Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumeona Nchi za kiafrika zilizoungana na kuishia kumezana kuuwana kubaguana.Toa maelezo kidogo mkuu
Tumeona Nchi za kiafrika zilizoungana na kuishia kumezana kuuwana kubaguana.
Mfano mzuri ni Zanzi na huku kwetu Senegal na The Gambia Eritrea na Ethiopia Somalia na Somaliland
Kwetu sisi bado sana kumbuka hata hii Jumuiya ya EAC wakati wa Magufuli alianzisha bifu lisilokuwa na maana dhidi ya Kenya na kama angeendelea kutawala hii Jumuiya ingesambaratika.Tunashindwa kipi? Mkuu unafikiri tunaweza kukifanya machafuko na kuuana wenyewe kwa wenyewe yasitokee
Umoja ni nguvu popote pale na binadamu dunia nzima tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na mazingira yetu
Ila kwa unafiki, uchoyo, umimi na ubinafsi wa binadamu hatuwezi kuungana.., bado hatujapevuka na kustaarabika kwa kiwango hicho....
Na sababu hatuwezi kuungana kwa kugawana mapato tunaweza kusaidiana katika uzalishaji na research and development..., ni aibu kuona kuna baadhi watu wana njaa wakati pengine kuna watu wanakosa masoko..., tuna shida na nishati wakati tuna gesi. maporomoko, mafuta n.k.
Kwahio not Africa..., but the World we need to Unite ingawa practically ni ngumu tokana na ubinafsi
Kwetu sisi bado sana kumbuka hata hii Jumuiya ya EAC wakati wa Magufuli alianzisha bifu lisilokuwa na maana dhidi ya Kenya na kama angeendelea kutawala hii Jumuiya ingesambaratika.
Bado tuko primitive labda miaka elfu ishirini.Kwa hivyo haiwezekani hata baada ya miaka 50 tukianza sasa et!
Yaani Kagame aungane na Museveni! Paul Biah Nguema kina Bongo nk. Unawezaje kuunganisha nchi na watu wa aina hii.
Habari zenu,
(Mzungu) mataifa ya nje yataendelea kuitumia vibaya na kujinufaisha na Africa mpaka mataifa ya Africa yatakapoamua kujiunga.
Sijui tumepumbazwa na nini? Ambacho kinakuwa kizuizi ya sisi kujiunga na kuwa kitu kimoja ambacho kitaweza kutupa misingi mizuri ya bara letu.
Utaona pindi utakapotaka kutafuta visa ya kwenda mataifa makubwa Marekani,wingereza na mataifa mengine Kuna ugumu sana mpaka kupata hiyo visa ila wao ni raisi sana kuingia nchi za Africa.
Na hii ndio inaonyesha adui ni rahisi sana kuingia mataifa yetu kuliko kwenda kwenye mataifa yao ndio maana tunaona maraisi wa Africa wanauliwa na majeshi tusiyoyatambua na sisi hata hatujishughulishi kwa kukemea wala kuchukua hatua.
Tunaona hata kwenye maisha ya kawaida familia ikiwa haielewani wanachelewa kupata maendeleo kama sio kukosa kabsa maendeleo Baba akiwa aelewani na Mama na watoto pia hawaelewani watashindwa kusaidiana pia ila tofauti yake familia ikiwa inaelewana ni raisi mno kupata maendeleo na kuinuka kwa haraka.
Viongozi walafi kujali matumbo yao kuliko maendeleo ya mataifa yao wanaofia muungano ukipita kutakuwa na kaugumu cha kupiga pesa namengineyo.
Wataendelea kuja kuwaua kinyama viongozi wa Africa kama tutaacha kuungana.. watawaua kila wanapotaka na wataendelea kuja kuvuna mali kila kukicha na idadi wa wazungu wazee kuja kuoa vibinti vitaongezeka na itafanana na vijana wa kiafrica kuoa vibibi vya kizungu.. tutaendelea kuwa wajinga mpaka tutakapoungana.
Africa tuungane wewe unataka Africa iungane au una mtazamo gani?
Shida binadamu naturally ni mchoyo na mbinafsi anajipenda yeye na wa kwake kuliko wengine..., Hivyo huenda muda ukifika binadamu watapata uelewa kwamba kwa kuungana wote tutapata zaidi kuliko kwa kutokuungana..., Pia gundua kwamba system ya Ubepari na Competition inaenda against muunganiko bali ni individuality na kuwa opportunistic....Safi sana mkuu.. maelezo mazuri sana .. kwa hivyo tuanzie wapi? Tuweze kuanza kuutengeneza muungano wa Africa hata kwa miaka 50 baadae yaani tuanze sasa