Afrika-Asia shavu kwa Blatter majibu saa 2000!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Hii ni ajabu sana Marekani, Kanada, Australia na sijui kanchi kanaitwa New Zealand wamekataa kumpigia kura kura Sepp Blatter na wameamua kumpa kura Mwarabu ajulikanye kama Ali bin Al Huseni kutoka nchi ya Jordani lakini kubwa na muhimu kuliko yote Waafrika (CAF) na Waasia (AFC) wameamua kubaki na kumpa shavu Sepp Blatter, hivyo hiyo inatosha kabisa kumbakisha mpiganaji Sepp Blatter ambaye kwangu mimi namkubali sana ikumbukwe ya kwamba ni Sepp Blatter ndiye aliyepigania Kombe la Dunia kuja Afrika kwa mara ya kwanza wakati Wayahudi wa Marekani walipinga hivyo hiyo kwangu mimi ni sababu tosha kabisa na kama Blatter angekuwa mla russhwa basi wangemkamata lakini wameshindwa!

Na cha ajabu kuliko vyote kabisa Nchi zilizokataa kumpa kura (Marekani, Kanada, Australia na Zealand) wala siyo wapenzi wa SOKA sasa yote haya ya nini? Si wakachague viongozi wao wa Rugby sijui hoki huko watuachie gemu yetu na Sepp Blatter wetu!

Kaeni mkao wa kula kura zinaanza saa 1600 na matokeo yanategemewa saa 2000 (Muda wa Uswisi, Ulaya)
 
Dikteta tu yule, ila kafuata nyayo za alikuwa kabla yake...alikuwa rais wa FIFA for 3o Years
 
pamoja na kuhis rushwa ndio ilifanya qatar ipewe kuandaa kombe la dunia, lakini sikubaliani na fitina za usa na uropa kutotaka kumpokonya urusi asiandae kombe la dunia, kisa mgogoro wa ukraine.

marekani atutolee siasa kwenye soka, siasa zinaweza angamiza mpira wa soka duniani.
 
1. 1974 - 1977 FIFA Technical Director, Sepp
Blatter,
2. 1977 - 1981 FIFA Technical Director, Sepp
Blatter,
3. 1981 - 1985 FIFA Secretary General, Sepp
Blatter,
4. 1985 - 1989 FIFA Secretary General,
5. 1989 - 1993, FIFA Secretary General,
6. 1993 - 1998 FIFA Secretary General, Sepp
Blatter,
7. 1998 - 2002, FIFA President, Sepp Blatter,
8. 2002 - 2007 FIFA President, Sepp Blatter,
9. 2007 - 2011 FIFA President, Sepp Blatter,
10. 2011 - 2015 FIFA President, Sepp Blatter,
11. 2015 - 2019 FIFA President, Sepp Blatter
(expected).
MY TAKE.!

Kazi ipooo..., kwa mtindo huo unafikiri ataukosa tena, think we need some changes
 
Blatter anapata sapoti kubwa Africa na Asia,yule Rais wa UEFA ametishia kujitoa kwa ncni za Ulaya kombe la Dunia 2018 iwapo tu iwapo kama Blatter atashinda..
 
Mkuu Blatter ana mizizi,atachaguliwa tu...
 
6. 1993 - 1998 FIFA Secretary General, Sepp
Blatter,
.................................
8. 2002 - 2007 FIFA President, Sepp Blatter,
.....................
MY TAKE.!

Kazi ipooo..., kwa mtindo huo unafikiri ataukosa tena, think we need some changes

Hivi vipindi vya U-FIFA ni miaka minne au mitano?
 
Blatter anapata sapoti kubwa Africa na Asia,yule Rais wa UEFA ametishia kujitoa kwa ncni za Ulaya kombe la Dunia 2018 iwapo tu iwapo kama Blatter atashinda..
Matisho kibaaao wakati kipaji chenyewe cha kusakata kabumbu hawana wanategemea wachezaji wanaotoka mataifa yanayomuunga mkono Blatter!
 
