Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Status
Not open for further replies.
Tuzo za hovyo na za kipuuzi sanaa, hadi nkurunzinza kapata nae tuzo?
 
Hadi Pierre Nkurunziza?

Ujasiri upi? WA kung'ang'ania kuongoza baada ya muhula wake kuisha? Au ujasiri wa kubadili katiba?
 
Hawa waafrika Kusini wamemdhalilisha Shujaa marehemu Mandela. Tuzo anapewa mpaka Nkuruzinza!
 
Wangempa na yoweri mseven tuzo ya kung'ang'ania kukaa madarakani ingependeza. Ingewatia moyo wanaotaka kuongeza muhula wa miaka 7.
 
Hadi Nkurunzinza kapewa tuzo ya ujasiri, no wonder dikteta mwrnzake Magufuli kapewaa pia
 
Magufuli na Nkurunziza siamini kabisa kama kuna mtu mwenye Akili zake timamu anaweza kuwazawadia tuzo!
 
mpaka tuzo wananunua ha ha ha ha..jamani ni utani tu msijeniokota cocobeach kwenye kiroba ha ha natania jamani....hii nayo ni amani pia ha ha.......
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).


this is a fake news,sio kweli kabisa elewa Mandella Brand ni kubwa mno kitu kama hiki kingechukua nafasi ndani ya SA press,lakini nipo hapa Lingusenguse na google kuangalia press ya SA imeliongelea hili sipati kabisa from news24.com,iol.co.za,enca.com,sowetain.co.za .sabc nothings at all,chanzo wapi cha habari hii au ni yuotube!!!!,good news Liberia got the new president MR.G.WEAH,bad news the richest man in Africa he lost more money than more than 13 African countries!!!in just of few days
 
I wish ingekuwa kweli.Wanaovunjiwa nyumba ndiyo hao wanyonge,ajabu na kweli
Mbona wengine eneo hilo hilo hawakuvunjiwa?
Kamati ya Tuzo za Mandela, Afrika Kusini imempa Rais @MagufuliJP Tuzo ya Amani ya Mandela 2017 (Mandela Peace Prize 2017) kutambua jitihada zake katika kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati hiyo ilipokea maombi takribani 5000 kuwania tuzo hizo.
Source [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG].

2e57cadeab5d9c88db0e61c67b988ec2.jpg
 
Mbona MNAZINGUA[\COLOR] hizo ni njugu ehe? FF0000[\MOBILE[\COLOR]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom