Kwa tuliowahi kuishi nchi za kusini mwa Afrika tulikuwa tukijua toka kale kuwa kuufinya na kuufinyanga uchumi wa Zimbabwe waliumiza sana Wazimbabwe lakini lengo lilikuwa ni kuipiga mkwara SA not to do the same. Watu hawakununua ardhi bali waliipora lakini eti hairuhusiwi sehemu ya ardhi waliyopora igawawiwe kwa kwa wazawa ambao ndiyo wengi na hawana ardhi.
Kutoka Beitbridge mpaka Cape Agulhas kwa mtu aliyeishi tu nchi ya kijamaa kama Bongo lazima atashangaa, ardhi yote iko fenced na vibao vya 'do not trespass it's private property' ni common na unajua trespassing ni criminal offense.
Kwenye kulinda interests za Wazungu hata kama ni Wazungu waishio/raia wa nchi za Afrika hapo utabaini kuwa Wazungu wote huungana hata kama ni kwa kuitesa kiuchumi nchi ya Afrika alimradi wanapigania interests za Wazungu wenzao na baadhi ya Africans huwa hawausomi mchezo kwa kuwa media hufanya brainwashing kwa propaganda na kulaumu huo mpango wa land redistribution.
The funny part ni kwamba ardhi yote waliipora lakini kurudisha a portion of that land hawakubali.
Zimbabwe walikubaliana na Britain kwenye Lancaster House Agreement kwamba baada ya uhuru wawaachie Wazungu ardhi kwa miaka kumi then ndiyo waigawanye(that was Mugabe's great mistake kwani walipaswa kuipora immediately walipopata uhuru na kusingekuwa na kelele) na British ilidai italipa fidia kwa land owners ili igawanywe after ten years Britain waka-change kibao Mugabe akakauka akawapa tena ten years mingine wajipange hapo ndiyo wakamchomolea mazima na hiyo kumbuka war veterans wanazidi kuzeeka na makubaliano wakati wa mapambano ya uhuru ni kuwa wao ndiyo watapewa umuhimu wa kwanza kwenye kugawiwa ardhi kwani wanachopigania ni ardhi na si tu kubadili rangi ya bendera na kumtoa mzungu katika kuongoza nchi. Veterans wakampiga mkwara Mugabe mpaka akawakubalia ardhi wakaichukua kibabe, kumbuka war veterans huwa na nguvu sana kuliko hata wanasiasa kwenye nchi zilizomwaga damu katika kutafuta uhuru.
Viva antingo de combatentes💪.