Afungwa miaka 30 kwa kosa la kuingilia kinyume na maumbile

Afungwa miaka 30 kwa kosa la kuingilia kinyume na maumbile

Huko inabidi woteeee wafungwe.maana inaeleweka
 
Huko ni kama kumtoa Samaki kutoka bahari moja na kumtupa bahari nyingine! Kwa maswala ya Ushoga Zanzibar, maisha ya gerezani hayafofautiani na maisha ya uraiani!
Ndiyo kwanza nasikia kesi kama hii Zanzibar! Sijui kesi ya namna hii ilikatwa lini Zanzibar!
Hata huyo nadhani alikosa fedha ya kuhonga wazazi wa mtoto ili kumaliza mambo kimyakimya!
Kwa Zanzibar bado hakuna Mahakama ilichofanya!
 
Mahakama ya Mkoa wa Vuga, leo tarehe 31/10/2023 imemhukumu mshtakiwa MOH'D ALI HASSAN (35) Mkazi wa Jumbi Uwandani Unguja kutumikia kifungo cha miaka 30 Chuo cha Mafunzo (jela) kwa kosa la Kuingilia kinyume na maumbile.

Awali mshtakiwa huyo alimuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 06 jambo ambalo ni kosa, kinyume na kifungu cha sheria 133 (a) cha sheria ya adhabu namba 6/2018 Sheria ya Zanzibar.

Akisoma maelezo ya hukumu hiyo, Hakimu wa mahakama hiyo Mhe. TAKI ABDALLAH amesema Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama ambao haukuwa na chembe ya shaka ambapo umemtia hatiani mtuhumiwa kwa makosa hayo.

Jumla ya mashahidi watano (05) walitoa ushahidi mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani tarehe 21/08/2023 ambapo ilipewa kesi namba 127/2023.
Sasa Unguja si ipo Zanzibar?

Kwani hilo ni jambo la ajabu kwa huko Zanzibar?

Huyo ataachiwa tu, wameshazoea
 
Mkuu kosa halilipwi kwa kosa!

Maw ni mfano wa wazazi wakikuwa watoto wanagombana, utasikia: 'mpige na wewe'!
Badala ya kuwaamua, yeye anaogeza wigo wa tatizo!

Ingelikuwa ni hukumu za kibabe hivyo, basi wezi wangelihukumiwa kuibiwa, wachawi wangelihukumiwa kurogwa, wanaume wazinzi, wangelihukumiwa kuziniwa wake zao nk nk na dunia pasingelikuwa ni mahali salama tena pa kuishi.
 
Back
Top Bottom