Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Nikiwa Rais naondoa huu upuuzi wa magari..kila mtu ajinunulie gari lake au adandie daladala..

Mbona wafanyakazi wengine wanatumia gharama zao kufika maeneo yao ya kazi?.

Gari zitakuwa chache tu na zitakuwa hazina mwenyewe..ukitokea uhitaji wa kusafiri kikazi ndo utatumika tu and not otherwise.
Naona unaota,,hebu amka..
 
Mtu kazaliwa kijijini, kakulia chumba kimoja na mbuzi leo ana madaraka anataka atembelee gari ya million 600, ambayo hajaitolea jasho, ni kodi za maskini wenzake.View attachment 2476045View attachment 2476044
Na wewe pambana ufike huko juu,ule mema ya nchi,
Binadamu kwa uhalisia wake,ni kiumbe mbinafsi,hata kama umezaliwa kwenye ufukara,sio kwamba hupendi mali,ukwasi,ukipata fulsa tu,ni kupiga.
Mtoto wa Raisi Biden,anachunguzwa kwa ma deals aliyofanya na serikali ya Ukraine,wakati Baba yake akiwa makamu wa Raisi,Kuna tetesi Biden alitumia nafasi yake kuzishinikiza baadhi ya nchi kufanya biashara na makampuni ya familia yake la sivyo USA itazinyima hizo nchi msaada wa kijeshi.
Nchi hii dawa ni kuingia mtaani kuandamana na kupindua serikali,
Unakuta waziri,anasema wananchi watakopeshwa simu janja!!yaani ameona shida kubwa ya wananchi ni simu janja,mama muuza vitumbua,mahindi,kijana wa boda boda,simu janja inamsaidia nini?
 
Mil 600 ni hala ndogo sana kwa Serikali, ni sawa na wewe unavyokula wali nyama home au unavyomiliki infinix.
Kama ni ndogo kwanini watoto bado wanakosa madarasa ya kusomea hadi wanapeana shift kuingia darasani?

Milioni 600 ingeajiri walimu wangapi kwa kuwalipa mshahara huo kwa mwezi?

Milioni 600 kwa haraka ingeweza kuajiri walimu zaidi ya mia 500 kwa kumlipa kila mwalimu let say milioni moja na pointi kadhaa hivi.

Ingenunua madawati mangapi ikapunguza adha ya madawati kwa shule za serikali?
 
Unajuaga kutetea upuuzi.
Mimi ni mtu wa enzi za Mwalimu, kuwa na private car ilionekana ni ufahari na hata kuwa na TV ilikuwa inahesabika ni anasa!. Kumbe usafiri ni kitu muhimu sana for mobility na if you can afford to get the best, why not?. Escort ya Nyerere ilikuwa Peugeot 404, mawaziri wa Nyerere walitumia Peugeot 504!. Benz ya rais ilikuwa E Class 240, Tajiri Lord Rajpar akaleta nchini S Class 720, alikamatwa na kutiwa ndani kwa kosa la kumiliki gari la ufahari kuliko la Mkuu wa nchi.

Sasa TV sio anasa, magari ni mobility rais anatumia S Class ya 720, Speaker na CJ wao ni S Class 500!, kwanini wabunge, mawaziri, ma PS na wakurugenzi wasitumie ma V8?. Viongozi wetu wangekuwa wanatumia magari armored, Tundu Lissu angefanywa vile?.

Mimi naishi njia ya Bagamoyo, kila Mzee wa Msoga akieanda na kurudi kutoka Msoga, huku rodini ni shughuli!, nikashauri kwanini asitumie chopper?. Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!
Nashauri wenye uwezo na private jet walete wenye uwezo na Chopper walete, watu wa V8 walete na sisi wa TZ 11, bajaj, boda boda na dala dala, pia tuendelee!.
P
 
Mtu wa kawaida kumwelewa Pascal Mayala sio rahisi ila wale ambao ni gifted wanampata sawa sawa kabisa. Kwenye elementary of economics kuna dhana 2 za muhimu sana, Rsource are always scarce but needs are unlimited halafu kuna opportunity Cost-the forgone choice. Sasa sijui kama Pascal alimaanisha kwamba kwamba sisi hizi kanuni tumeshazifikia au la
Mkuu Patrick Girigo , mimi sio mchumi, kama serikali yetu ni tajiri na tuna fedha za kununua midege kwa cash, why not drive the best cars around?.
P
 
Nikiwa Rais naondoa huu upuuzi wa magari..kila mtu ajinunulie gari lake au adandie daladala..

Mbona wafanyakazi wengine wanatumia gharama zao kufika maeneo yao ya kazi?.

Gari zitakuwa chache tu na zitakuwa hazina mwenyewe..ukitokea uhitaji wa kusafiri kikazi ndo utatumika tu and not otherwise.
Siku ukigombea nitonye. Sema sasa ukiingia madarakani waweza basilica mara moja. Ogopa sana!
 
Kuambatana na Rais haina maana uwe na hadhi sawa na Rais.

Wewe umeona hilo gari pekee ndo lenye hadhi ya mkuu wa mkoa?

Akitembelea Prado, Harrier ama Vitz hawezi kuwa na hadhi ya mkuu wa mkoa?
Kwamba hizo gari zinauweza mwendo wa msafara wa rais na pakawa na usalama!?..una uelewa wowote na magari!?..mkuu wa mkoa atembelee vitz akizuru mkoa wake,unafikiri sawasawa!!?
 
Hebu lipeni kodi acheni kubwabwaja

Siku zote wanadam ndo mlivyo ,ukiona mwenzako anafaidi huchelewi kumtilia figisu,viongozi ni watoto wa masikini ,waacheni waendelee kula mema ya nchi hadi pale milija itakapo katika,hata tuwaweke nyie wana jf kwenye ulamba asali ,mtatufanyia mambo ya ajabu hadi tutamani kufa

Waacheni watembelee 600ml ,ni mda wao,mda ukiisha watatoka
 
Back
Top Bottom