Afrika ina Asilimia 3 tu ya magari yote duniani

Afrika ina Asilimia 3 tu ya magari yote duniani

Sio lazima tuwe na magari mengi.
Kama kwenye magari hatupo basi tunaweza kuongoza katika uwingi wa pikipiki na bajaji[emoji38][emoji38]
 
Ni kweli maana unakuta nchi nzima ina magari labda laki sita na katika hayo laki tano yapo Capital city Bamako [emoji38][emoji38]
Mkuu najua umetoa mfano tu, lakini Mali hawajafikisha hata nusu ya hayo magari laki sita.

December 2015 Mali ilikuwa na magari 203,000.

December 2014 ilikuwa na magari 192,000

Data za Tanzania mpaka 2015 zipo kwenye link hapa chini, magari yalikuwa 380,000.

Makadirio kwa sasa Tz yatakuwa mangapi?
Maana ni magari mengi sana yameingia Tz kipindi cha miaka hii nane japo almost yote ni mikangafu
 
Tena hapo afrika imepanda kwa asilimia 1, mwaka 2000 afrika ilikuwa na magari asilimia 2 tu. Kwa tz kila magari 100 yanayoingia nchini magari 80 yanabaki dar
 
Nchi kama chuma chakavu cha BMW ya 2021 kodi yake si chini ya Tsh 50 milioni au Fusso Tipper inatakiwa eti uwe na 80 m ili uishike mkononi unategemea hiyo 3% itaongezeka wao vitu vya kujenga Nchi wameweka kodi kubwa na vinaongeza gharama ya ujenzi na usafirishaji wa bidhaa huku % kubwa ya raia wao wakijificha kwenye bajaji na bodaboda...
 
Australia ina population ya 26M na imesajili magari 21M maana yake kuna uwezekano wa kila kaya ina gari zaidi ya 1.
 
Jioni hii BBC Dira wamesema Afrika ina asilimia 3 ya magari yote duniani.

Ikabidi nichimbe nikakutana na hii.

Kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya 2022, kulikuwa na takriban magari bilioni 1.45 ulimwenguni, ambayo karibu bilioni 1.1 ni magari ya abiria.

Hiyo ina maana kwamba kuna gari kwa kila watu 7.18 kwenye sayari dunia.

Bara la Antaktika hadi wakati huo lilikuwa na magari 50 tu na mengi ya hayo hayatumii magurudumu.

Kwa mujibu wa Hedges & Company, karibu theluthi moja ya magari yote yako katika eneo la Asia-Pasifiki, eneo la dunia ambalo lina magari milioni 531.

Hii ni pamoja na magari milioni 21 yaliyosajiliwa nchini Australia, kulingana na data ya ABS.

Ulaya ni bara la pili kwa wingi wa magari baada ya Asia, likiwa na magari milioni 405.3 (asilimia 28) yaliyoenea katika nchi za EU na zisizo za EU.

Amerika Kaskazini - ambayo inajumuisha Kanada na Mexico - inamiliki magari milioni 351 (asilimia 24), ambayo milioni 290.8 yako Marekani.

Baada ya hapo kuna mabara yenye magari machache mno kama vile bara la AFRIKA lenye magari ASILIMIA 3 tu.

Mengi ya hayo magari ya Afrika ni mkono wa pili.

Amerika ya Kusini ina magari milioni 83

Mashariki ya Kati ina magari milioni 49.

Afrika katika uchache ina magari milioni 26 tu.

Antaktika ina magari 50 tu.

MY TAKE
• Tupunguze kodi ya magari ili kuongeza idadi ya magari hasa commercial vehicles. Magari hasa ya abiria ya kibiashara/umma ni kichocheo cha uchumi

• Tuhamasishe investors kuanzisha car assembly factories

• Tujenge miundombinu ya barabara zitakazovutia watu na taasisi kuleta magari zaidi.

MAGARI NI MUHIMU SANA KATIKA KUUKIMBIZA UCHUMI. KILA KUNAPOKUCHA MAGARI NDIYO YANAUBEBA UCHUMI WETU.

