Afrika ndio atakayepata hasara katika vita kati ya Ukraine na Urusi

Afrika ndio atakayepata hasara katika vita kati ya Ukraine na Urusi

Nato hawapokei simu za rais wa Ukraine watu wanasema labda ajaribu kutuma sms..🤣🤣
Wiki mbili mbali huko!
🤣🤣🤣

Ndio maana tuendelee tu kulipenda taifa letu pendwa Tanzania....kwani hata wanasiasa "wanaotumiwa nao" na mwisho kukimbilia UGHAIBUNI huishia tu kupata STRESS baada ya kuendelea kuishi mafichoni huku wakipewa ULINZI MKATE NA SIAGI tu.....🤣🤣

#KutumiwaKubaya
#UsalitiMbaya
 
hakuna cha safari we mwenyewe umeona jamaa anadai viongozi karibu wote nchi ulaya wameshimdwa kumjibu.Unadhani nini kinaendelea si wanaogopa
Jamaa kajiaibisha mno...

Hili ni FUNZO kwa sisi vijana tunaopiga makelele ya "domookraasia" muda wote......

Wanadoomokrasia wamemtelekeza swahiba yao 🤣🤣🤣
 
Biden: Nilizungumza na viongozi wa G7 leo, na tukakubaliana kikamilifu kuwa;

○Tutapunguza uwezo wa Urusi kuwa sehemu ya uchumi wa dunia.
○Tutadumaza uwezo wao wa kufadhili na kukuza jeshi la Urusi.
○Tutahathiri uwezo wao wa kushindana katika teknolojia ya hali ya juu kwenye uchumi wa karne ya 21.

Kutokana na maneno haya ya Biden na freezing kwa akaunti kwenye mabenki Russia itapata pigo ila kwa issue ya military power is hidden issues sababu kuja watu/nations they're silently to see what's going kwa mataifa chokozi na chonganishi.
 
