Afrika iwafundishe Mashariki ya Kati utu, waachane na miungu yao ya uharibifu

Afrika iwafundishe Mashariki ya Kati utu, waachane na miungu yao ya uharibifu

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Kwa hali inavyoendelea huko Mashariki ya Kati hata Ukraine, kuna kitu kinakosekana. Nadhani wenzetu kuanzia Wazungu, Waarabu na Wahindi wana kasoro moja. Hawana utu bali ubaguzi, ubinafsi, ufahari, na ukatili. Rejea mfano, Wazungu walivyotutawala, kutuibia, na kutupeleka utuwani au wanavyoendelea kutunyonya.

Angalia walivyopindua serikali za Kiafrika zilizokataa kuwekwa nyumba ndogo na kuhujumu watu wake kama mijibwa kama Mobutu, Kamuzu Banda, Houphouet-Boigny, Bokassa, Omar Bongo na wengine kama hao.

Angalia walivyotuletea dini zao na kujenga chuki baina yetu tukaanza kuchukianana kudharauliana kwa misingi ya dini. Angalia, kama mbwa, walivyotupachika majina yao ili kututambua watakapotuhitaji mbali na kutugawana.

Angalia mabaki mfano ya Waarabu au Wahindi yanavyotubagua wakati yananeemekea kwenye ardhi yetu mbali na kutoturuhusu kuishi kwao.

Angalia Waarabu wa Mashariki ya Kati wanavyotesa Waafrika wanaofanya kazi majumbani au wale wa Maghreb wanaotuita hayawani.

Angalia wanavyotuibia na kuficha kwao, mfano Wahindi wanaoficha hata Ulaya. Mifano ni mingi. Cha mno, hawa watu wasipoachana na miungu yao ya ukatili na visasi ambapo ukikosea inakuchoma moto, watamalizana.

Kama wangekuwa hawana ubaguzi na dharau, Waafrika tulipaswa kwenda kuhubiri utu dunia nzima lau kuwapa wahusika utu na namna ya kujitambua na kuwatambua wenzao.

Je, wewe unashauri nini?
 
Back
Top Bottom