Kwani hakuna viongozi wengine wa kugombea nafasi ya uraisi zaidi ya blatter.shem on you ondoa upuuzi wako hapa.
figo alikuwa anafaa sana
 
Uchaguzi wa Rais wa FIFA, UDIKTETA wa BLATTER na Wapigakura wake kutoka CAF unasadifu kabisa na chaguzi zetu za huku Afrika..!!

Sababu zinazotolewa na Wajumbe wengi kutoka Africa kwa kweli ni za kitoto na hazina mashiko kimantiki.. Hizo fedha na miradi inayotolewa utafikiri Blatter anaitoa kwenye mifuko yake..!!. Maamuzi ya miradi au misaada inayokuja Afrika na Asia hutolewa na FIFA kama taasisi wala sio mtu mmoja..

Waseme ukweli, wengi wa wajumbe wa Africa wamehongwa.. sema wanajificha kwenye eti Blatter ameisadia Africa.

Ni kununuliwa tu, hakuna kingine.

Hivi huyo Mwarabu akiingia ndiyo atabadilisha mipango na miradi yote ya FIFA.

Uchaguzi huu unaonyesha ujinga wetu wa Africa.. ni sawa sawa na chaguzi zetu za kisiasa, kuna watu wanaamini bila CCM Tanzania haitakuwepo.. Yaan ni UPOPOMPO MTUPU!!

RUSHWA NA UCHAGUZI kwa WAAFRICA ni kama UJI NA MGONJWA... Blatter ameshajiua ugonjwa wao kinachoendelea ni kuwanunua tu.

Sawasawa na RAIS wa CAF Issa Hayatou.. ni yaleyale majizi na matoa rushwa.. Kwa mfano Tanzania tunaendela kumchagua Issa Hayatou kwa lipi hasa katufanyia kukuza mpira wetu.. Kila siku ratiba zikitoka utasikia YANGA vs Zamalek wanajua ndiyo mwisho wetu hapo tutakutana mwaka unaofuata

Ujinga mtupu.. Naungana na wale wanaomkataa Blatter, tuseme imetosha miaka 20 aruhusu akili na mawazo mapya yaendeshe mpira..!!
 
Kinachonikera ni kwenye hili jambo ni kwamba motive ya Marekani na washirika wake ni kuhakikisha kuwa unapatikana uhalali wa kuipokonya URUSI (RUSSIA) haki ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2018 kwasababu ya hii vita iliyopo kati ya Russia na West. Marekani wako mbioni kutoa ushahidi kuwa hata Urisi walishinda uenyeji wa 2018 world cup kwa rushwa kama ilivyokuwa na South Africa. Ushindi wa Sepp Blatter pekee ndio utakaohakikisha Urusi haipokonywi haki hii kwani tayari walikwisha anza kuwekeza kwenye maandalizi! Endapo muarabu atashinda, itakuwa rahisi sana kwa Marekani kumtumia kwenye adhima yao ya kuipokonya Urusi haki hiyo.
Hii ni ajabu sana Marekani, Kanada, Australia na sijui kanchi kanaitwa New Zealand wamekataa kumpigia kura kura Sepp Blatter na wameamua kumpa kura Mwarabu ajulikanye kama Ali bin Al Huseni kutoka nchi ya Jordani lakini kubwa na muhimu kuliko yote Waafrika (CAF) na Waasia (AFC) wameamua kubaki na kumpa shavu Sepp Blatter, hivyo hiyo inatosha kabisa kumbakisha mpiganaji Sepp Blatter ambaye kwangu mimi namkubali sana ikumbukwe ya kwamba ni Sepp Blatter ndiye aliyepigania Kombe la Dunia kuja Afrika kwa mara ya kwanza wakati Wayahudi wa Marekani walipinga hivyo hiyo kwangu mimi ni sababu tosha kabisa na kama Blatter angekuwa mla russhwa basi wangemkamata lakini wameshindwa!

Na cha ajabu kuliko vyote kabisa Nchi zilizokataa kumpa kura (Marekani, Kanada, Australia na Zealand) wala siyo wapenzi wa SOKA sasa yote haya ya nini? Si wakachague viongozi wao wa Rugby sijui hoki huko watuachie gemu yetu na Sepp Blatter wetu!

Kaeni mkao wa kula kura zinaanza saa 1600 na matokeo yanategemewa saa 2000 (Muda wa Uswisi, Ulaya)
 
Kwani hakuna viongozi wengine wa kugombea nafasi ya uraisi zaidi ya blatter.shem on you ondoa upuuzi wako hapa.
figo alikuwa anafaa sana

Wewe ndiyo mpuuzi na wala haulewi hata unachokiongelea! kwani kuna Mtu amekatazwa kugombea FIFA? Hata marehemu baba yako pia angependa angeweza na kuna uchaguzi ambao ni lazima ashinde!
 
Uchaguzi wa Rais wa FIFA, UDIKTETA wa BLATTER na Wapigakura wake kutoka CAF unasadifu kabisa na chaguzi zetu za huku Afrika..!!

Sababu zinazotolewa na Wajumbe wengi kutoka Africa kwa kweli ni za kitoto na hazina mashiko kimantiki.. Hizo fedha na miradi inayotolewa utafikiri Blatter anaitoa kwenye mifuko yake..!!. Maamuzi ya miradi au misaada inayokuja Afrika na Asia hutolewa na FIFA kama taasisi wala sio mtu mmoja..

Waseme ukweli, wengi wa wajumbe wa Africa wamehongwa.. sema wanajificha kwenye eti Blatter ameisadia Africa.

Ni kununuliwa tu, hakuna kingine.

Hivi huyo Mwarabu akiingia ndiyo atabadilisha mipango na miradi yote ya FIFA.

Uchaguzi huu unaonyesha ujinga wetu wa Africa.. ni sawa sawa na chaguzi zetu za kisiasa, kuna watu wanaamini bila CCM Tanzania haitakuwepo.. Yaan ni UPOPOMPO MTUPU!!

RUSHWA NA UCHAGUZI kwa WAAFRICA ni kama UJI NA MGONJWA... Blatter ameshajiua ugonjwa wao kinachoendelea ni kuwanunua tu.

Sawasawa na RAIS wa CAF Issa Hayatou.. ni yaleyale majizi na matoa rushwa.. Kwa mfano Tanzania tunaendela kumchagua Issa Hayatou kwa lipi hasa katufanyia kukuza mpira wetu.. Kila siku ratiba zikitoka utasikia YANGA vs Zamalek wanajua ndiyo mwisho wetu hapo tutakutana mwaka unaofuata

Ujinga mtupu.. Naungana na wale wanaomkataa Blatter, tuseme imetosha miaka 20 aruhusu akili na mawazo mapya yaendeshe mpira..!!

Hata wewe unaoongea usichokuelewa Sepp Blatter haungwi mkono na Afrika peke yake bali na ASIA pia hivyo wawakilishi wa nusu nzima ya Binadamu wa Dunia hii wanamuunga Mkono Sepp Blatter na kwa Afrika kwangu mimi sababu ya kumkubali Sepp blatter ni moja nayo ni kwamba bila Sepp Blatter Kombe la Dunia lisingekuja Afrika kwa maana wazungu walishagoma na hata walikuwa tayari wanatafuta nchi mbadala lkn Sepp Blatter alikataa na kusema Afrika wanaweza na matokeo yake kila mtu anayajua AK waliaanda moja kati ya maonyesho yaliyofanikiwa kupita yote ktk historia ya kombe la Dunia!
 
Back
Top Bottom