Afrika ndio atakayepata hasara katika vita kati ya Ukraine na Urusi

Afrika ndio atakayepata hasara katika vita kati ya Ukraine na Urusi

Jelavic

Senior Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
183
Reaction score
380
Kinachoendela hivi sasa kati ya urusi na Ukraine katika ile miji ya donbas ni hatari kwa africa. Urusi imeitambua miji ya Donetsk na Luhansk kama nchi huru zinazojitegemea, haya maeneo kijiografia yamepakana na urusi lkn kwa makubaliano ya umoja wa mataifa baada vita ya pili ya dunia ni sehem ya nchi ya Ukraine tangu kuanguka dola la soviet.

Raia wa haya maeneo wanaiunga mkono urusi bali ni warusi kihistoria na hata kitamaduni lkn serikali ya ukraine pamoja ya kuwa ilikuwa ni sehem ya dola la kisoviet ila miaka ya karibuni imekuwa ikibadili siasa zake na kuelekea upande wa magharibi, chanzo hasa cha yote ni Ukraine ilipodhamiria kuomba kujiunga na umoja wa NATO na hii ndio sabab kubwa iliyotonesha kidonda cha putin kilicho kuwa kimeanza kukauka, kwanini?

Kwasabab kama ukraine ikijiunga na NATO maana yake matumain ya urusi kurudisha dola yake ya soviet yatakuwa yameisha lkn pia uwezekano wa urusi kumegwa zaidi katika miaka ijayo ungekuwa ni mkubwa, urusi iliridhia ukraine iwe nchi huru lakin isiingie katika umoja wa NATO, sasa turudi kwenye maudhui.

Kwaiyo kitendo cha urusi kuzitambua nchi hizo imepelekea marekan na umoja wa ulaya kuchukua hatua mbali mbali za mwanzo kama kufunga benk tano za urusi zilizopo ulaya, kuganindisha account za wafanya biashara wakubwa wakirusi waliopo ulaya ,kuiondoa urusi katika mfumo wa mabadilishano ya miamala ya kifedha wa dunia(swift system) n.k, kwa mtazamo wa magharibi sio tu urusi inavunja heshima ya uogongozi wa nchi huru bali inachofanya ni tishio la aman ya nchi zingine za Ulaya.

Ikumbukwe Ukraine iko ulaya ila haiko katika umoja wa majeshi ya NATO.
Tangu jana na leo mapambano ya silaha katika haya maeneo ya donbas inaendelea, habari ya yanayojiri tunaendelea kuzipata katika vyombo vya habari vya dunia , ama kuhusu maudhui yangu

KIVIPI AFRICA ITAUMIA NI KAMA IFUATAVYO?
Asilimia 21 ya ges inayotumika ulaya inatoka Ukraine. Asilimia 55 ya gesi inayoingia ulaya inatoka urusi kupitia ujeruman ( ndio bomba refu zaidi duniani ambalo linatokea urusi hadi ulaya). Kama ulaya wataendelea kutoa adhabu kwa urusi na kama urusi atandelea kuishambulia Ukraine maana yake ulaya atapata upungufu wa gesi kwa zaid ya silimia 70, maana yake nini?

Maana yake ulaya atalazimika kutafuta soko mbadala la gesi na mafuta, hapa ataelekea mashariki ya kati(nchi za kiarabu).
Kwa lugha nyingine mahitaji ya gesi yataongezeka bei itapanda zaidi , maana yake na uchumi wa nchi za africa utaporomoka kwa kadri bei ya mafuta itakavopanda yan gharam zitakuwa juu.

Kabla ya hii vita bei ya jumla ilipanda hadi kufika dola 100 kwa bilmmil moja nadhan mnatambua serikali ya Tanzania hatua ilizochukua angalau kupunguza athari ya moja kwa moja kwa mtanzania wa kawaida ikaondoa baadhi ya tozo katika mafuta ambazo ni haki ya seikal ili kupunguza mzigo kwa wanachi , maana yake tunakoelekea bei itapanda na hali itakuwa mbaya.

Hali hio ambayo pamoja na ubaya wake mm naiona inaunafuu sabab mafuta yatakuja lakn yatakuwa ghali, lakin wachambuzi wanasema ili ulaya itosheke na kiasi cha gesi inayopata saiz kutoka urusi na Ukraine basi inabidi nchi za kiarabu kwa ujumla wao zisipeleke gesi kokote isipokuwa Ulaya.

Hapo ndio inakuja ile kauli ya mama etu kwamba ambae kamba yake ni ndefu ndio atakula zaidi, tunaweza tukaingia katika hali mbaya zaidi ya kichumi.

Na sehemu ya mwisho ambayo Africa italipia gharama ya hii vita ni kupitia mikataba ya madini tunayo sain na makampuni ya ulaya, sehem kubwa ya makapuni haya tumekubaliana katika KUGAWANA FAIDA, uchumi ukiyumba ulaya watatumia hio nafasi kama fimbo ya kutuchapia watasema hawajaingiza faida kutokana kupanda kwa gharam za uchakataji sabab ya kupanda kwa nishati n.k na tusije kushangaa tukaambiwa yamepata hasara. Nadhani katika hili eneo ni vema mamlaka zikawa macho zaidi ili tusipigwe.

Mungu ibariki africa mungu ibariki Tanzania.

1645709992356.jpg
 
Ukraine ni Taifa la Zamani zaidi ya Urusi na lenye historia ndefu kuzudi Urusi. Putin anafanya Propoganda tu kusema Ukraine ilikuwa sehemu ya Urusi.
 
CCM itanufaika sana umasikini wa Watz ukizidi.
Hii nifuraha kwa CCM
😳😳😳

Wewe jamaa wa ajabu kweli .....umekurupukia kutoka "ubanda" wa komoni nini ?!!!

CCM ndiyo inayolinda maslahi endelevu ya watanzania kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.....

#Siempre CCM🙏
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom