Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
Usiku mwingine, kimtazamo wa kiroho huwa haifai kuangaliwa moja kwa moja. Ukishika udongo unahisi joto la wafu wa kale. Ukikalia jiwe la porini, linaloonekana zuri jioni, usiku linakuwa ni mgongo wa kiumbe kisicho na jina, kinacholia kama mtoto aliyezaliwa tumboni mwa ndoto. ardhi ya udongo haijawahi kuwa ya kawaida ni tumbo la siri nzito, giza linalotafuna nuru kidogo kidogo kama ugonjwa usio na jina.
Misitu yake si ya kijani tu ndani kuna vichwa vya waliokatwa usiku, vikililia haki. Kuna miti mikubwa inayolia ukipita karibu, hasa ukiwa na siri moyoni. Kuna njia panda ambazo ukizikanyaga vibaya, unaweza kurudi ukiwa sio wewe. Eti kiroho wanaamini ya kale eti inakumbatia maiti na kuwasalimia wachawi kwa ndimi za moto. Kuna mapango ya vizuka vilivyorudi tumboni mara saba na ndondocha wanaolia kwa sauti ya kuku aliyechinjwa bila tambiko.
Katika vijiji vya kale kiimani, bado wapo wanaokula nyama za watu si kwa njaa, bali kwa nguvu za giza. Wapo wanaofukia viembryo kwenye vyanzo vya maji ili mvua inyeshe. Kuna madawa ya kienyeji yanayotengenezwa kwa kuchanganya vipande vya kucha za maiti, nywele za wachawi waliouawa, na damu ya paka mweusi wa usiku wa mwezi mweusi.
Ooh udongo mweusi eti Wazee walisema Ukiona kivuli chako kimejipinda bila sababu, kuna mtu anakuita kutoka upande mwingine wa maisha. Wapo waliokataa kutoa tambiko wakazaa watoto wa miguu mitatu. Wapo waliokataa kuamini mizimu wakakuta maiti ya ndoto kwenye vitanda vyao. Usiku mwingine unaweza kuamka ukiwa umezungukwa na mawe saba, kila moja likiwa na jicho moja, linalokutazama bila kupepesa.
Mizimu hailali. Wachawi hawafi. Mahoka hawasahau. Miti ya tambiko bado inanyonya damu ya walioanguka miaka mia moja iliyopita. Makaburi mengine huzaliwa siyo kuchimbwa. Na kuna vijito vinavyobeba macho ya waliodhulumiwa, vikitembea polepole kuelekea mlango wa nyumba yako.
Karibu kwenye simulizi za imani za kle ambayo watu huogopa kuisema kwa sauti.