Maji ya arusha na mkoa wa kilimanjaro yana kiwango kikubwa sana cha fluoride per mililiters kitu kinachosababisha tatizo lijulikanalo kama dental fluorosis ndo kule meno yanakuwa kama yameungua .
Hii pia inategemeana na eneo ambalo upo mfano kuna maeneo arusha watu wana meno meupe mno hawa ni wale ambao wanakaa maeneo ambayo yapo mbali na mlima meru .
Dental fluorosis pia ina stages zake mfano ikiwa stage ya awali basi hayo meno yanaweza kusafishika vizuri ikifikia late stage basi ni ngumu kuwa reversed na damage yake ni permenent.
Mbaya zaidi ikizidi sana basi inaathiri hadi mifupa (skeletal fluorosis) mfano watu wanaoishi kata ya maji ya chai arusha .