Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Status
Not open for further replies.
Tangu nizaliwe sijawahi kuona tuzo za ovyo na zinazogawiwa kama njugu namna hii. Hii inashusha credibility ya wataalam na wasimamizi wa hiyo tume ya mandela. Ni mwendelezo wa kututukanisha waafrika kwamba tunafikiri kwa kutumia masaburi. Pia wamemdhalilisha hayati Mandela. Ovyo kabisa, poor African leaders!
 
Mzungu aliposema ' Africa is a Dark Continent' hakukosea
South Africa wamemdhalilisha Nelson Mandela
Shame on You South Africa
All in all we as Tanzanians tunaujua ukweli
Mtu mwenye tetesi za kunanihiiii leo mnampongeza???
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

Huyo ndo Raisi wangu, na nita destroy takataka wote watakaojaribu kuzuia mafanikio yetu!
 
Hii haiwezi kuwa habari nzuri kwa wapinga kila kitu.
 
Tuzo nyingi zinazotolewa hapa duniani kuanzia zile za Nobel, Mo hata hizi ukiangalia kwa jicho la tatu ni za kinafiki kupindukia .
 
endelea kufanya kazi rais wangu, kundi kubwa sana la wazalendo lipo nyuma yako.
 
Sishangai maana hata nkuruzinza kapewa
 
Ccm imepata tuzo ya uonevu wa kidemokrasi? Kama hapana basi ccm imehonga hizo tuzo
 
Mzungu aliposema ' Africa is a Dark Continent' hakukosea
South Africa wamemdhalilisha Nelson Mandela
Shame on You South Africa
All in all we as Tanzanians tunaujua ukweli
Mtu mwenye tetesi za kunanihiiii leo mnampongeza???
Hii hatari sana mkuu
 
Inaonekana ni HABARI KUBWAAAAAAAAAAA....lakini hadi nashiriki kutoa maoni ndiyo kwanza ina page tatu, hapo ina masaa mawili tangu iwe posted. Wakati habari ya Tundu Lissu kuanza mazoezi jana, ndani ya nusu saa iliweza kujaza zaidi ya kurasa tatu. Mjipime aisee.
Ukiona uzi unaomtaja Magufuli siku hizi lazima udode maana watu wamemchoka ile mbaya!
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

Nice
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom