Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Ni ajabu kuona Afrika kuwa ni bara lenye rasilimali nyingi, tukiwa na ardhi yenye rutuba, madini, mafuta, na nguvu kazi kubwa ila masikini upande wetu Mungu katunyima viongozi wenye kujua waafrika tunataka nini.
Afrika ni bara ambalo limekuwa likitegemea misaada kutoka nchi za Magharibi katika sekta ya afya, ikiwa ni pamoja na tiba ya VVU/UKIMWI, dawa za ARV, na matibabu ya kansa. Ingawa misaada hii ina umuhimu wake, ni muhimu kuzingatia kwamba Afrika ina uwezo wa kifedha na rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kusaidia kugharamia huduma za afya bila kutegemea nchi za nje.
Ni ajabu kuona eti ili wananchi wa Manyara ili wapate huduma bora za kiafya dhidi ya changamoto za magonjwa ya kifua kikuu, pamoja na VVU basi ni lazma wapate msaada kutoka mfuko wa USAID, ilihali wananchi hao hao wanalipa kodi kadhaa kwa serikali? Malaika wa zamu wanatushangaa sana Waafrika.
Yaani ili tuone mabadiliko kwenye sekta ya afya Tanzania inahitaji mpango kazi wa USAID wa mwaka 2021-2026? wakati ambao vyombo na mamlaka za kukusanya kodi zinajipiga kifuani kuwa zinakusanya kodi na kuvunja rekodi? Afrika ni chaneli maalumu ya vichekesho na huzuni mbinguni.
Miongoni mwa sekta kubwa za afya zinazohitaji fedha ni matibabu ya saratani, pamoja na VVU na UKIMWI ila sio ajabu kuona serikali za mataifa kama Algeria, Libya, Misri pamoja na Afrika Kusini zikililia wahisani watoe misaada ilihali wana hifadhi kubwa ya madini ya dhahabu, hakika kwenye miti mingi hakuna wajenzi. Katika miaka ya hivi karibuni, mataifa ya Afrika yameweza kufanya maendeleo makubwa katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya HIV.
Rasilimali za kifedha zinazohitajika katika kugharamia huduma za afya zipo ndani ya Afrika, tumezikalia wenyewe. Nitakupa mfano, Mtoto wa mlipakodi akihitaji upasuaji atapewa rufaa na utazunguka naye kwenye hospitali na ndani humu Tanzania, ila mtoto wa waziri ambaye saini yake ipo kwenye pesa huwezi kukuta anazungushwa Mara Bugando, eti aendee KCMC mara rufaa ya kwenda Muhimbili imekwama. Ila kwako wewe kapuku mwenzangu hii ndo hatma yetu.
Mataifa mengi yana rasilimali za asili ambazo zinachangia uchumi wao. Kwa mfano, mataifa ya Nigeria, Angola, na Ghana ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani, huku baadhi ya nchi kama Zambia, Afrika Kusini, na Botswana zikiwa na madini muhimu kama shaba na almasi.
Pamoja na hili, nchi nyingi za Afrika zina nafasi nzuri ya kuongeza uwekezaji katika sekta ya afya kwa kutumia mapato yatokanayo na rasilimali hizi, badala ya kutegemea misaada kutoka nchi za nje. Mungu ametubariki na kila kitu ila amewanyima akili viongozi wetu wanaendeshwa na tamaa zao binafsi.
Kupitia utalii, Afrika inayo nafasi ya kutengeneza mifumo ya afya ya kifedha itakayojitegemea. Nchi kama Morocco, Kenya, na Tanzania zimefanikiwa kuvutia watalii na kupata mapato mengi kutoka katika sekta hii. Mapato haya yanaweza kuingizwa katika sekta ya afya ili kuboresha huduma na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata matibabu bora.
Ila bado tunategemea misaada kwa kiasi kikubwa kutoka kwa mashirika kama JICA kutoka Japan, KOICA kutoka Korea Kusini, pamoja na USAID kutoka Marekani, tena kwenye mambo ambayo kwa kodi zetu hizi hizi kila kitu kinaweza kufanyika kwa wepesi.
TRA na mamlaka zingine zinatoka hadharani na kuweka wazi kuwa wanavunja rekodi za ukusanyaji wa kodi, hizi pesa zinakwenda wapi? Au mnaziweka kwa ajili ya kikazi kijacho? Au kwa ajili ya familia zenu? TRA ni mali ya Watanzania, sio mali ya mtu mmoja au wawili bali watanzania wote!
Sidhani kama utapata amani ukisikia mama fulani amefariki dunia kisa kashindwa kufika kituo cha afya kisa barabara mbovu mkoani Geita ikiwa TRA mnakusanya mapato kutoka AngloGold Ashanti tena mabilioni ya pesa, ama na hii mnasubiria wahisani?
Afrika inahitaji kuwekeza katika mifumo yake ya afya kwa kutumia rasilimali zilizopo, na kuachana na utegemezi wa misaada ya nje. Nchi za Afrika zina uwezo wa kutengeneza mifumo ya afya inayojitegemea, inayowafaidi wananchi wake, na kuboresha maisha ya watu kwa ujumla.
Hii haihitaji nguvu kubwa kama kupika ugali wa muhogo, bali tunahitaji viongozi wenye maono na huruma kwa wananchi, viongozi wenye kujua uchungu wa maisha ya watanzania.
Uliowapatia akili hawana maamuzi na uliowapa nafasi ya maamuzi hawana akili.