Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Status
Not open for further replies.
Hivi yule mwandishi wa habari amepatikana?
Ili nijue kweli kuna amani!
Huu ni uzushi, hakuna cha tuzo hapo, tundu lissu mwenyewe hajapona bado, ben wa saanane mpaka leo hajapatina, hiyo itakuwa tuzo ya lumumba🙂)😀
Amani hulindwa kwa njia nyingi.Cha msingi uhakikishe amani inakuwepo.Amani haina njia moja ya kuilinda.Amani yaweza lindwa hata kwa risasi.Waliotoa tuzo wanajielewa na waelewa amani.Polisi na wanajeshi wanaitwa walinzi wa Amani zana zao za kuhakikisha amani inakuwepo ni pamoja na kutumia silaha zao. Zile silaha nazo sina mchango mkubwa sana kuhakikisha amani inakuwepo
 
Unauhakika??
Unataka kusema walivunjiwa bila kigezo cha ukomo!
Serikali IPO tu hata kosa kinyemela ukasubiri huruma.
Utilitarianism
is an ethical theory which states that the best action is the one that maximizes utility
"Utility" is defined in various ways, usually in terms of the wellbeing of people or entinties,
Utility here is the sum of all pleasure that results from an action, minus the suffering of anyone involved in the action.
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

Pongezi kwake
 
Inaonekana ni HABARI KUBWAAAAAAAAAAA....lakini hadi nashiriki kutoa maoni ndiyo kwanza ina page tatu, hapo ina masaa mawili tangu iwe posted. Wakati habari ya Tundu Lissu kuanza mazoezi jana, ndani ya nusu saa iliweza kujaza zaidi ya kurasa tatu. Mjipime aisee.
 
Magufuli ni chaguo la Mungu wasiopenda wahame nchi maana bado ana miaka 7 ya kuingoza nchi hii
Mbona una comment kwa hasira Sana?
mtu akiwa chaguo la Mungu haiamanishi kwamba hawezi kupingwa, mbona Yesu alipingwa?
Wanaompinga Magufuli waacheni waendelee kumpinga, ishu siyo kuhama nchi kenge la kihaya wewe.
 
Amani ya kummiminia Lissu risasi, amani ya kuota miili ya watu kwenye viroba, amani ya kuambia tusiseme vyuma vimekaza.
Hongera kwa UK ulistahili, wewe ni Baba wa Demokrasia hapa EAC.
 
For sure this Africa!!.... Nimeona sehemu mpaka nkurunziza yumo katika tuzo😛😛😛😛
 
Tuzo ya Rais wa Burundi Imenikosha zaidi.... Hongera Nkurunzinza
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

Umenikumbusha Trump alipoachana na Republican akajiunga na CCM ili kumuunga mkono Yohana ktk shughuli anazozifanya pale Tz
 
Ni kama zile tuzo za kina Ali Kiba na Daimond wanazogombaniaga huko marekani na ulaya.

Ni kama vile siku hizi hata chekechea kuvaa joho. zimekosa dhamani kabisa.

Mkuu, wewe ushawahi pewa tuzo ngapi au hata acknowledment tu kutoka kwa ndugu zako??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom