KERO Responded Afya za Wananchi Kata Nyaishozi-Karagwe zipo hatarini, wanatumia maji ya madimbwi

KERO Responded Afya za Wananchi Kata Nyaishozi-Karagwe zipo hatarini, wanatumia maji ya madimbwi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa vitongoji vya Kikungili, Omukajiji, Rushanje na Rwandalo Kata ya Nyaishozi, wilayani Karagwe mkoani Kagera, tunakabiliwa wanalazimika kutumia maji yasiyo safi na salama kutoka kwenye madimbwi kwa matumizi ya nyumbani, kufuatia kuharibika kwa kisima walichokuwa wakikitumia takribani miaka mitatu.
photo_2026-04-13_18-45-39.jpg

photo_2026-04-13_18-45-35.jpg
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameeleza kuwa wanalazimika kutumia maji hayo ya dimbwi ambayo sio salama kutokana na kutokuwa na mbadala wake hivyo kuiomba serikali kuwasaidia kupata maji safi na salama .

“Kwakweli tuna shida ya maji tunachota maji haya ya dimbwi ambayo sio safi kwahiyo tunaomba msaada ili tupate maji mazuri na masafi tunashida kubwa tunaomba watuangalie” alieza mmoja ya wananchi

Naye Mwananchi mwingine anaeleza kuwa dimbwi hilo ni hatarishi kwa wakina mama na watoto ambao mara kadhaa wamekuwa wakidumbukia katika dimbwi hilo.

“Tunayo changamoto ya maji katika maeneo haya tunatumia dimbwi hili ambalo wakati mwingine wakina mama na watoto huwa wanaanguka katika dimbwi hili kwahiyo tunaiomba serikali iweze kutungalia katika tatizo hili la maji”
photo_2026-04-13_18-45-26.jpg

photo_2026-04-13_18-45-21.jpg

photo_2026-04-13_18-45-15.jpg
Pia Mwanachi mwingine Mkazi wa Kitongoji Rushanje amesema kuwa awali walikuwa wanatumia kisima ambacho kwa sasa kimeharibika kwa muda mrefu zaidi ya miaka mitatu nyuma na kuiomba serikali kuwatengenezea kisima hicho.

“Tulikuwa tunatumia kisima na baada ya kuharibika tukachimba dimbwi ambalo nalo maji yake sio salama lakini kwa sababu ya uhaba wa maji tunayatumia haya hali inayohatarisha afya zetu kwasababu watu wengi wanaugua matumbo kwa sababu ya haya maj

Kufuatia hali hiyo wametoa wito kwa serikali kukamilisha haraka kwa mradi wa maji wa miji 28 wa Rwakajunju ili kuleta suluhu ya muda mrefu.

Ikumbukwe akizungumzia mradi huo Bungeni karibuni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew amesema kuwa mradi wa Rwakajuju kwa sasa umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake.

“Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi miwili ya maji katika mji wa Kayanga wilayani Karagwe ukiwemo mradi wa maji wa Rwakajunju unaotekelezwa kwa thamani ya shilingi bilioni 64.3 sambamba na mradi wa usambazaji wa maji wa katika mji wa Kayanga unaogharimu shilingi bilioni 1.3, mheshimiwa Naibu spika utekelezaji wa miradi hii umefikia asilimia 70”alisema Kundo Mathew

Kukamilika kwa miradi hiyo inatarajiwa kuwanufaisha wananchi wapatao 356,790 wa wilaya ya Karagwe hali itakayo wasaidia wananchi wilayani kuondokana na adha ya kutumia maji ambayo sio safi na salama.

Taarifa za awali inadaiwa ulianza kutekelezwa tangu Aprili Mwaka 2023 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Desember 2025.

Majibu ya Serikali ~ RUWASA: Kata ya Nyaishozi na Kitongoji cha Akajiji (Kagera) wanapata maji, pampu ilikatika, imerekebishwa
 
Mradi wa Rwakajunju mbona nasikia unapita pande hizo
 
Back
Top Bottom