Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Huko wanafuata nini? Hakuna watumishi wengine wa umma?

Ni self justifications tu zisizo na maana na kutotaka kugatusha madaraka pamoja na resources
Kawaida mambo yakiharibika huwa jamii ailaumu watumishi wa umma bali wanasiasa (mawaziri).

Halikadhalika kama kuna photo opportunity serikali imefanikiwa kwenye jambo watataka wachukue hizo credit.

Ni kwamba hizo safari azikwepeki
 
Sijawahi kuelewa kwa nini hizi gari zinagharama hivyo. Kwa wingi wa magari tunayonunua kutoka Toyota, ungetegemea tupewe discount kubwa ila inaonyesha si hivyo, gharama ni kama tena zinaongezeka.

Wanaokula hizi hela za nchi hawatazifaidi wao wala vizazi vyao. Hizi pesa zina laana.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?.

With all due respect Pascal 600 M for one car😳 let's check out the reality HIYO HELA HAKUNA. Piga mahesabu kuanzia DC, wabunge na wengineo wakitumia GXR bajeti tunayospendi kwenye magari KIASI Gani?

I saw an article from the Citizen where Tanzania is one amoung the countries which spend a lot of money for buying expensive cars to government officials
Pasingekuwa na issue ya kukopa kila siku hata sisi wanyonge tungefikiri kama Pascal..tuache mzaha kwenye mambo yanayotushushia hadhi duniani.
 
Kuna wakati waziri wa nchi mojawapo ya Ulaya alifika Tz, akaombwa msaada na akakubali kufikisha hilo ombi nchini kwake. Siku ya kuondoka walikutana na Waziri wa Tz anaenda Ulaya, wa Tz alipanda first class na WA Ulaya alipanda second class. Angalia sasa Mwafrika anaenda kuomba msaada nje.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy!. Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P
Ndio maana madaraka yanapiganiwa sio kutumikia bali kutumikiwa! Huku ni kutumikiwa. Viongozi wana deserve kuwezeshwa lakini huku ni kudekezwa katikati ya lindi la umaskini!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua hilo gari la serikali unaonyesha kumshambulia RC kana kwamba ni lake wakati akikoma kuwa rc analiacha serkalini.Hii Roho ya kushambulia viongozi bila Elimu mnapata wapi?
Akili zako ndio zinavyokwambia watu wanamshambulia Rc?.watu wanaongelea manunuzi ya magari ya anasa kwenye uchumi wa tozo wewe unawaza uRC.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy!. Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P
Kwanini viongozi watembelee armored cars wakati nchi inajiasibu kisiwa cha amani?

Serikali inapendwa hizo bullet proof za nini?

Kuhusu kushambuliwa TAL hiyo ilikuwa mipango ya kishetani iliyopangwa na shetani mkuu na wenzie na kwa nyakati tofauti kauli zao zilithibitisha hilo.

Kaa ukijua kutorejea kwa Mr Lissu kutoka ughaibuni sio kwa bahati mbaya he is well informed kuanzia plot nzima na hadi masalia ya walioshirik8 kumuangamiza japo wengi wao ndio hivyo wao ndio wametangulia kwenda udongoni.

CCM muache kuchukulia watanzania bado wana akili za enzi za 1970'.
 


Baada ya kuyapiga picha mjini, kuna upande mwingine hayo Magari yanaenda. Njia mvua ikinyesha mtihani. Hapo walikwama kwa masaa mawili.

Ukiweka magari ambayo siyo imara hakuna sehemu watafika kwa wakati na udhani kama hayo magari yenyewe yatamudu.

Kwa kuangalia tu hizi ziara zao haya magari ya viongozi hasa mawaziri sitoshangaa kabisa kama kwa mwaka yanapiga zaidi ya 10000 miles +.

Kasheshe uwe una ziara ya week halafu gari sio comfortable na hayo makongoro ya njiani sio muda unatengua kiuno na safari yenyewe inakuwa ngumu ukifika kwenye hiyo ziara ata kwenye kazi inaweza kuwa shida.

Halafu hilo gari alifiki tsh 600 million
Kwahiyo hapo ufumbuzi kwa kiongozi wa serikali ni kununua gari itakayomtipitisha yeye binafsi kwenye hiyo barabara mbovu nasio kutengeneza barabara ili itumike kwa wananchi wote?
 
Back
Top Bottom