Kwa kiuhalisia, shida ni wivu.
Kwa kiuhalisia, shida ni porojo.
Kwa kiuhalisia, shida ni Uwongo wa Kupandikiza.
Hayo mabilioni hata hawa manabii uchwara kwa mabakuli yao tu....V.800??? Kibao. Sembuse serikali.
Mbadala unaoletwa ni wa kukejeli, wa kuduwaza kama sio kudumaza. Porojo tu
Inanishangaza, kuona baadhi ya wanahudhuri na viherehere vyao, Ati, kwa sababu Hao Viongozi ni Masikini, wametoka vijijini, washamba n.k basi V.8 haziwafai- Ni wivu tu huo.
Wanavyo linganisha na kutofautisha-mtu au Kiongozi katoka wapi; na Gari anayostahili tena kwa lugha ya ukimbari ni karaha tupu! Wivu tu huo tena wa kukaripiwa. Wanapeana dole tupu Aaati?
Mwisho wa siku hakuna anayeleta mbadala bila kejeli au mbadala usio na kejel au dhihaki- halafu ndio unategemea Serikali iwatilie maanani? Tunapandikiza chuki tu
Kama ni vya kujadiliwa, viwe vinajikita kwenye mchakato mzima wa upatikanaji wa hayo Magari au? Mie naona humo ndio kuna hitilafu.
Kuna jamaa amesema miaka ya nyuma tulikuwa na 'European cars' Je anajua kwa nini ilikuwa rahisi kupatikana kwa magari hayo? Unajua Tanganyika motors? Unajua kwa nini Serikali ilitumia TM? Kwanini walibadilisha?
Eniweyi nimetupia tu hilo mtajijiju.
Kiuhalisia hakuna Serikali isiyokuwa na Matumizi- Yeyote ile, hata NGO's
Kiuhalisia inakuwa vizuri Serikali kujitathmini kila baada ya mda kuona kama kuna ulazima wa kuwa na hayo Magari yenye, kama wengi wanavyodai ni ya Kifahari mno na wala hayamfai.mtu aliyotoka Kijijini. Pathetic fikra gani hizo???
Kitaeleweka.
Yaani Blangeti Kubwa Afrika....halafu unaonyeshwa Toyota ya R.C Tanzania wapi na wapi?
Nape tunakuomba wewe na Kamati yako mfanye kazi kwa Haraka. Najua unalo Kabrasha la kulimwaga Davos.
Mtujuze