Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Huko wanafuata nini? Hakuna watumishi wengine wa umma?

Ni self justifications tu zisizo na maana na kutotaka kugatusha madaraka pamoja na resources
Kawaida mambo yakiharibika huwa jamii ailaumu watumishi wa umma bali wanasiasa (mawaziri).

Halikadhalika kama kuna photo opportunity serikali imefanikiwa kwenye jambo watataka wachukue hizo credit.

Ni kwamba hizo safari azikwepeki
 
Sijawahi kuelewa kwa nini hizi gari zinagharama hivyo. Kwa wingi wa magari tunayonunua kutoka Toyota, ungetegemea tupewe discount kubwa ila inaonyesha si hivyo, gharama ni kama tena zinaongezeka.

Wanaokula hizi hela za nchi hawatazifaidi wao wala vizazi vyao. Hizi pesa zina laana.
 
Pasingekuwa na issue ya kukopa kila siku hata sisi wanyonge tungefikiri kama Pascal..tuache mzaha kwenye mambo yanayotushushia hadhi duniani.
 
Kuna wakati waziri wa nchi mojawapo ya Ulaya alifika Tz, akaombwa msaada na akakubali kufikisha hilo ombi nchini kwake. Siku ya kuondoka walikutana na Waziri wa Tz anaenda Ulaya, wa Tz alipanda first class na WA Ulaya alipanda second class. Angalia sasa Mwafrika anaenda kuomba msaada nje.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy!. Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P
Ndio maana madaraka yanapiganiwa sio kutumikia bali kutumikiwa! Huku ni kutumikiwa. Viongozi wana deserve kuwezeshwa lakini huku ni kudekezwa katikati ya lindi la umaskini!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua hilo gari la serikali unaonyesha kumshambulia RC kana kwamba ni lake wakati akikoma kuwa rc analiacha serkalini.Hii Roho ya kushambulia viongozi bila Elimu mnapata wapi?
Akili zako ndio zinavyokwambia watu wanamshambulia Rc?.watu wanaongelea manunuzi ya magari ya anasa kwenye uchumi wa tozo wewe unawaza uRC.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy!. Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P
Kwanini viongozi watembelee armored cars wakati nchi inajiasibu kisiwa cha amani?

Serikali inapendwa hizo bullet proof za nini?

Kuhusu kushambuliwa TAL hiyo ilikuwa mipango ya kishetani iliyopangwa na shetani mkuu na wenzie na kwa nyakati tofauti kauli zao zilithibitisha hilo.

Kaa ukijua kutorejea kwa Mr Lissu kutoka ughaibuni sio kwa bahati mbaya he is well informed kuanzia plot nzima na hadi masalia ya walioshirik8 kumuangamiza japo wengi wao ndio hivyo wao ndio wametangulia kwenda udongoni.

CCM muache kuchukulia watanzania bado wana akili za enzi za 1970'.
 
Kwahiyo hapo ufumbuzi kwa kiongozi wa serikali ni kununua gari itakayomtipitisha yeye binafsi kwenye hiyo barabara mbovu nasio kutengeneza barabara ili itumike kwa wananchi wote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…