni Sepp Blatter ndiye aliyepigania Kombe la Dunia kuja Afrika kwa mara ya kwanza wakati Wayahudi wa Marekani walipinga hivyo hiyo kwangu mimi ni sababu tosha kabisa na kama Blatter angekuwa mla russhwa basi wangemkamata lakini wameshindwa!
Na cha ajabu kuliko vyote kabisa Nchi zilizokataa kumpa kura (Marekani, Kanada, Australia na Zealand) wala siyo wapenzi wa SOKA sasa yote haya ya nini? Si wakachague viongozi wao wa Rugby sijui hoki huko watuachie gemu yetu na Sepp Blatter wetu!
Kaeni mkao wa kula kura zinaanza saa 1600 na matokeo yanategemewa saa 2000 (Muda wa Uswisi, Ulaya)