SoC01 Afya ya akili mtaji kwa vijana

SoC01 Afya ya akili mtaji kwa vijana

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Sep 8, 2021
Posts
55
Reaction score
78
Afya ya akili ndio msingi wa maendeleo kwa kijana yeyote mwenye chachu yakuweza kufanikiwa au kufikia malengo fulani ambayo amejiwekea. Katika kipindi cha ujana vipo vingi ambavyo kama vijana tumekua tukivifanya wenda tukifahamu madhara ya tukifanyacho au pengine hatukuwa na ufahamu juu ya kitendo tukifanyacho lakini baadhi ya vitendo hivyo moja kwa moja vina athiri afya ya akili zetu.

Toka miaka ya 80 m sasa biashara ya video za ngono imezidi kushamiri duniani kote ikichochewa na ukuaji wa tehama.

Kutokana na biashara hii kumiliki asilimia 75% ya machapisho yote ya mitandaoni hivyo ni rahisi kwa vijana ambao ndio watumiaji wa mitandao hii kujihusisha na biashara hii ikiwa ni kwa kutazama au kushiriki moja kwa moja katika uandaaji wa machapisho haya katika mitandao.

Kwanza kabisa kama ilivyo urahibu wa madawa na vilevi machapisho haya yanaweza kuleta urahibu kwa mtizamaji na ilivyo mbaya zaidi urahibu wa machapisho haya si rahisi kutambulika kama tayari ni muasirika wa machapisho ya ngono.

Pia machapisho haya uzaa tabia nyingine mbaya ambayo imekua ikikingiwa vifua na makampuni makubwa yanayojihusisha na uchapishaji wa video hizo kuwa hakuna madhara yoyote kwa dhumuni la kuendeleza kuuza machapisho hayo hivyo wengi wa vijana wanaotizama machapisho haya hujiushisha na tabia ya kujichua ambayo uongezea athari katika afya ya akili.

Zifuatazo ni athari zinazotokea katika afya ya akili ya kijana alie athirika na urahibu wa machapisho ya ngono pamoja na kujichua.

AIBU (SHYNESS)
Kutoka na tabia hizi kuwa za sirini kijana ambaye ni mrahibu au anaejihusisha na tabia hizi ugubikwa na aibu wakati wote ata sehemu ambazo si zakuona aibu hii yote ni madhara yanayokwa yamesababishwa na machapisho na vitendo hivyo katika ubongo kwa muda mrefu

KUTOWEZA KUJICHANGANYA NA JAMII ( Social anxiety)
Hii ni hofu ya kukutana na watu wapya au kushindwa kujumuika na jamii kwa namna moja au nyingne ambayo hali hii inatengenezwa katika akili ya muathirika kuwa awezi kujichnganya na watu wengine na muda mwingi hutamani kuwa pekea yake na kuweza kutizama machapisho haya na kufanya kitendo cha kujichuwa.

Msongo (Depression)
Vijana wanaotizama machapisho haya kwa muda mrefu na wanaojihushisha na vitendo vya kujichua ugubikwa na msongo wa mawazo mda wote hali hii utokana na ubadilikaji wa mfumo wa ubongo Internet Pornography and the Emerging Science of Addiction Your Brain on Porn: Internet Pornography and the Emerging Science of Addiction - Google Search

KUPUNGUA KWA HESHIMA (Low self respect)
Kutokana na picha hizi kujirudia kichwani kwa muathirika kila wakati hata wakati ambao hatizami muathirika utizama picha hizi juu ya watu wote anaowatizama hivyo kushusha heshima yake kwa jinsia tafauti ambayo ufanya kwa mwenye dharau au kutokuheshimu wengine

KUPOTEZA KUMBUKUMBU (Brain fog)
Watizamaji wa video hizi ukumbwa na tatizo la kupoteza kumbukumbua kutokana na mfumo wa ubongo kufanya kazi katika kufikiri juu ya video hizo za ngono hivyo kupuuza vitu vingne vinavyoendelea kila siku na kufanya kusahau vitu vya msingi vinavyoendelea kitika maisha ya kila siku

KUKOSA FURAHA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU
Ubongo wetu umetengenezwa kwa chemikali iitwayo dopamine ambayo ni chanzo kikuu cha kutupa furaha katika kila kitu tunachokifanya kila siku kama kuzungumza na watu kufikia marengo fulani lakini kutokana na chemikali hii kutumika kwa wingi wakati mfupi wa kutizama video hizi na kujichua hivyo muathirika hujikuta hana furaha na vingne vyote ambavyo uenda mwanzo kabla ya urahibu huu vilikwa vikmpa furaha kama vule kusikiliza mziki ama kuangalia kupata kiasi fulani cha fedha hivyo ubongo unaiti chemikali nyingi zaidi ili uweze kupata furaha ya maisha na kemikalj hii tayari inakwa imetumika katika kujichua na kutizama machapisho ya ngono

UPWEKE (Loneliness)
muathirika hujiisi mwenye furaha tu pale anapotizama machapisho haya na kujichua pindi anapokwa hajafanya kitendo hiki hujiisi mpweke na asiye hitajika katika jamii lakini si kweli yote hii ni madhara yalioletwa baada ya kupata uathirika wa machapicho na vitendo vya kujichua

KUPOTEZA SHAHUKU KATIKA TENDO LA NDOA HALISIA
Ubongo wa muathirika wa machapisho haya na kujichua hufikia hatua na kukosa hamu ya kufanya tende la ndoa au kufanya na kukosa furaha alisia ambayo unatakiwa kuipata hii yote ni baada ya ubongo wa muathirika kuwa amezoea kutizama machapisho na kujichua hvyo hupoteza shahuku kuwa kitendo iko anaweza kukipata kwa jinsia yake tofauti na kuamini kuwa anaweza kujiburudisha mwenywe kupitia kujichua na kutizama machapisho hayo.

Jamii kubwa kutoka ulaya na mataifa mbalimbali ya Amerika yameanzisha mjadala mkubwa na unaoenea kwa kasi kubwa juu ya upingaji na uchapishaji wa maudhui haya ya ngono na vitendo vya vijana kujichua huku vijikita kuwalinda zaidi kuonesha madhara ya afya ya akili kwa kijana mwenye urahibu huu ambao hauonekani kama una madhara katika jamii ya leo Je ni kipi tufanye ili tuweze kuliondoa tatizo hili katika jamii yetu ya kitanzania.

Yapo madhara mengi ambayo yatamkuta muathirika wa machapisho haya na kujichua sasa tutizame ni kipi kifanyike ili tuweze vijana na urahibu huu mbaya ambao unakua kwa kasi sasa, kwanza kabisa naunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita kwa kufungia mitandao yote inayochapisha machapisho haya ya ngono hii itafanya waathirika kukosa maudhui haya hivyo itawasaidia kujihusisha na vitendo hivyo pamoja na kuto kuzalisha waathirika wapya wa urahibu huu.

Elimu juu ya madhara ya machapisho na vitendo vya kujichua inatakiwa itolewe kwa wingi zaidi juu ya vijana hii itasaidia vijana wengi kutambua ni wapi wataenda au utakuwa mwisho wao kama watachagua kutizama au kuendelea na machapisho haya na vitendo vya kujichua

Tukiweza kufanya haya tutaweza kutengeneza taifa la vijana wenye afya nzuri ya akili ambao watakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya taifa letu
 
Upvote 2
Back
Top Bottom