Kinachoendela hivi sasa kati ya urusi na Ukraine katika ile miji ya donbas ni hatari kwa africa.
Urusi imeitambua miji ya Donetsk na Luhansk kama nchi huru zinazojitegemea, haya maeneo kijiografia yamepakana na urusi lkn kwa makubaliano ya umoja wa mataifa baada vita ya pili ya dunia ni sehem ya nchi ya Ukraine tangu kuanguka dola la soviet.
Raia wa haya maeneo wanaiunga mkono urusi bali ni warusi kihistoria na hata kitamaduni lkn serikali ya ukraine pamoja ya kuwa ilikuwa ni sehem ya dola la kisoviet ila miaka ya karibuni imekuwa ikibadili siasa zake na kuelekea upande wa magharibi, chanzo hasa cha yote ni Ukraine ilipodhamiria kuomba kujiunga na umoja wa NATO,na hii ndio sabab kubwa iliyotonesha kidonda cha putin kilicho kuwa kimeanza kukauka, kwann..?
Kwasabab kama ukraine ikijiunga na NATO maana yake matumain ya urusi kurudisha dola yake ya soviet yatakuwa yameisha lkn pia uwezekano wa urusi kumegwa zaidi katika miaka ijayo ungekuwa ni mkubwa, urusi iliridhia ukraine iwe nchi huru lakin isiingie katika umoja wa NATO, sasa turudi kwenye maudhui.
Kwaiyo kitendo cha urusi kuzitambua nchi hizo imepelekea marekan na umoja wa ulaya kuchukua hatua mbali mbali za mwanzo kama kufunga benk tano za urusi zilizopo ulaya, kuganindisha account za wafanya biashara wakubwa wakirusi waliopo ulaya ,kuiondoa urusi katika mfumo wa mabadilishano ya miamala ya kifedha wa dunia(swift system) n.k, kwa mtazamo wa magharibi sio tu urusi inavunja heshima ya uogongozi wa nchi huru bali inachofanya ni tishio la aman ya nchi zingine za ulaya.
Ikumbukwe Ukraine iko ulaya ila haiko katika umoja wa majeshi ya NATO.
Tangu jana na leo mapambano ya silaha katika haya maeneo ya donbas inaendelea, habari ya yanayojiri tunaendelea kuzipata katika vyombo vya habari vya dunia , ama kuhusu maudhui yangu
KIVIPI AFRICA ITAUMIA NI KAMA IFUATAVYO...?
Asilimia 21 ya ges inayotumika ulaya inatoka Ukraine.
Asilimia 55 ya gesi inayoingia ulaya inatoka urusi kupitia ujeruman ( ndio bomba refu zaidi duniani ambalo linatokea urusi hadi ulaya). Kama ulaya wataendelea kutoa adhabu kwa urusi na kama urusi atandelea kuishambulia Ukraine maana yake ulaya atapata upungufu wa gesi kwa zaid ya silimia 70, maana yake nini..?
Maana yake ulaya atalazimika kutafuta soko mbadala la gesi na mafuta, hapa ataelekea mashariki ya kati(nchi za kiarabu).
Kwa lugha nyingine mahitaji ya gesi yataongezeka bei itapanda zaidi , maana yake na uchumi wa nchi za africa utaporomoka kwa kadri bei ya mafuta itakavopanda yan gharam zitajuwa juu.
Kabla ya hii vita bei ya jumla ilipanda hadi kufika dola 100 kwa bilmmil moja nadhan mnatambua serikali ya Tanzania hatua ilizochukua angalau kupunguza athari ya moja kwa moja kwa mtanzania wa kawaida ikaondoa baadhi ya tozo katika mafuta ambazo ni haki ya seikal ili kupunguza mzigo kwa wanachi , maana yake tunakoelekea bei itapanda na hali itakuwa mbaya.
Hali hio ambayo pamoja na ubaya wake mm naiona inaunafuu sabab mafuta yatakuja lakn yatakuwa ghali, lakin wachambuzi wanasema ili ulaya itosheke na kiasi cha gesi inayopata saiz kutoka urusi na Ukraine basi inabidi nchi za kiarabu kwa ujumla wao zisipeleke gesi kokote isipokuwa ulaya.
Hapo ndio inakuja ile kauli ya mama etu kwamba ambae kamba yake ni ndefu ndio atakula zaidi, tunaweza tukaingia katika hali mbaya zaidi ya kichumi.
Na sehem ya mwisho ambayo africa italipia gharama ya hii vita ni kupitia mikataba ya madini tunayo sain na makampuni ya ulaya, sehem kubwa ya makapuni haya tumekubaliana katika KUGAWANA FAIDA, uchumi ukiyumba ulaya watatumia hio nafasi kama fimbo ya kutuchapia watasema hawajaingiza faida kutokana kupanda kwa gharam za uchakaji sabab ya kupanda kwa nishati n.k na tusije kushangaa tukaambiwa yamepata hasara.
Nadhani katika hili eneo ni vema mamlaka zikawa macho zaidi ili tusipigwe.

Mungu ibariki africa mungu ibariki Tanzania.

View attachment 2130693
Vita ina gharama yake.....

Itaanzia kwa hao wapiganao na kufikia hadi kwetu....

Kikubwa tu DUNIA haijaweza kuwa sehemu salama wakati wote....changamoto za vipindi aina hii ni vya kujifunza na KUJIFUNGA MIKANDA TU .....

#Siempre JMT🙏
 
Biden: Nilizungumza na viongozi wa G7 leo, na tukakubaliana kikamilifu kuwa;

○Tutapunguza uwezo wa Urusi kuwa sehemu ya uchumi wa dunia.
○Tutadumaza uwezo wao wa kufadhili na kukuza jeshi la Urusi.
○Tutahathiri uwezo wao wa kushindana katika teknolojia ya hali ya juu kwenye uchumi wa karne ya 21.

Kutokana na maneno haya ya Biden na freezing kwa akaunti kwenye mabenki Russia itapata pigo ila kwa issue ya military power is hidden issues sababu kuja watu/nations they're silently to see what's going kwa mataifa chokozi na chonganishi.
Hakika UCHAWI si tu kuruka na ungo usiku na kupiga wengine "mwangeni"......

Magharibi hawataki kuiona URUSI ikipiga hatua ya maana kimaendeleo 🤣🤣
 
Awapi subiri utaona Urusi ana nini cha maana? akipewa hapo hata Ufarasa pekee inamtosha
Russia alitoka akaenda kumlinda Maduro Us kama wana jeuri hiyo waende wapeleke majeshi Ukrain
Jamaa kajiaibisha mno...

Hili ni FUNZO kwa sisi vijana tunaopiga makelele ya "domookraasia" muda wote......

Wanadoomokrasia wamemtelekeza swahiba yao 🤣🤣🤣
Hakuna anayetaka vita mkuu kila mtu anaogopa nukes
 
Hivi Israel wao huwa hawasaidii nchi zingine?
Israel ana kimeo chake Iran, bora NATO watulie ngoma isije kuwa vita ya tatu ya dunia maana unaelewa Iran na Hamas watapiga makombora yao kuelekea wapi...
 
hakuna cha safari we mwenyewe umeona jamaa anadai viongozi karibu wote nchi ulaya wameshimdwa kumjibu.Unadhani nini kinaendelea si wanaogopa
Sio wameogopa ndugu yangu wamechagua busara ya kumkalia kimya mjinga mwenye matusi.Baada ya hili Putin ataanza kulalamikiwa duniani kote na hata raia wake watamnanga.Anajichapa mwenyewe ngoja lipoe hili utaona
 
Kinachoendela hivi sasa kati ya urusi na Ukraine katika ile miji ya donbas ni hatari kwa africa.
Urusi imeitambua miji ya Donetsk na Luhansk kama nchi huru zinazojitegemea, haya maeneo kijiografia yamepakana na urusi lkn kwa makubaliano ya umoja wa mataifa baada vita ya pili ya dunia ni sehem ya nchi ya Ukraine tangu kuanguka dola la soviet.

Raia wa haya maeneo wanaiunga mkono urusi bali ni warusi kihistoria na hata kitamaduni lkn serikali ya ukraine pamoja ya kuwa ilikuwa ni sehem ya dola la kisoviet ila miaka ya karibuni imekuwa ikibadili siasa zake na kuelekea upande wa magharibi, chanzo hasa cha yote ni Ukraine ilipodhamiria kuomba kujiunga na umoja wa NATO,na hii ndio sabab kubwa iliyotonesha kidonda cha putin kilicho kuwa kimeanza kukauka, kwann..?

Kwasabab kama ukraine ikijiunga na NATO maana yake matumain ya urusi kurudisha dola yake ya soviet yatakuwa yameisha lkn pia uwezekano wa urusi kumegwa zaidi katika miaka ijayo ungekuwa ni mkubwa, urusi iliridhia ukraine iwe nchi huru lakin isiingie katika umoja wa NATO, sasa turudi kwenye maudhui.

Kwaiyo kitendo cha urusi kuzitambua nchi hizo imepelekea marekan na umoja wa ulaya kuchukua hatua mbali mbali za mwanzo kama kufunga benk tano za urusi zilizopo ulaya, kuganindisha account za wafanya biashara wakubwa wakirusi waliopo ulaya ,kuiondoa urusi katika mfumo wa mabadilishano ya miamala ya kifedha wa dunia(swift system) n.k, kwa mtazamo wa magharibi sio tu urusi inavunja heshima ya uogongozi wa nchi huru bali inachofanya ni tishio la aman ya nchi zingine za Ulaya.

Ikumbukwe Ukraine iko ulaya ila haiko katika umoja wa majeshi ya NATO.
Tangu jana na leo mapambano ya silaha katika haya maeneo ya donbas inaendelea, habari ya yanayojiri tunaendelea kuzipata katika vyombo vya habari vya dunia , ama kuhusu maudhui yangu

KIVIPI AFRICA ITAUMIA NI KAMA IFUATAVYO...?
Asilimia 21 ya ges inayotumika ulaya inatoka Ukraine.
Asilimia 55 ya gesi inayoingia ulaya inatoka urusi kupitia ujeruman ( ndio bomba refu zaidi duniani ambalo linatokea urusi hadi ulaya). Kama ulaya wataendelea kutoa adhabu kwa urusi na kama urusi atandelea kuishambulia Ukraine maana yake ulaya atapata upungufu wa gesi kwa zaid ya silimia 70, maana yake nini..?

Maana yake ulaya atalazimika kutafuta soko mbadala la gesi na mafuta, hapa ataelekea mashariki ya kati(nchi za kiarabu).
Kwa lugha nyingine mahitaji ya gesi yataongezeka bei itapanda zaidi , maana yake na uchumi wa nchi za africa utaporomoka kwa kadri bei ya mafuta itakavopanda yan gharam zitajuwa juu.

Kabla ya hii vita bei ya jumla ilipanda hadi kufika dola 100 kwa bilmmil moja nadhan mnatambua serikali ya Tanzania hatua ilizochukua angalau kupunguza athari ya moja kwa moja kwa mtanzania wa kawaida ikaondoa baadhi ya tozo katika mafuta ambazo ni haki ya seikal ili kupunguza mzigo kwa wanachi , maana yake tunakoelekea bei itapanda na hali itakuwa mbaya.

Hali hio ambayo pamoja na ubaya wake mm naiona inaunafuu sabab mafuta yatakuja lakn yatakuwa ghali, lakin wachambuzi wanasema ili ulaya itosheke na kiasi cha gesi inayopata saiz kutoka urusi na Ukraine basi inabidi nchi za kiarabu kwa ujumla wao zisipeleke gesi kokote isipokuwa Ulaya.
Hapo ndio inakuja ile kauli ya mama etu kwamba ambae kamba yake ni ndefu ndio atakula zaidi, tunaweza tukaingia katika hali mbaya zaidi ya kichumi.

Na sehemu ya mwisho ambayo Africa italipia gharama ya hii vita ni kupitia mikataba ya madini tunayo sain na makampuni ya ulaya, sehem kubwa ya makapuni haya tumekubaliana katika KUGAWANA FAIDA, uchumi ukiyumba ulaya watatumia hio nafasi kama fimbo ya kutuchapia watasema hawajaingiza faida kutokana kupanda kwa gharam za uchakaji sabab ya kupanda kwa nishati n.k na tusije kushangaa tukaambiwa yamepata hasara.
Nadhani katika hili eneo ni vema mamlaka zikawa macho zaidi ili tusipigwe.

Mungu ibariki africa mungu ibariki Tanzania.

View attachment 2130693

Jambo hili linaweza kuwa na athari pamoja na faida pia. Uchambuzi wako umejikita katika kutazama kesho ya afrika kwa kutazama nini kinafanayika au kitafanyika nje ya afrika. Uchambuzi wako kwa kutazama nini kitanyika nje ya afrika uko sahihi lakini hujatazama changamoto hizi zinaweza kuleta nini afrika.

Waafrika tumekuwa wazito sana katika kutazama mbele na kuchukua hatua stahiki.

mzozo wa ulaya mimi naona unaweza kuikomboa afrika. Chukulia nchi kama Tanzania tuna gesi ya sili na upo uwezekano wa kutumia gesi ya asili badala ya mafuta. nakumbuka zamani sana nilisikia mpango wa kubadirisha magari yetu ili yatumie gesi ya asili badala ya mafuta lakini hatutekelezi.

bora bei za mafuta zipande ili tuwe na akili za kufanyia kazi mipango yetu ukiwemo kutumia gesi kuendesha magari na mitambo
 
Back
Top Bottom