N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Jioni hii BBC Dira wamesema Afrika ina asilimia 3 ya magari yote duniani.
Ikabidi nichimbe nikakutana na hii.
Kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya 2022, kulikuwa na takriban magari bilioni 1.45 ulimwenguni, ambayo karibu bilioni 1.1 ni magari ya abiria.
Hiyo ina maana kwamba kuna gari kwa kila watu 7.18 kwenye sayari dunia.
Bara la Antaktika hadi wakati huo lilikuwa na magari 50 tu na mengi ya hayo hayatumii magurudumu.
Kwa mujibu wa Hedges & Company, karibu theluthi moja ya magari yote yako katika eneo la Asia-Pasifiki, eneo la dunia ambalo lina magari milioni 531.
Hii ni pamoja na magari milioni 21 yaliyosajiliwa nchini Australia, kulingana na data ya ABS.
Ulaya ni bara la pili kwa wingi wa magari baada ya Asia, likiwa na magari milioni 405.3 (asilimia 28) yaliyoenea katika nchi za EU na zisizo za EU.
Amerika Kaskazini - ambayo inajumuisha Kanada na Mexico - inamiliki magari milioni 351 (asilimia 24), ambayo milioni 290.8 yako Marekani.
Baada ya hapo kuna mabara yenye magari machache mno kama vile bara la AFRIKA lenye magari ASILIMIA 3 tu.
Mengi ya hayo magari ya Afrika ni mkono wa pili.
Amerika ya Kusini ina magari milioni 83
Mashariki ya Kati ina magari milioni 49.
Afrika katika uchache ina magari milioni 26 tu.
Antaktika ina magari 50 tu.
MY TAKE
• Tupunguze kodi ya magari ili kuongeza idadi ya magari hasa commercial vehicles. Magari hasa ya abiria ya kibiashara/umma ni kichocheo cha uchumi
• Tuhamasishe investors kuanzisha car assembly factories
• Tujenge miundombinu ya barabara zitakazovutia watu na taasisi kuleta magari zaidi.
MAGARI NI MUHIMU SANA KATIKA KUUKIMBIZA UCHUMI. KILA KUNAPOKUCHA MAGARI NDIYO YANAUBEBA UCHUMI WETU.
AFRIKA HOIYEE, TANZANIA HOIYEE