Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Alafu kiongozi anaawambia vijana wajiajiri wakalime mihogo na viazi mviringo wafuge na bata mzinga 😂😂😂😂 wao wakikuona unatoka jasho nguo zimepasuka ndo wanakusifia...
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy! Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P
Kwanini huwa mnawaza hivi? Uingereza hata waziri wa fedha hatembelei gari aghali kama hili. Matajiri wana bana matumizi, masikini kama sisi ndio matumizi yetu balaa. Hatujihurumii.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy! Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari ya viongozi wetu wakiwemo wabunge, mawaziri yote yawe ni armored.

P
Hao wezi waendelee kulindwa ili waibe zaidi au,wanashambuliana wao kwa wao kwa tamaa zao za madaraka,wananchi wa kawaida wananufaika padogo sana na uwaziri wao au ubunge na vyeo vingine mbali mbali vya utumishi wao wa umma.
Viongozi Wengi ni majizi na mafisadi wasio kinao madaraka wala vyeo.

Hakuna la maana wanalo fanya zaidi ya kuendelea kuwatia umasikini watanzania kwa kuwalipisha kodi kubwa,vikokotoo vya ajabu,na sheria kali kali kwa masikini na kwa watendaji wa makosa madogo madogo ya kibinadamu na huku wao wakiiba mabillion na hakuna wa kuwashitaki wala kuwafunga .

Wanatumia vibaya sana pesa za walipa kodi,viongozi wetu hawana uchungu na mtanzania wala Tanzania yenyewe .Acha wapige mana ndo mda wao ,
 
Ni asili yetu, magari kama haya yakipungua sana Serikalini kote ni 300. Sasa piga hesabu mzee wangu hiyo hela si inatosha kusambaza maji vijiji vyote TZ.
 
Ni asili yetu, magari kama haya yakipungua sana Serikalini kote ni 300. Sasa piga hesabu mzee wangu hiyo hela si inatosha kusambaza maji vijiji vyote TZ.
Mbona hamuulizi makaa ya mawe na uranium inayosombwa inasimamiwa na nani na je faidi inaelekea wapi
 
Tuache roho ya chuki.

Hayo magari ndo standard ya viongozi.

Tena yalipaswa kuwa bora kuliko hayo.

Ni magari ya serikali siyo ya kwao pia tukumbuje, bi maana ni katika mali za serikali.
 
Huu upuuzi ulianza enzi za JK, ukakua zaidi kipindi cha Jiwe na sasa unaendelea.

Usimwamini Mwafrika ndugu.

Magufuli kwenye kampeni 2015 alisema ataondoa ma V8 na alipoingia ndiye aliyebariki mpaka ma DAS kuanza kutembelea ma V8.

Mungu-Mzungu-mwarabu-mwafrika-Sokwe
Hivi unaakili kweli, ninani aliyemfukuza kazi das wa geita kwa kuwa na gari la bei kubwa
 
Back
Top Bottom