Afungwa Jela miaka 30 kwa kumbaka mfanyakazi wake wa ndani

Afungwa Jela miaka 30 kwa kumbaka mfanyakazi wake wa ndani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mkazi wa Miembesaba mkoani humo, Otienal Ibrahimu (36), baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mfanyakazi wake wa ndani mwenye umri wa miaka (15).

Hukumu hiyo imetolewa Julai 31, 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Fahamu Kibona huku upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Elizabeth Olomi, akisaidiana na Asifiwe Mzava na upende wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Iddi Msawanga.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, ilielezwa kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 15, 2023 alfajiri nyumbani kwao huko Miembesaba, baada ya mke wake kuelekea kazini na hivyo mdaiwa kutumia mwanya huo kutekeleza unyama

Ilielezwa kuwa siku hiyo mshtakiwa huyo alimfuata mfanyakazi wake chumbani huku akiwa amevaa taulo na pesa mkononi kiasi cha Sh20,000 akitaka kumpatia ili amkubalie kufanya naye mapenzi, jambo ambalo msichana huyo hakuliafiki na hivyo Danielic kumshika kwa nguvu na kumbaka.

“Baada ya kutekeleza kitendo hicho, mfanyakazi wake alimueleza mke wa mshtakiwa aliporejea kutoka kazini, lakini pia aliwasiliana na baba yake aishie mikoani na hata kuwaeleza rafiki zake waishio kwenye eneo hilo ambao walilivalia njuga suala hilo na kuripoti kituo cha polisi,” amesema Hakimu kibona.

Amesema kuwa baada ya taarifa kufika polisi msako ulianza na kwamba mshitakiwa alikimbilia mkoani Dodoma, hata hivyo alikamatwa na Polisi Juni 9, 2023 na hivyo kufikishishwa mahakamani kuendelea na kesi hiyo.

Imeelezwa kuwa mahakama hiyo ilifikia hatua ya kumhukumu adhabu hiyo baada ya kuridhishwa pasipo na shaka na ushahidi uliotolewa na daktari na mwathirika wa tukio hilo, huku mshitakiwa akijitetea kuwa siku ya tukio hilo hakuwepo nyumbani ingawa utetezi wake huo haukumnusuru na adhabu hiyo ya miaka 30 jela.

MWANANCHI
 
Usilazimishe mapenzi kwa mwanamke yeyote akisema hataki au hata kukuzungusha achana nae. Utapata wa kwako ikishindikana kwa wakati unaotaka wewe, nenda kwa madada poa maliza haja zako huko na maisha yataendelea kwa uzuri kabisa
 
Ko ulitaka afungwe mwezi mmoja.
Mwezi mmoja, Hapana.

Angekula miaka 3 au 5 , miaka 30 hapo ukute plate number yake inacheza 40+ ukiweka hiyo 30+ si atatoka jela akiwa antembelea mkongojo, upande WA Pili bado anafamilia inamtegemea cha kusikitisha zaidi aliemrubuni utakuta aliishia la 7c . 🥴
 
Huu ni mchongo wa mke wa jamaa.
Ni dhairi jamaa aliwekewa mtego wa mkakati ambao kwa mazingira yake wadau walifahamu lazima anase.
Hakuna cha mtego wala nini, wengi wenu mmezoea kuwanyanyasa na kuwadhulumu kingono watoto wadogo hasa mahousegirls.

Tafuta jimama achana na watoto wadogo utafungwa sana mpaka uchanganyikiwe.
 
Hatari Sana, hapo anatoka jela akiwa mstaafu 🥴
Nikishinda urais 2025 nitamtoa kwa msamaha, maana mm sijaona kosa lake huyo mwanaume.

Kwan huyo mwanaume kaondoka na kiungo cha huyo binti? Au jamaa amekiziba hicho kiungo?

Kwann jamaa achezee mvua zote hizo wakati binti akiendelea kuwapa wahuni wengine bila shida?

Nikipata urais 2025 nitamuachia huru huyo jamaa
 
Back
Top Bottom