AFRIKA HOIYEE, TANZANIA HO

Hapo Dar foleni zimewashinda na bado mnatamani kuongeza magari?!
 
Nchi kama chuma chakavu cha BMW ya 2021 kodi yake si chini ya Tsh 50 milioni au Fusso Tipper inatakiwa eti uwe na 80 m ili uishike mkononi unategemea hiyo 3% itaongezeka wao vitu vya kujenga Nchi wameweka kodi kubwa na vinaongeza gharama ya ujenzi na usafirishaji wa bidhaa huku % kubwa ya raia wao wakijificha kwenye bajaji na bodaboda...
Hii ya magari ya biashara kupigwa ushuru mkubwa inaumiza sana. Imagine coaster mayai used inatafuta 80 pia tipper hata dogo la tani 5 bila milioni 50 huchukui, hizi kodi za importation inafaa ziangaliwe upya
 
Waondoe VAT kwenye New Cars
Na waweke flat ni 30% ya CIF hapo gharama zote hadi usajili
 
Wamejaribu Climate change tumewastukia.

Sasa wanadai hatuna Magari.

Davos Marketing Strategy.

Miaka 10 ijayo makampuni mengi yatakuwa yakitengeneza magari ya Umeme. Kutakuwa hakuna uhitaji wa magari ya peteroli

Miaka 10 ijayo kutakuwa na mitumba ya Magari kwao , yatakuwa yanajaza ardhi yao, kama inavyotokana na nguo(kuna dampo(mashariki ya ulaya) hayaozi, utakuwa kama uchafuzi wa mazingira vile, kama maplastiki na nguo zinazo wakaba roho kwa uchafuzi wa mazingira huo sasa wanakuja na magari

Ni sawa nakutafuta dampo lao huku wao wakijuchulia fedha(tax incentives)ikiambatana na cop-15 starategy na matokeo ya mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani.

Huku sisi tunakuja kuharibu Mazingira(Ukweli safari hii)

Tusubiri wakianza kuuza kama mitumba ya nguo. Labda
 
Hii ya magari ya biashara kupigwa ushuru mkubwa inaumiza sana. Imagine coaster mayai used inatafuta 80 pia tipper hata dogo la tani 5 bila milioni 50 huchukui, hizi kodi za importation inafaa ziangaliwe upya
Wamedumaza maendeleo hatuna viongozi hapo unawezaje kulipia Tipper eti 50m wakati Nchi wanayouza hayo magari used yanauzwa kama chakavu viongozi hawawezi kupunguza kwa sababu wataona wanapunguza mapato yanayopatikana kirahisi ila inakera sana ndio maana unaona wengi wanajificha kwenye fusso wakiacha ma Truck ya maana hata ukiangalia hizi bara bara zinazojengwa pana muda magari yenye namba za kigeni ndio yatajaa kuleta mizigo huku Watanzania wakibaki kusifia 113 Scania ya 1982 sijui huko wakati tupo kwenye G 460 Scania..wanazotumia Wasomali wanaoishi Tanzania na Watanzania wachache sana...
 
Barabara na sehemh za kuya paki kwanza...
Tuna eneo pana. Mimi kilo changu washushe ushuru angalau kwa magari ya MIZIGO na ABIRIA(Commercial) ili tuwezeshe uchumi kutembea kwa haraka. Ushuru wetu wa magari uno juu sana, unakosa uhalisia wa maisha halisi ya Mtanzania.

Ushuru wa magari hasa ya Biashara ukishuka, MKULIMA, MFANYABIASHARA MDOGO na MWEKEZAJI Wataleta mavumba zaidi kwenye uchumi.

Huu ushuru wa TRA wa magari Used kwa sasa hauna uhalisia. Huwezi ukaagiza gari chakavu la Milioni 50 eti na ushuru uwe milioni 50 au zaidi, huku ni kukomoana.
 
Back
Top Bottom