Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Status
Not open for further replies.

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

UPDATE:

NTV Kenya, ambao ndio walitangaza habari hizi kupitia runinga yao wameonesha kutotoa taarifa sahihi, habari hii inafungwa kwakuwa imekosa uthibitisho.

President Uhuru Kenyatta is the recipient of Mandela democracy
 
Kamati ya Tuzo za Mandela, Afrika Kusini imempa Rais @MagufuliJP Tuzo ya Amani ya Mandela 2017 (Mandela Peace Prize 2017) kutambua jitihada zake katika kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati hiyo ilipokea maombi takribani 5000 kuwania tuzo hizo.
Source [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG].

2e57cadeab5d9c88db0e61c67b988ec2.jpg
 
Hivi yule mwandishi wa habari amepatikana?
Ili nijue kweli kuna amani!
Huu ni uzushi, hakuna cha tuzo hapo, tundu lissu mwenyewe hajapona bado, ben wa saanane mpaka leo hajapatina, hiyo itakuwa tuzo ya lumumba🙂)😀
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom