Afungwa miaka miwili kwa kutamka "Bismilallahi" huku akila nyama ya nguruwe

Afungwa miaka miwili kwa kutamka "Bismilallahi" huku akila nyama ya nguruwe

Kazi ipo nakwambia
Unajua shida ipo hivi hawa watu wamekremu maisha hawajajua nini maana ya kiarabu , maneno mengi ya kiarabu sio ya kislamu ila kwa maana mtume wao katumia lugha hiyo ndio wa mekremu kuwa ndio maneno ya dini yao . Hata kuvaa kanzu wameweka ni kislam tena kuvaa ijabu ni kislamu ila nikiarabu tokea mavazi,lugha na kila kitu
 
UCHOCHEZI wa kueneza chuki dhidi ya Waislamu

Indonesia yote Waislamu. Sasa nani kachochewa kumchukia nani ???

UCHOCHEZI limebaki kuwa kosa nchi za third world tu.

Wakili Maalum Jack Smith alikataa kumshitaki Rais Trump kosa la KUCHOCHEA wapinga matokeo ya uchaguzi kwenda kuvamia ofisi za bunge kinyume na ushauri wa Kamati ya Uchunguzi ya Bunge. Aijua wangefanana na third world...
 
Masheikh wa huko Ibumu jioni kwny Ulanzi wanakanyaga km kawa Ijumaa waenda zuia waumin wasile
FB_IMG_16946101095982358.jpg
 
Staa wa TikTok kutoka nchini Indonesia, Lina Mukherjee amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na video aliyo-post inayomuonesha akisema neno linalotumiwa na Waislamu la ‘Bismillah’ kabla ya kula nyama ya nguruwe, jambo ambalo limelaaniwa vikali nchini humo.

Neno hilo hutumiwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanapoanza Dua, kula au shughuli mbalimbali wakimaanisha wanaanza ‘Kwa jina la Mungu/Allah’, ambapo katika video hiyo, Lina alionekana akisema Bismillah kabla ya kula chakula kisha akaanza kula nyama ya nguruwe ambayo kwa mafundisho ya Dini hiyo, ni kitu kilichopigwa marufuku (Haram).

Lina aliripotiwa na Jirani yake na video hiyo imekusanya mamilioni ya Watu waliotazama mtandaoni, amepatikana na hatia ya 'kueneza habari zinazolenga kuchochea chuki dhidi ya Watu wa Dini na makundi maalum' katika Mahakama moja iliyopo Mji wa Palembang nchini Indonesia.

Mukherjee, ambaye anasema yeye ni Muumini wa Dini ya Kiislamu pia amepigwa faini ya Rupiah milioni 250 (Tsh Mil 40), Indonesia ndio Taifa kubwa zaidi lenye Waislamu wengi duniani na lina sheria kali dhidi ya makosa ya kukiuka mafundisho ya Dini hiyo
huyo dada ni mwarabu ila sio muisilamu?

hebu saidi kidogo hivi angesemaje kwa lugha ya kiarabu kwa mfano?
 
Back
Top Bottom