Mwanamke mmoja Raia wa Kenya ajulikanaye kwa Jina la Beatrice Mutuku asimuklia yaliyomkuta Nchini Saudi Arabia alipoenda kufanya kazi za ndani, Beatrice anadai kwenye nyumba hiyo aliyokuwa akifanya kazi alimkuta mfanyakazi mwengine aitwaye Sharmin ambaye Bosi wake alidaiwa kumuua.
“Bosi wangu alikuwa ananifungia muda wowote anatoka nyumbani, nilikuwa nafanya kazi na mwanadada mwingine nikimuuguza mtoto wa bosi wangu, siku moja nilisikia sauti, baadaye nilisikia mtoto akilia, nikamuita mwenzangu, lakini hakujibu kisha akanijibu huku akiogopa na kuniambia atakufa siku hiyo kisha nikasikia mlango ukigongwa kwa nguvu na sikumsikia tena yule binti,” alikumbuka vyema”
Beatrice alisema mlango wake ulifunguliwa ghafla, na kumuona mtoto akivuja damu, huku mfanyakazi mwenzake (Sharmin) akiwa amelala chini.
“Bosi na Mkewe walitoa mtoto nje ya nyumba na wakaniambia mwili wa mwenzangu Sharmin niupeleke Chooni” alisema Beatrice.
“Haikuniingilia akilini kuwa Bosi anaweza kumfanyia Sharmin kitu kama kile, Sharmin alilala pale chini, nilianza kuwaza kwanini Sharmini haonekani anapumua na kwanini walikuwa wakiniita badala yake, nilijaribu kuita jina lake kwa sauti ya chinichini kwa sababu niliogopa kumchunguza mbele ya Bosi na Mkewe lakini niliogopa Beatrice anasema.
Beatrice alisita kuubeba mwili huo hadi chooni kwa sababu alihofia angeweza kuacha alama za Vidole vyake kwenye mwili wa Sharmin na nguo zake.
Beatrice aliogopa maana sauti ya kwanza aliyosikia ilikuwa ni Mlio wa Risasi kwani Sharmin alikuwa kimya kwa muda, licha ya hofu yake Beatrice aliuvuta mwili baada ya kupigwa bila huruma na Bosi huyo katili.
“Waliponiomba nimvute Sharmin nilimvuta na mara moja nikiwa chooni nilifungiwa naye, alikuwa ni binti mdogo tu hana hata mtoto. nilikaa hapo kwa muda wa siku tatu na mwili huo hadi ukaanza kupata harufu, kwa kweli, nilikuwa nikinywa maji ya chooni, na sikuweza hata kulala, na hadi sasa, nina picha hiyo akilini,” alisimulia Beatrice.
Baada ya Siku tatu Bosi wake ambaye siku hizo hakuwepo nyumbani na Familia yake, alifika kwa ajili yake na kumpa masharti Magumu kabla ya kuachiwa huru, jambo embalo alikubali kwa usalama wake.
Chanzo: BONGO 5