Afrika yafaidika na maendeleo ya China katika sekta ya sayansi na teknolojia

Afrika yafaidika na maendeleo ya China katika sekta ya sayansi na teknolojia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111347107459.jpg

Mwezi Oktoba mwaka jana, aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) Bill Burns alisema kuwa, Shirika hilo linaanzisha vituo viwili vikubwa, kimoja kikilenga China na kingine teknolojia zinazoongoza.

Hatua hiyo iliashiria kuwa, kiongozi huyo anaamini kuwa, uwanja mkubwa wa ushindani kati ya China na Marekani utakuwa katika maendeleo ya teknolojia. Swali ambalo Wamarekani wanapaswa kujiuliza ni kwamba, je China itashinda katika mbio hizo?

Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Belfer cha Chuo Kikuu cha Havard inayoitwa “Ushindani Mkubwa katika Teknolojia” imejibu swali hilo, kuwa inawezekana China ikashinda mbio hizo. Ripoti hiyo inasema, China imepiga hatua kubwa katika sekta ya sayansi na teknolojia, na kwa sasa ni mshindani mkubwa katika zama hizi.

China imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na uvumbuzi tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China miaka zaidi ya 70 iliyopita. Hatua hiyo imeifanya China itangulie duniani kwenye sekta za teknolojia ya kisasa ya akili bandia, 5G, kulipa kwa kutumia njia ya kidigitali, reli za mwendo kasi, magari yanayotumia nishati mpya, teknolojia ya fedha na nyinginezo.

Nchi nyingi za Afrika zimefaidika kutokana na maendeleo ya teknolojia ya China, hususan katika ujenzi wa miundombinu. Kwa mfano, Kenya imeweza kuwa na reli ya SGR kutoka Mombasa hadi mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, iliyojengwa na kampuni ya China, ambayo imesaidia mno kupunguza muda wa usafiri kati miji hiyo miwili. China pia imesaidia ukarabati wa bandari ya Lamu nchini Kenya na kuongeza ubora wake na uwezo wa kupokea meli kubwa za mizigo. Ukarabati wa bandari hiyo umesaidia kuondoa shinikizo kubwa kwa bandari ya Mombasa ambayo ni kitovu cha usafirishaji na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya Kenya.

Pia katika sekta ya anga ya juu, China imepata mafanikio makubwa, hivyo, katika miaka ya karibuni, ushirikiano kati ya nchi hiyo na Afrika katika sekta ya anga ya juu umeendelea kupanuka kwenye maeneo ya utafiti, kuendeleza na kutengeneza satelaiti, na hii inahimiza uwezo wa nchi za Afrika wa kujiendeleza katika mambo ya anga ya juu.

Mwezi Desemba mwaka 2019, Ethiopia ilirusha satelaiti yake ya kwanza kwenye anga za juu kupitia Kituo cha Anga za Juu cha China. Muhimu zaidi ni kwamba, satelaiti hiyo ilibuniwa kwa pamoja na wahandisi kutoka China na Ethiopia.

Kwa hakika, China imekuwa mwenzi wa kutegemeka kwa nchi za Afrika kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia nchini humo.
 
Back
Top Bottom