Afya ya meno: Wenye meno meupe yanayong'ara mnafanyaje jamani tupeane maujanja, nina hali mbaya

Afya ya meno: Wenye meno meupe yanayong'ara mnafanyaje jamani tupeane maujanja, nina hali mbaya

Meno unayasafisha kwa utulivu.

Utumie muda mrefu kuosha meno.

Let's say asubuhi,
weka dawa kwa mswaki, pitisha kwanza maji mdomoni, sukutua kidogo kisha tema,

Ile dawa kwenye mswaki, weka maji kidogo.

Anza kusukutua meno, hakikisha hadi ndani meno umesukutua, kwa utulivu chukua muda mrefu kidogo .

Mwisho pitisha mswaki kwenye ulimi, yaani vuta ulimi nje kisha pitisha mswaki.

Fanya hivyo asubuhi na wakati wa kulala

NB unaweza enda hapo Regency hospital kuosha meno pia, bima inakubalika
Ukitia maji kwenye dawa ya meno basi unaipunguza nguvu yake ya usafishaji
 
Meno yaliyoharibika yenye rangi kama ya dhahabuni mtaji ya cheki Yale ya aseki.
 
Na je wale wenye tatizo la kutokwa damu upande mmoja wa fizi wakati wa kuswaki inakuwaje tiba zao?
 
Kuna utaalamu wa kuyang'arisha mfano Arusha kuna clinic nyingi za kung'arisha meno.
Maji ya arusha na mkoa wa kilimanjaro yana kiwango kikubwa sana cha fluoride per mililiters kitu kinachosababisha tatizo lijulikanalo kama dental fluorosis ndo kule meno yanakuwa kama yameungua .

Hii pia inategemeana na eneo ambalo upo mfano kuna maeneo arusha watu wana meno meupe mno hawa ni wale ambao wanakaa maeneo ambayo yapo mbali na mlima meru .

Dental fluorosis pia ina stages zake mfano ikiwa stage ya awali basi hayo meno yanaweza kusafishika vizuri ikifikia late stage basi ni ngumu kuwa reversed na damage yake ni permenent.

Mbaya zaidi ikizidi sana basi inaathiri hadi mifupa (skeletal fluorosis) mfano watu wanaoishi kata ya maji ya chai arusha .
 
Tumia banking powder na ndimu,,, au tumia majivu Mzee wangu Kila baada ya mlo utakuja kushukuru achana na madawa ya kolgate sijui majitu ni gan
 
Dawa nzuri.

Saga Mkaa na majivu weka chumvi hasa ya mawe kidogo.
Tumia kijiti cha Muarobaini.

Au tumia Baking powder kwa kiswaki.

Ukishindwa hapo juu tumia Karafuu.

ACHANA NA MA WHITE DENT YAMEPITWA NA WAKATI.
 
Tumia banking powder na ndimu,,, au tumia majivu Mzee wangu Kila baada ya mlo utakuja kushukuru achana na madawa ya kolgate sijui majitu ni gan
Mchanganyiko wa baking soda na ndimu/limao ni hatari na utumiaji wa mara Kwa mara ni hatari zaidi Kwa afya ya meno.

Mnaharibu enamel kwenye meno na kujiletea matatizo makubwa zaidi Kwa ajili ya kutafuta urembo.
 
Tumia mswaki wa mti achana na dawa hizo nyingi ni fake kwa umasikini wa huko
Chukua mkaa saga mpaka uwe Unga kabisa hatafu pigia mswaki wa mti
 
Zamani kipindi mi mtoto,kule kijijini,tulikua tunatumia miti flani inaitwa MIDAA,yaani ukiswakia meno yanakua meupe kinoma..... I miss those old days.
 
Back
Top Bottom